juu

Saturday 15 February 2020

Mbinu za Kumchagua Mwenza Ambaye Hawezi Kukutelekeza



Chagua mtu mwenye msimamo
Muda aliotumia mpenzi wako kudumu katika uhusiano wake uliopita unaweza kukupa ishara ya nguvu ya mtu kudumu na wewe; Unaweza kutumia njia hii kama kipimo cha matarajio ya uhusiano wenu mpya. Ikiwa, kwa mfano, mwenza wako anayetarajiwa alikuwa na mahusiano kadhaa ambayo yalidumu kwa muda mrefu takribani yenye utulivu wa miaka miwili au zaidi, hii inaelezea uwezo wake mzuri wa kujitoa. Kwa upande mwingine, mtu ambaye ana historia ya uhusiano usio thabiti, wa muda mfupi lazima aonekane kama hatari hata kama atatoa kile kinachoonekana kuwa ni sababu za halali. Kamwe haiwezi kuwa kosa la mtu mwingine kila mara anapovunja uhusiano.

Chagua mtu mwenye mfano mzuri:
Kwa mfano, kuchagua mtu kutoka nyumba iliyovunjika, sio aibu. Lakini unaweza kutaka kujua jinsi mtu huyo alivyotatua maumivu hayo. Baadhi ya watu huwa wamejifunza kuwa njia bora ya kutatua tatizo ni kukata tamaa. Tumaini kuwa mtu huyo amejifunza na kutofautisha mambo mengi kutoka kwenye makosa ya wazazi wake na yupo tayari kuonesha matokeo chanya katika maisha yake.

Chagua mtu anayeweza kustahimili msongo wa mawazo:
Watu ambao wanaweza kustahimili matatizo kwa usahihi watakuwa na uwezo zaidi wa kubaki upande wako hata wakati unapopitia mambo magumu. Watu hawa wanaelewa dhana ya kujitolea, uaminifu, na kazi ya pamoja. Watu wenye wasiwasi sana wanaweza kuwa na hofu hasa kwa sababu ya tabia ya kutambua hali yenye shida ambayo ni mbaya sana kuliko ilivyo kawaida.

Chagua mtu mwenye huruma:
Mtu anayeelewa maumivu yako na anayeweza kufanya jitihada za kukuweka sawa pindi unapokuwa katika kipindi kigumu. Chagua mtu mwenye fadhila na mwenye ukarimu; mtu ambaye ana moyo wa huruma, na asiyeogopa kuionesha huruma yake kwa vitendo.

Chagua mtu ambaye haogopi kufunguka:
Amini nakuambia, ni jambo salama sana kuwa na mtu asiye na tabia ya kuyaficha maumivu yake moyoni mwake. Na mojawapo ya hali inayoogopesha zaidi katika mapenzi ni ile hali ya kutoweza kujua anachokiwaza mpenzi wako hasa kuhusu wewe. Watu ambao hawako tayari kueleza kinachowasibu au dukuduku zao hujitengenezea bomu la matatizo bila kujijua, bomu ambalo hata lisipolipuka leo linaweza kulipuka muda wowote siku moja bila hata kujua sababu; unaweza kuwa vizuri sana. Naamini umewahi kusikia mikasa ya watu ambao mapenzi yao yaliisha bila ya wao kutarajia, mume au mke anarejea nyumbani kutoka kazini anakuta mwenza wake amekusanya kilicho chake na kuondoka.

Chagua mtu ambaye anataka kuwa karibu na wewe, kimwili na kihisia:
Chagua mtu anayependa kuwa karibu kihisia na kimwili; mtu ambaye hachoki kuzungushia mkono wake shingoni, begani, kiunoni au kushikilia mkono wako; mtu ambaye anapenda kukubusu. Kugusa kunaweza kuongeza radha yamapenzi katika uhusiano. Na kwa kuchagua mtu ambaye anaonekana kufurahia kuzungumza na wewe. Mtu ambaye hapendi ujisikie mpweke.

Chagua mtu ambaye ana maadili mema na mnayeshabihiana:
Unaweza kupuuzia na kuchukulia kuwa hili ni jambo dogo tena halina maana ya msingi, lakini nakuambia kuwa mtu asiyependezwa na yale unayofurahia anaweza kuishiia kuvuna janga la upweke utakao pelekea kutelekezwa. Na hatimaye wanaweza kumtafuta mtu mwingine ambaye wanaendana naye. Ikiwa wewe ni mkimbiaji, tafuta mkimbiaji; ikiwa wewe ni mwandaaji mziki, tafuta mtu anayevutiwa na muziki; ikiwa wewe ni mtu wa ibada, mtafute mtu anayependa ibada pia!.
Kufuata ushauri wangu sio njia ya uhakika kwamba hamtatengana. Kwa hakika utakuwa na mambo mengine machache ya kuyazingatia kama; kuwa na tabia njema kwa mpenzi wako, kuwa na heshima, na uwe mwepesi wa kutatua matatizo
Share:

Mambo 2 Muhimu Ya Kumfanyia Mpenzi Wako Pindi Mnapo Maliza Kufanya Mapenzi Soma Hapa



Mambo 2 Muhimu Ya Kumfanyia Mpenzi Wako Pindi Mnapo Maliza Kufanya Mapenzi Soma Hapa


Wanaume na wanawake walio wengi pindi wanapomaliza kufanya mambo yao na wapenzi wao chumbani hujikuta wakikaa pembeni bila kuzingatia vitu muhimu vinavyotakiwa kufanywa pindi wanapomaliza kuse*x.

VIFUATAVYO NI VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA PINDI UNAPOMALIZA TENDO NA MPENZI WAKO CHUMBANI:

1. MFUTE FUTE MPENZI WAKO

Mpenzi msomaji faham kuwa unapokwenda kufanya mapenzi na mpenzi wako hakikisha unakwenda ukiwa na kitambaa kisafi (LESO) hiki kitambaa unakuwa nacho maalum kwa ajili ya kumfuta mpenzi wako pindi mnapomaliza kufanya mapenzi.

Hakikisha unapomaliza kusex na mpenzi wako unamfuta jasho mwilini na pitisha kitambaa chako katika sehemu zake za siri mfute fute taratibu mpenzi wako usikubali mpenzi wako ajifute yeye mwenyewe na usisubiri akuambie umfute.

2. MUULIZE MPENZI WAKO KAMA KARIDHIKA AU BADO ANAHITAJI KUENDELEA:

Wapenzi waliowengi wanapomaliza kufanya mapenzi huwa hawaulizani swali kama hili wengi hujistukia na kuamua kuvaa nguo zao na kuondoka hili ni kosa kubwa, siku zote katika mapenzi mwanaume huwah kufika kileleni kuliko mwanamke hivyo mwanaume hujikuta ameisharidhika ikiwa mwanamke hajaridhika hivyo nivizuri pindi unapojiona umeridhika muulize na mpenzi wako kama nae karidhika akikuambia tayari basi mnaweza kuishia hapo au akikwambia bado ni wajibu wako wewe kuendelea tena kufanya mapenzi mpaka nayeye aridhike.

Lakini kunatatizo moja hujitokeza sana kwa upande wa wanawake wanawake walio wengi wanapoulizwa na wapenzi wao kama wameridhika huwajibu wapenzi wao “Ndio nimeridhika” lakini kumbe bado hawajaridhika.

Napenda niwaambie wanawake wote wenye mtindo huu kuwa si mzuri kuweni wakweli pindi unapoona hujaridhika usimfiche mpenzi wako mwambie ukweli kwani ni haki yako kuridhishwa.
Share:

Fahamu: Mwanamke Ukiwa na Sifa Hizi Ni Lazima Utaachwa Tu





Bila kuwachosha nizame moja kwa moja kwenye mada yetu hii ambayo inazungumzia mambo 12 wasiyoyapenda wanaume kwa wapenzi au wake zao.

WIVU WA KUPINDUKIA
Mwanamke mwenye wivu wa kupindukia humfanya mwanaume kukosa amani kwani hata awapo kazini kwake mwanamke atataka kumfuatilia na kumnyima uhuru.

Hawa wenye tatizo hili huachwa na wanaume wao haraka kwani wengi hawapendi kuonewa wivu wa hivyo, wengine huuita wivu wa kijinga.

KUJIPAMBA KUPITILIZA
Mwanamke kama mwanamke ni mapambo na ili awe mwanamke anao ulazima wa kuhakikisha anaonekana smati kwa kujipamba lakini si kama wafanyavyo wanawake wa siku hizi.

Wanaume wengi wamejikuta wanachukizwa na hali ya mwanamke kujipamba kupitiliza.

Yaani unakuta mwanamke anajipamba utadhani siku hiyo ni siku yake ya kufunga ndoa, hilo ni tatizo na husababisha hata mwanaume kuogopa kuongozana naye.

Sasa je, kama unatoka na mume au mpenzi wako, unajipamba hivyo kumfurahisha nani hasa? Mbona ukiwa nyumbani unakuwa wa kawaida tu?

MATUMIZI MAKUBWA YA FEDHA
Mwanamke mwenye matumizi makubwa ya fedha ambaye hafikirii kesho itakuwaje ni adui mkubwa wa mwanaume.

Hata kama atakuwa anakupenda kiasi gani, atakuvumilia siku za mwanzo lakini kadiri mnavyokwenda atajitoa kwako taratibu. Hii ni kwa sababu mwanaume atahisi siku akija kuwa hana kitu anaweza kuibiwa na wenye fedha.

MUONGEAJI SANA
Mwanamke muongeaji sana asiyekuwa na staha, mwanamke ambaye hawezi kumvumilia mwanaume pale anapokuwa akimsema kwa jambo f’lani kwa nia ya kutaka maelewano ni tatizo.

Namzungumzia yule ambaye muda wote anataka kushindana na mume/ mpenzi wake katika kuongea, yaani kuonesha kuwa hajakosea, anaonewa au na yeye yumo kwenye kuongea, huyu hawezi kumshika mtu wake.

Mwanamke anayeijenga ndoa yake anatakiwa kuwa chini pale mwanaume anapokuwa anapaza sauti, akishapoa na wote mmepoa. kama una dukuduku lako ongea naye taratibu.

Haiwezekani mume na mke kuwa juu hasa mnapokuwa kwenye mgogoro, inatakiwa mwanamke kumsoma mume wake au mpenzi wake kwa wakati huo.
Share:

Tuesday 4 February 2020

Mwanaume epuka kumwambia maneno haya mpenzi wako

Wanaume wengi hudhani ni vigumu sana kuwafurahisha wanawake lakini si hivyo, ni jambo rahisi, matendo yako kwenye mambo madogo madogo ya kimapenzi na kuchunga ulimi wako vinaweza kumfanya mwanamke wako kuwa na furaha kupita kiasi na kama yeye akiwa na furaha basi ndugu yangu maisha yako yatakua na amani na wewe utakua na furaha.

Kwa kawaida wanaume kuna vitu tunaviona vya kawaida sana na vya kipuuzi lakini kwa wanawake ni vitu muhimu na tunatakiwa kuwa makini tunapovizungumzia. Katika kukusaidia tu ndugu yangu katika mahusiano hapa nimekuandalia mambo matano ambayo unapaswa kuwa makini unapoyaongelea, hizi ni kauli tano ambazo mwanaume ni dhambi kabisa kumuambia mwanamke.

1. Hiyo Nguo imekutoa vizuri imefanya makalio yako yaonekane makubwa; Ingawa wanwake hupenda sana kusifiwa na kauli yako ilianza vizuri lakini umemalizia vibaya kumuambia ‘imefanya makalio yako yawe makubwa’ ni sawa na kumuambia umepigwa pasi na hata kama hatakujibu utamuumiza mbaya na kumuondolea kujiamini.

Sio kwamba alikuwa hajui kuwa makalio yake si ya mwendo kasi lakini kwa kumuambia wewe tena ukasema kapendeza kwasababu yanaonekana makubwa basi unamuambia kua unapenda makalio makubwa na kipindi chote hicho mlivyokuwa naye basi ulikua unavumilia tu na hufurahii. Ndugu yangu katika mahusiano achana na hiyo kauli, ishia tu kumuambia umependeza basi!

2. Kweli kabisa anza Diet; Hapa ni yeye kaja kukuambia kuwa anajihisi mnene na anataka kuanza diet ili apungue, ndugu yangu acha kujifanya kiherehere kuwa eti kweli anahitaji kupungua, hata kama unaona anahitaji kupungua mwanangu wewe sema tu unavutiwa hivyo hivyo na tena ukimshika shika kumuambia ndiyo unavyopenda mwili unakua na pakushika sio mifupa mitupu.

Akizidi kusisitiza wewe muambie hata kama anafanya hiyo diet basi asipungue sana. Hapo utakua umemuambia kuwa unampenda jinsi alivyo na unafurahia vile alivyo. Kumuambia kweli kabisa unatakiwa kufanya dieti ni sawa na kumuambia kuwa wewe ni mnene na siku nyingi nilitamani upungue sifurahii kabisa ulivyo. Kuwa makini na muonekano wa mwanamke, utamnyima raha na akikosa raha hutakuwa na raha.

3. Kwanini usiwe kama yule rafiki yako; Bila kujali unatolea mfano kitu gani lakini kamwe usimsifie rafiki yake na kumkosoa yeye hata kama ni kwa utani. Usiseme kwanini usingenunua rangi kama ya flani, au kwanini huwi mpole kama flani na mambo kama hayo, kutole amfano kuwa anatakiwa kua kama flani inamaana unampenda na kumfurahia flani kuliko yeye. Hata kama nia yako si hiyo lakini acha kumlinganisha na rafiki zake au wanawake wengine.

4. Kweli alipendeza…; Mmetoka out mlienda kwanye sherehe au sehemu na marafiki zake na wakati mnarudi au mko nyumbani anaanza kumsifia rafiki yake mmoja alivyokua kapendeza, ndugu yangu huo ni mtego usiongeze neno hata kama uliona kweli kapendeza. Kumuambia kweli alipendeza utakua umefanya makosa matatu, kosa la kwanza ulikuwa unamuangalia sana rafiki yake labda umemtamani ndiyo maana ulijua kapendeza.Kosa la pili umemuambia yeye hakupendeza kwani utakuwa labda ulimlinganisha na kosa la tatu hujali hisia zake unamuwaza huyo aloambiwa kapendeza. Msikilize tu na kama utachangia sema tu mbona kawaida tu hata hukuona kipya. Kwanini utafute matatizo ya bure muhimu ni usiponde sana kwani ukiponda zaidi atastuka unaongea vile ili kumfurahisha na si kweli, jibu kidogo kama vile hutaki na badilisha stori mara moja.

5. Hivi huwezi kunyamaza; Anaongea sana, analalamika sana lakini hupaswi kumuambia kua anaongea au kulalamika sana kwani utamfanya azidi kuongea sana na kulalamika kuwa unamuambia anaongea na kulalamika sana. Najua ushachanganyikiwa zaidi lakini ndivyo wanawake walivyo, hutoa stress zao kwa kuongea, ni njia ya kujitetea ni silaha ya mapambano kwao.

Kwa maana hiyo hata kama anaongea sana analalamika sana wewe umilia au jaribu kuzidi kumuonyesha mapenzi. Kulalamika kuwa anaonge ana kulalamika sana utampa kitu kingine cha kulalamika na utazidi kuchanganyikiwa zaidi kwani haitasaidia kumnyamazisha. Nikazi ya mwanaume kumpenda mwanamke bila kuuliza au kutaka kujua kwanini anampenda na wala usitake kumuelewa kwani kamwe hutamuelewa wewe mpende tu.
Share:

Tuambizane tu ukweli ili tupate kilicho bora katika mahusiano ya kimapenzi

Kwenye swala zima la mahusiano ya mapenzi pesa haina chochote cha kuthibitisha. Na anayetanguliza pesa mbele katika mapenzi hana upendo wala mapenzi ya kweli.

Wanawake
Usikimbilie kumpima imani mpenzi wako kwa kumuomba pesa ili ujue kama anakupenda au laa mwanaume ni kiumbe anayeweza kufanya kila unachotaka akamilishe malengo yake.
Be careful utachezewa na utatumika sana lakini kumpata wa kuishi naye forever hutapata.

Wanaume
Kumpatia pesa mpenzi wako kila akihitaji hakumfanyi yeye akuone ni kiasi gani unampenda ila huenda ukageuzwa kitega uchumi chake. Lugha ya mjini tunaita atm yake.

Unampomuapproach mwanamke epuka kumuonyesha maisha ambayo siyo level zako maana kama utampa pesa sana kabla ya kumuoa jiandae kufanya hivyo baada ya ndoa
Ukishindwa black brother huna ndoa tena, Wahenga wanasema "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo"

Nyote
Epuka kuweka mbele katika mahusiano vitu ambayo vinaisha na kupotea kabisa kama pesa, mali na mengine mengi maana yakiisha hayo yatatengeneza hatima ya mapenzi yenu..

Busara yangu/ ushauri
Katika mapenzi siku zote tanguliza moyo wako na hisia za kweli kwa uliye naye , mpe moyo wako na yeye akupe wake ila mambo mengine mungu atawapatia mbele kwa mbele.

Kama nilichosema haifai na kimekuudhi utanisamehe lakini nimeongea ukweli na mambo ambayo yemetawala sana kwenye mahusiano ya sasa hivi.
Share:

Maneno ambayo unapaswa kumwambia mpenzi wako ili kuongeza ladha katika mahusiano

Mapenzi yanayotawaliwa na maneno matamu hunawiri na kuchanua kama mmea uliopandwa kando ya mto. Hakika maneno mazuri husadifu mambo mengi mazuri baina yenu ikiwemo upendo, kujali, kuthamini, heshima, utii, upole, nidhamu, uaminifu, unyenyekevu, usikivu, ukarimu na faraja hivyo ni vema kuhakikisha kama kweli unampenda kinywa chako daima kimtolee lugha nzuri ya maneno matamu.

Weka desturi ya kusema mambo haya kwa mwenza wako hakika inazidisha furaha na amani kati yenu..

Nakupenda
Nakupenda ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mwenza wako. Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mwenza wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko pamoja.....```

Umependeza
Kama umekuwa kwenye ndoa kwa muda mrefu, ni rahisi kujisahau katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha mwenza wako kuwa anakuvutia. Kumjulisha kuwa ulivo vaa umependeza sana’ kutamfanya ajisikie vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye.

Samahani
Kila mtu hukosea wakati fulani. Wakati mwingine hujikuta tukiongea maneno kwa hasira na baadaye kugundua kuwa hatukuwa sahihi. Ubishi hauna nafasi kwenye ndoa ya wenye furaha, hivyo omba msamaha unapofanya kosa. Omba msamaha kwa kukasirika. Omba msamaha kwa kuumiza hisia za mwenza wako..```

Nilikuwa nakuwaza
Ni muhimu kumjulisha mwenza wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu moja. Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho kinakufanya umkumbuke, mjulishe...```

Siku yako ilikuaje?
Muulize masuala ambayo mwenza wako anakutana nayo katika shughuli zake kazi kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mwenza wako kushare sehemu zingine za maisha yake kutasaidia kuumuweka sawa.```

Napenda mawazo yako.
Mwambie mwenza wako kuwa unapenda mawazo yake. Mjulishe kuwa unaona ana akili, mcheshi, anajua kupenda na ana kipaji.```

Nakuunga mkono
Mpe moyo mwenza wako kwa kumjulisha kuwa unaunga mkono maamuzi yake. Unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kujaribu kumsaidia afanikishe malengo aliyojiwekea. Maisha yamejaa vikwazo vingi, na ile hisia kuwa una mtu mwingine upande wako zinaweza kukusaidia kuvivuka. Msiwe wanandoa tu, kuweni timu. Kumkumbusha mwenza wako kuwa upo nyuma yake kutaimarisha umoja wenu.

Hakuna kama wewe.
Mwenza wako anatakiwa kuwa rafiki yako. Kama hautaki kutembea naye, basi hamkupaswa kuwa pamoja. Mfanye mwenza wako ajue kuwa yeye ni bora na hakuna kama yeye.
Share:

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger