juu

Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Monday, 12 August 2019

Njia ya asili ya kujitibu tatizo la kuwashwa kwa ngozi ya mwili


Kuwashwa sehemu yoyote ya mwili inaweza kuwa ni matokeo ya tatizo fulani lililoko mwilini,kama vile mzio (allergy) minyoo.

Kwahiyo mwili unapowasha kunaweza kuwa ni dalili za ugonjwa unaohitaji kuchunguzwa na kutibiwa  badala ya kutafuta kutibu dalili za ugonjwa.

Pamoja na hayo, kuna baadhi ya tiba za kukabiliana na tatizo hilo, ambazo ni pamoja na soya, ndimu, komamanga , unga wa ngano pamoja na majani ya ngano, lakini katika tiba zote hizo leo hii tutaelezea hii tiba ya kutumia  unga wa ngano ambayo pengine inaweza kuwa ni rahisi kwa wengi.

Unachopaswa kufanya katika kutumia unga wa ngano kama tiba ni kupaka unga wa ngano sehemu zote za mwili zinazowasha na hakikisha unatumia tiba hii kwa muda wa siku 10.



Share:

Mchango wa marafiki katika maisha yako


Kuna aina mbili za marafiki ambao tunaishi nao katika maisha yetu ya kila siku.  Aina ya kwanza ni marafiki ambao ni wema na aina ya pili ni marafiki wabaya.

Tukianza na kuangalia aina hiyo  ya kwanza, marafiki wema  ni marafiki ambao ni watu ambao wana mawazo chanya katika kukushauri hata kutenda mambo mbalimbali yenye mchango mkubwa wa kuyabadili maisha yako kwa kiwango cha juu sana. Pia katika kundi hili la marafiki  wema ni wapo wachache sana.

 Aina ya pili, marafiki wabaya hawa ni  marafiki ambao ni watu ambao hawana msaada wowote katika safari yako ya mafanikio zaidi ya kukukatisha tamaa tu. Aina hii ya marafiki hawapo tayari kukusaidia katika shida bali wapo kwa ajili ya raha pekee.

Pamoja na hayo watu wengi tunafeli kimaisha hii ni kutokana na kufanya uchaguzi mbaya wa marafiki. Wengi wetu tunaambatana na marafiki wabaya hata sehemu ambazo hatustili kuishi na watu hao .

Vile vile wengi wetu tumekuwa tukiomba ushauri kwa watu ambao siyo sahihi hata kidogo. Kwa mfano leo hii tumeona marafiki wabaya huwa na mtazamo mmoja wa kushindwa kufikia malengo yao nay a watu wengine.
Tumekuwa tukishuhudia  baadhi ya wanafunzi ambao pindi waendapo  masomoni baada ya kufika huko wamekuwa  wakibadilika sana tabia zao, wengi wao wamekuwa na  tabia za ajabu sana, hii ni kutokana wamekutana na marafiki ambao sio sahihi kwao ni wao kutokana na ufinyu wa fikra walizonazo wamejiunga nao.

Tumeona baadhi ya vijana hao wamekuwa wakijingingiza kwenye wimbi la ulevi,  utumiaji wa madawa ya kulevya na hata kuuza miili yao hii ni kutokana watu hao wameshindwa kuchagua marafiki sahihi.

Achilia mbali wanafunzi, Wapo baadhi ya watu wameshindwa kuwa sehemu fulani kwa sababu ya marafiki walio nao. Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakipata baadhi ya mawazo mazuri yenye kuleta mapinduzi katika maisha yao na jamii kwa ujumla, ila wamekuwa wakiwashirikisha marafiki zao mawazo hayo kabla ya kuyaamua kuyafanyia kazi, na marafiki hao  wabaya walio nao baadala ya kuwapa ushauri mwema wamekuwa wanazidi kuwakatisha tamaa tu.

Neno haiwezikani ndilo linalowaongoza wao kwa silimia kubwa, Kwa mfano unaweza ukamshirikisha rafiki yako kuwa unataka kufanya biashara ya fulani. Baada ya kumwambia rafiki huyu uliyenaye utamsikia akisema Biashara hiyo haitatoka kwa sabubu fulani  naye anaifanya au fulani kaliteka soko la biahara hiyo, hivyo  wewe hatuweza ni bora utafute kitu kingine cha kufanya. Kwa kuwa na wewe muoga na unaamini katika maneno ya kuambiwa unajikuta unaacha. Kwa staili hiyo akama endapo hutaamua leo kubadilika ni kwamba neno mafanikio utaendelea kulisikia tu.

Hii ni kwa sababu ukichunguza kwa umakini juu ya marafiki wabaya huwa hawana sababu ya msingi ya jambo ambalo anakwambia kwa nini usifanye zaidi ya kukwambia usifanye tu.

Vile vile wapo baadhi ya marafiki ambao wao pia ukiwashirikisha jambo lako na wao huchukua jukumu la kuwashirikisha wengine. Marafiki wa aina hiyo hawafai hata kidogo.

Kimsingi ni kwamba watu wengi walio fanikiwa leo hii walichagua marafiki sahihi wa kuwashauri juu ya mambo yao. Hivyo na wewe chagua marafiki sahihi ambao unahisi wanamsaada mkubwa katika maisha yako, pia ukumbuke  msemo usemao ndege wafananao huruka pamoja hivyo ni wasaa wako mzuri wa kuchagua marafiki wema kwako. Marafiki wabaya ambao hawana mchango na msaada wowote juu ya maisha yao wafute na wala usijali watesema nini.

Marafiki hao wabaya wakianza kukuliza kwanini siku hizi umebadilika jibu la kuwajibu ni rahisi ni kwamba utawaambia "always forward, backward never" ikiwa na maana ya daima mbele, nyuma mwiko.
Chagua marafiki sahihi ambao wao ukiwaambia juu ya jambo lako zuri tegemea kupata majibu sahihi pia kwa kile ulichowashirikisha na sababu za msingi.

Pia kumbuka usemi usemao ya kwamba kila gumu unalokutana nalo mbele yako limebeba siri ya mafanikio yako, usinung'unike kutokana na magumu unayokutana nayo katika mizunguko yako lakini ifundishe akili yako, usingalie nani kasema nini? nani kasema kipi juu yako. Jambo la msingi ni fanya kazi kwa bidii zote na simamia mipango yako . Siku moja utakuwa mtu wa thamani sana mbele ya jamii.

Ndimi Ofisa Mipango na Maendeleo: Benson Chonya



Share:

Fahamu faida za kutumia alizeti kiafya


Alizeti ni moja kati ya mazao ambayo hupatikana hapa nchini katika baadhi ya mikoa ikiwemo Singida na Iringa. Zao la alizeti hutumika hasa kwa kuchuja mafuta yake ambayo hutumika sana kwa kupikia. Lakini alizeti zinapochunjwa hutoka uchafu, uchafu huu huitwa mashudu, ambayo ni mazuri sana kwa ajili ya mifugo. Kwa wale ambao ni wafugaji wenzangu nadhani hapa watakuwa wanaelewa vizuri nazungumzia nini hasa.

Naomba hapa nikuarike ili uweze kujifunza faida ya mbegu za alizeti kama ifutavyo; mbegu mbichi za alizeti ni tiba ya mishipa ya fahamu. mapafu mafua na kifua.

Alizeti pia zina uwezo mzuri wa kuimarisha mifupa kutokana na kuwa na madini ya ‘magnesium’ na ‘copper’ ambayo husaidia kuifanya mifupa kuwa imara.

Hali kadhalika alizeti zimesheheni vitamin E, ambayo husaidia kuondoa maumivu ya viungo katika mwili pamoja na kupambana ana miale hatari ya jua yaani 'UV rays' na hivyo kumfanya mhusika kuwa na ngozi nzuri muda wote.

Matumizi ya robo kikombe cha alizeti huweza kukuweka mbali zaidi na uwezekano wa kushambuliwa na maradhi ya moyo, kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mafuta hatari mwilini ‘cholesterol’ hivyo kumuepusha mhusika na shambulio la moyo.

Hivyo  kila wakati unashauriwa kutumia alizeti kwa faida kem kem.



Share:

Juma Abdul na Dante pasua kichwa, Yondani ajiunga kambini, Yanga watoa tamko


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela,  amesema kuwa bado hajajua wachezaji wa Yanga ambao hawajajiunga na kikosi watarejea lini kwa sasa.

Juma Abdul na Andrew Vincent 'Dante' hawakujiunga na kikosi kambini Morogoro hata timu ilipojichimbia Visiwani Zanzibar hawakugusa kambini kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa wanadai stahiki zao.

Habari zinaeleza kuwa beki kisiki, Kelvin Yodani yeye amejiunga na timu ila sharti lake ni moja kama ilivyo kwa wenzake kwamba ni lazima alipwe stahiki zake zote.

Mwakalebela amesema kuwa:"Kwa sasa sijajua wachezaji hao watarejea lini kambini kwa kuwa wao ndio walianza kugoma,

"Ni wachezaji muhimu na mchango wao ni mkubwa kama ambavyo walipambana msimu uliopita ila kwa sasa uongozi tutakaa ili kumaliza matatizo haya," amesema.

Share:

Makonda ajipanga kuwakomesha wanaume wanaowatelekeza wanawake


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Makonda amepanga kuzisajiri ndoa zote za mkoa huo kwa ajili ya kukabiliana na wanaume wanaowalaghai wanawake kimapenzi.

Bwana Makonda amesema kuna mpango wa kuanzisha kanzi data ya ndoa zote zilizopo kwenye mkoa wake ili kupunguza utapeli wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa kuolewa.

Kanzidata hiyo itahusisha usajili wa ndoa zote ili wanaume waliooa waweze kubainika na kuwanusuru wanawake wasitapeliwe na kuumizwa mioyo kwa kutegemea ndoa.

Makonda amesema pamoja na kanzidata hiyo atatumia mkutano wa SADC kupata uzoefu kutoka kwa nchi nyingine kufahamu namna gani wanakabiliana na utapeli wa aina hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kumekuwepo na malalamiko mengi ya wanawake kuumizwa hivyo wakati umefika wa kuanza kushughulikia."Tutaanza kuangalia na kupata uzoefu kwa wenzetu wa SADC ambao kama haya wanashughulikiaje na mkutano ukiisha tutajadiliana kama mkoa tunawezeshaje usajili huo," amesema.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amedai kwamba amekuwa akikutana na malalamiko mengi sana kutoka kwa wadada wa mkoa huo kwamba wamechoka kutapeliwa.

''Tunaompango mzuri tu wa kukutana na wadada walioumizwa, huwezi kuwa kiongozi afu unaongoza watu walioumizwa na kutapeliwa na vijana ambao wanaona raha tu, tunataka tufikie hatua mtu akioa anaandika kwenye database ya mkoa, ili mwanamke akitaka kuolewa anaangalia huyu jamaa kaoa au hajaoa'' amesema Makonda.

Makonda ameongeza kuwa, wanaoumizwa wengi ni kina dada kwa sababu wanawake wakipenda huwa wanapenda kweli na wao kuwa wahanga wakubwa wa matapeli.

Amesema atatumia mkutano wa SADC unaowajumuisha wakuu 16 wa nchi wanachama kujifunza mambo mbalimbali, ikiwemo suala la wadada kutapeliwa juu ya masuala ya ndoa, kwa kuangalia nchi zingine zinashughulika vipi na masuala hayo.

Hii si mara ya kwaza kwa mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salam, kujaribu kusaidia kutatua matatizo yanayowakumba wanawake jijini Dar es Salaam.




Share:

Cristiano Ronaldo aanza kuchunguzwa na Polisi


Polisi wa Korea Kusini wameanza kufuatilia suala la Cristiano Ronaldo kugomea kucheza mechi ya kirafiki kati ya Juventus dhidi ya Kombaini ya mastaa wanaocheza Ligi Kuu Korea Kusini.

Mechi hiyo ilichezwa Julai 26 mwaka huu ambalo Ronaldo aligoma kucheza licha ya mkataba kudai kwamba angecheza.

Promota wa mchezo huo aliahidi kuwa atacheza jambo lililofanya mashabiki wengi kununua tiketi ambazo zilikuwa bei ghali.

Mashabiki walivamia ofisi za promota huyo wakitaka watajiwe sababu kwa nini nyota huyo hajacheza jambo lililofanya Polisi waweke usawa na kuwataka mashabiki kufungua kesi.

Mahabiki hao wamefungua kesi Polisi ya ulaghai kutokana na kile walichoahidiwa kutokamilika.

Share:

Rais wa Afrika Kusini kutua nchini kwa ziara ya siku mbili, kupokelewa na JPM


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuwasili Nchini Jumatano ya August 14 kwa Mwaliko wa Ziara ya kitaifa (State Visit) ya siku mbili ambapo atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Ramaphosia atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere majira ya Saa Tano usiku na baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili ataendelea kubaki Nchini kwaajili ya kushiriki Mkutano Mkubwa wa Viongozi wakuu Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika SADC.

Aidha RC Makonda amesema Maraisi wa Mataifa mengine wataendelea kuingia Nchini kuanzia August 16 ambapo amewataka wananchi kuwa wakarimu kwa wageni na kutumia vizuri fursa ya ujio wa Viongozi hao.

Share:

Naibu Gavana BOT azitaka taasisi za kifedha kuzingatia uadilifu


Na  Ferdinand Shayo,Arusha.

Naibu Gavana wa benki kuu Tanzania (BOT) Dr.Bernard Kibesse  amezitaka taasisi za kifedha kuzingatia uadilifu katika utoaji wa huduma za kifedha hasa katika zama hizi za kidigitali ili kuwahahikishia wateja wao usalama wa fedha zao.

Akizungumza katika  kongamano LA
 Taasisi za kifedha za Afrika Mashariki linaloendelea jijini Arusha ,Naibu Gavana amesema kuwa licha ya changamoto za wizi kwa njia za mitandao bado taasisi hizo zina jukumu la kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu Mkubwa kwani ndio nguzo kuu ya huduma hizo.

Aidha amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua taasisi za kifedha zinazokiuka sheria ,maadali na tararibu za utoaji wa huduma ikiwemo kuzinyang'anya leseni .

Patrick mwisusa ni  mkurugenzi mtendaji wa  Tanzania institute of bankers amesema kuwa kongamano hilo linalenga kuangalia masuala ya nafasi ya maadili katika utoaji wa huduma za kifedha na kuhimiza suala la uadilifu katika kulinda tasnia ya fedha Katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Mshiriki wa kongamano  ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi za Kifedha nchini Kenya  Kenya,  Gilbert Allela amesema kuwa taasisi za fedha zina nafasi Mkubwa ya kulinda na kutunza uaminifu wa wateja wao kwa kujifunza mbinu za kisasa za kukabiliana na wizi wa kimtandao.

Share:

Waislamu Tabora wafanya dua kufuatia vifo vya watu 70 mkoani Morogoro



Na Rahel Nyabali, Tabora.

Waumini wa Dini ya Kiislamu mkoani Tabora leo wameungana na Waumini wengine ulimwenguni kote kuadhimisha sikukuu ya Eid al Adha na kufanya  dua kufuatia vifo vya watu zaidi ya 70 ambao wameungua moto katika ajali ya lori la mafuta mkoani Morogoro na kuwaombea majeruhi 46 wa ajali hiyo.

Katika ibada hii muhimu iliyohudhuriwa na waumini wa dini ya kiislamu wake kwa waume Sheikh Mkuu wa mkoa wa Tabora Alhaj Ibrahim Mavumbia akaudhurisha salamu za pole kwa ndugu na jamaa wa wafiwa na majeruhi wa ajali ya moto mkoani Morogoro.

“Msiba huu umepunguza nguvukazi ya jamii wote hawa walikuwa na ndoto zao lakini mauti imewakatiza niwape pole wale wote walio fikwa na msiba huo na tudumu katika imani ’’ amesema mavumbi

Sheikh Mavumbi amewataka  wananchi wote kuelekea uchaguzi  wa serikali za mitaa nchini kote  kushiriki uchaguzi huo kwa amani na utulivu ili kuweza kupata viongozi kwa amani .

Kwa upande wao Viongozi na waumini akiwemo Zinduna Kambangwa ambaye ni mwenyekiti wa taasisi ya kina mama wa kiislamu  mkoani Tabora amewataka waumini wenzake kudumisha amani na umoja katika nchi.

“Tunapo ona tukio kama hili nivyema  kuchukua tahadhali  siyo kukimbilia eneo la tukio hili tukio siyo  la kwanza kutokea, Mungu awatie nguvu wale wote walio fikwa na msiba” amesema Zinduna.

Aidha katika swala hiyo waumini wa madhehebu mbalimbali ya wametakiwa kumcha mwenyezi Mungu na kutii sheria za nchi  kama vitabu vitakatifu vinavyo fundisha.

Share:

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger