juu

Thursday, 5 September 2019

Wanawake wanavutiwa na nini zaidi kwa wanaume

Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.

USAFI BINAFSI

Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi.
Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani.
Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.

KUJIAMINI

Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya!
Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza!

KUJITETEA

Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kilichopita, lakini hapa ni kwenye upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.
Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote!
Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.
Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.

KUJALI

Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali.
Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.

UKARIBU

Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha mkubwa wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku.
Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi.
Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa!

KUMSIFIA

Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti wanavyotambulishana kwa jamaa zao.
MWANAUME: “Peter kutana na mke wangu, anaitwa mama Diana. Nipo naye mwaka wa tatu sasa, tuna watoto wawili, huyo Diana na mwingine anaitwa Cris. Mama Diana, huyu ni Peter nilisoma naye A – Level, Tosamaganga Sekondari.”
MWANAMKE: “Suzan, huyu ndiye mume wangu mpenzi…anaitwa Elifaraja lakini mimi napenda zaidi kumuita Elly. Kiukweli nampenda sana mume wangu jamani, tuna mtoto wetu mmoja, anaitwa Agness. (Akimgeukia mumewe) Baby, huyu hapa ni rafiki yangu Suzan. Yaani tumekua naye mtaa mmoja huko Arusha.”

ANGALIA TOFAUTI

Bila shaka kwa namna wawili hao walivyotambulishana unaweza kuona tofauti kubwa. Mwanaume amemtambulisha mkewe kawaida kabisa, hajaonesha manjonjo au namna anavyompenda na kumthamini mwenzake, lakini mwanamke amefanya hivyo.
Sikia nikuambie, KUMSIFIA mwanamke, kuna nafasi kubwa sana kwake. Chunguza kwa makini, hata kunapokuwa na mgongano katika familia, halafu wakatokea wageni, baada ya utambulisho na mazungumzo ya hapa na pale, wageni wakiondoka kunakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kumaliza mpasuko katika familia.
Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, unamuweka katika kilele cha upendo. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye.

MALENGO

Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika.
Hii si sahihi. Dunia ya leo imebadilika rafiki zangu. Inawezekana wazee wa zamani walikuwa sahihi, maana ilikuwa ni suala la kununua ng’ombe na kuwaweka katika zizi kwenye kijiji cha jirani, halafu wanapewa malisho mazuri, baada ya miaka miwili wanazaliana, hapo ndipo anamweleza mkewe.
Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi. Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu zaidi kuliko yeyote. Yes! Mkeo ndiye ndugu yako maana umetengeneza naye familia. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha pamoja.
Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.
Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu.

KIPAUMBELE

Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.

TENDO LA NDOA

Hiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi cha ndoa. Maana hata maandiko yanasema: “Mwanamke ataacha wazazi wake na kwenda kwa mumewe, nao watakuwa mwili mmoja.”
Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na kutengewa muda maalum wa kufurahia. Si papara. Kwa bahati mbaya wanaume huwa si wafuatiliaji sana wa kujua namna ya kuwafurahisha zaidi wenzao. Wenyewe wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna ya kuwakomoa wenzao.
Si sahihi. Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute nini nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara?
Kuna kitu nimesahau kweli? Kama kipo nitafute pembeni, kwa hapa haya yatoshe kukufanya uelewe nilichotaka kukuelekeza. Nikuache na neno moja; uamuzi wa kuijenga ndoa yako upo mikononi mwako. Ukitaka iwe shaghalabaghala, pia ni wewe tu!
Share:

Yafahamu mambo ambayo mwanamke anayahitaji katika mahusiano ya kimapenzi


Anataka mume anayemjali na kujali kila anachokitaka. 

Sio tu mahitaji ya kimwili, bali pia ayatambue mahitaji yake ya kisaikolojia, upendo na kujali hisia zake.

Anataka mume anayemlinda na kumfanya ahisi kuwa yuko salama wakati wowote, kiasi kwamba hana hofu ya chochote kwa sababu anajua kwamba mumewe atamlinda na kumkinga na maudhi.
Mume anayehisi kwamba ameshikamana naye na kuridhika naye.
Mume anayeshiriki naye katika maongezi matamu yenye hisia tamu. mume anayempa maneno laini, sio maongezi makavu yasiyokuwa na hisia za kimahaba.
Anataka mume anayembusu kila anapoagana naye au anapokutana naye. Mke anapenda jambo zuri linalofanywa mara kwa mara hata kama ni dogo, kuliko jambo kubwa linalofanywa kwa kuchelewa au kwa muda mrefu. Busu unalompa kila siku kabla ya kwenda kazini ni bora kwake kuliko “outing” unayompa baada ya miezi sita.
Anataka mume anayeyaona yanayofanywa na mkewe kwa ajili yake, hata kama ni madogo. “Attention” ya mume kwa mke ni jambo muhimu mno. Anataka attention yako kwenye mavazi, kwenye chakula na hata mabadiliko madogo anayoyafanya kwenye chumba chenu….sio unakuta kitanda kimebadilishwa mkao unaanza kuponda
Mke anataka mume anayemkubali vile alivyo na kuchunga sana usalama wa hisia zake.

 Usalama wa hisia za mwanamke ni muhimu mno kuliko hata usalama wa uchumi wake. Haitakuwa na maana kama unamnunulia mavazi mazuri, lakini ukawa unaziumiza hisia zake.

8.mke anataka mume mwenye imani asiyetereka wala kuyumbishwa kwa maneno ya dada zake hata wazazi wake anayeweza kujisimamia ,sio kuperekeshwa

Ili kujifunza zaidi namna ya kutunza na kuimarisha mahusiano yako Pia usisahau kusikiliza sauti ya Mungu na kutenga Muda wa kuomba zaidi.
Share:

Jinsi ya kumshawishi mwanaume akuoe



Kumfanya mwanaume aweze kuwa na majukumu ya kimaisha ni vigumu, lakini hizi mbinu ambazo tuko nazo za kumfanya mwanaume akuoe zitahakikisha umesimama na yeye madhabahuni haraka sana.

Hivi wewe umekuwa katika mahusiano na mwanaume kwa muda mrefu mpaka unaanza kushuku iwapo huyu mwanaume yuko serious na wewe ama anakuchezea tu? Na umekuwa kila siku ukimwomba Mola akusaidie angalau amfanye huyu mwanaume ulie naye atoe ishara za kuwa atakuoa mbeleni.

Well, sote tunajua kuwa ndoto ya kila mwanamke ni kuwa siku moja katika maisha yake atakuja kuolewa kwa harusi…so sisi hapa tunataka kukupa maujanja ya kumfanya huyo mwanaume atake kukuoa haraka sana.

Jinsi ya kumshawishi mwanaume akuoe;

Kuwa girlfriend kamili. Hivi wewe na mwanaume huyu mumekuwa na maisha ya fanaka. Nyote wawili mumeinjoy maisha ya furaha, mumezama katika mapenzi, na unaona kwamba una uwezo wa kumwambia kila kitu ambacho unakifikiria. Lakini hebu ngoja kidogo na ufikirie mambo ambayo unaweza kufanya zaidi ya hayo.

Mfanye ajihisi kuwa anakubalika, yuko salama na special, haya ndio mambo ambayo anahitaji zaidi. Bila shaka utakuwa unamjua zaidi ya mtu yeyote yule. Kile ambacho anapenda na kuchukia, na mambo ambayo yatamfanya akuone kuwa wewe unapendeza zaidi ya kitu chochote kile.

Hakikisha unafanya kila kitu ambacho mwanamke kamili anaweza kufanya. Mwonyeshe kila kitu ambacho anahitaki, na bila shaka atakuona wewe umejitweka jukumu la kuhakikisha kuwa wewe uko hapo kwa ajili yake.

Mtunze. Kama mwanaume anahisi kuwa hawezi kuishi bila wewe, basi bila shaka atahakikisha ametia kufuli jambo hilo.

Hakikisha kuwa unamtunza na unamfanya akutegemee kwa mambo madogo madogo, hata kama ni jambo rahisi lile la kushughulikia nguo zake ama kumpa sapoti wakati anapohitaji. Wewe kuwa ubavuni mwake kutafanya mabadiliko ya haraka sana, na hatoweza kustahimili kuishi bila wewe.

Kuwa shabiki wake mkuu. Jeuka shabiki mkuu wa mwanaume wako. Kitu chochote kile ambacho ayaamua kufanya, hata kama ni jambo la utani ama la kuchekesha wewe mpe sapoti kwa kumshabikia atimize azma yake.

Ile siku ambayo atakuja kugundua kuwa mafanikio yake katika azma yake yamechangiwa na wewe basi atakuweka karibu yake. Atakuona kuwa wewe umekuwa karibu yake bila hata kupoteza imani katika azma yake. Well utakuwa umetoboa.

Kuwa mkweli kwa kile unachotaka. Wanaume wengi si wajuzi wa kusoma akili ya mtu. Wakati mwingine unaweza kuwa katika mahusiano na mwanaume kwa miaka mingi na ukashangaa ni kwa nini mwanaume kama huyu hajakuposa. Kuna uhakika mkuu ni kuwa wazo kama hilo bado halijamlenga kwa kichwa chake.

Kama umekuwa na maongezi ya ukweli na mwanaume wako, na ukaweka wazi kuwa unampenda, na ukaeleza vile ambavyo unaona mahusiano yenu yatakuwa miaka inayokuja, basi anaweza kuingiwa na hali ya kutaka kuchukua hatua ya mbele kuhusiana na unavyosema. Hata kama hana uhakika na ndoa, atleast utakuwa umeliweka wazo hili katika kichwa chake.

Usimuogopeshe. Usimuogopeshe mwanaume ili akupose kwa kuwa hilo si jambo la kufuata. Inakubalika kuongea maswala ya ndoa, na kueleza msimamo wako. Lakini iwapo utakuwa kila wakati unamtia presha, kila wakati unagusia swala la ndoa, ama kuanza kutokwa na machozi kila upitapo mbele ya duka la harusi basi utafanya ile dhana ya kwake kukuoa kufifia haraka sana kwani atakuogopa.
Share:

Meseji nzuri za kumtumia mpenzi wako ili akupende daima



Kila wakati nimekuwa nikisema ya kwamba maneno mazuri yana mchanago mkubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi. Hivyo kila wakati tumia maneno mazuri ili kufanya mpenzi wako akupende daiama.

Zifuatazo ndizo massage nzuri za kumtumia mpenzi wako ili akupende daiam:

Wangu kipenzi ninayekuenzi, jua wanitia uchizi na kuninyima usingizi, sijui kama una kizizi au ni mapenzi ndiyo yaninyima huo usingizi, la azizi nimekumiss kichizi, u hali gani mpenzi?
Japo umeniuzi sina budi kukupa hizi pongezi, sijui umejifunza wapi mapenzi, hakika kwako mi ni mfungwa wa mapenzi! Nakupenza mpenzi nitunziye langu penzi!

Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka kuniacha kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi tambua nahitaji yako hifadhi na niko radhi kukupeleka hadi kwa wangu wazazi, amini kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda.

Mpenzi najua u-mbali nami, majaribu ni mengi wapaswa kujihami, nitunzie zangu zabibu wangu tabibu, jitahidi kuwa mvumilivu nitakuja kukutibu, miss u ma luv.
Hakika nimepata tabibu, maradhi yangu wajua kuyatibu, napenda jinsi unavyonitibu, huna papara yaani ni taratibu, mpenzi usijemuonyesha mwingine hizo zako zabibu, maswahibu yakatayonisibu hakuna atakayeweza kuyatibu, nakupenda.

Nimeamini wewe ni mtalam wajua kunitoa hamu, unipapasapo huhisi kupoteza fahamu, maneno yako matamu hunizidisha hamu, hakika wajua kunikamua, luv u.

Kuwa nawe najivunia, mtoto mapenzi wayajua, kiuno, sauti yako tamu mithili ya chiriki wajua hasa kuitumia, mua wangu wajua kuukamua, ukiniacha jua nitaumia, nakupenda usije niacha nitajiua!
Dear siku zimekaribia, miaka …… utatimiza katika hii dunia, hakika najivunia kupata mpenzi aliyetulia, hongera kwa wako wazazi kwa kunizalia kipenzi, zawadi yangu toka kwangu ni ahadi ya kulienzi lako penzi. Happy Birthday mpenzi.
Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi akupe maisha marefu na kukuepusha na maradhi, pongezi kwa wako wazazi kwa kukuzaa mpenzi, nakupenda la azizi.
Siamini kilichotokea, hakika nimekukosea, lakini naapa katu sitorudia, upuuzi niliokufanyia, najua jinsi gani waumia ndiyo maana umeninunia, nisamehe mpenzi nafsi yangu ipate kutulia kwani bila wewe sina thamani katika hii dunia!
Namini utakuwa umerejea kwenye yako makazi na umechoka na kazi mpenzi, badili yako mavazi, bafuni ingia upate maji kujimwagia, nakupenda la azizi, pole sana na kazi!
Giza limeingia simuoni wakunikumbatia niko kama kinda la njiwa na zaidi ya mshitakiwa mwenye hatiya, sjiui wapi joto kwa kwakulipatia na wajua kipupwe kimewadia, uko wapi my dear?






0
Share:

Sunday, 1 September 2019

Rich Mavoko Kwenye Utulivu na Wimbo Wenye Ujazo Kamili….








Share:

KUNA PENZI LA KUJITOA, JITOE IKIBIDI

MAISHA ya uhusiano yana changamoto nyingi sana. Yana raha na wakati mwingine yana karaha. Penzi linapokuwa moto, ni vigumu sana kujua au kufikiria yule aliyeko kwenye mateso ya mapenzi. Unaona kila kitu kinakwenda sawia, unaamini watu wote wapo hivyo. Sikia, kuna watu wanapitia kwenye wakati mgumu kwenye mapenzi kiasi cha kufika mahali pa kujuta. Mtu anajitahidi kufanya kila liwezekanalo ili tu kuhakikisha uhusiano wake unaendelea kukua, lakini wapi!

Rafiki zangu, maisha ya uhusiano haya yanahitaji kuelewana. Ndiyo maana nimekuwa nikieleza mara kwa mara katika makala zangu, ukiwa angali kwenye hatua za mwanzo, basi shughulikia sana kuhusu suala la maelewano. Ulipime kwenye mizani ili uweze kuona kama ‘damu’ zenu zinaendana au la. Achana na haya mambo, sijui mwenzangu mpole sana au mzuri sana, kila mtu anamtamani, lakini kubwa kwako liwe ni kuangalia ‘kuivana’.

Mtu ambaye unataka aje kuwa mume au mke wako ni vizuri mkawa mnaelewa. Yule ndiye msiri wako, ni mtu ambaye atakuwa wako wa maisha. Hivyo basi unashauriwa sana kutokata tamaa, kuwa mvumilivu kwa kiasi ambacho utaona kinafaa.

Watu wengi wamekuwa wakikutana na changamoto ya kuanzisha uhusiano mpya kila siku kwa sababu tu ya kushindwa kuwa wavumilivu, lakini katika uvumilivu huo unapaswa kuwa mtu wa kupima. Weka kwenye mizani kiwango cha ugomvi wenu halafu linganisha na furaha.

Kama unaona furaha inazidiwa na ugomvi kwa kiasi kikubwa halafu kwa muda mrefu, basi ujue kabisa ulipo si sehemu sahihi. Sehemu ambayo ina maumivu makali, yanayojirudia na umefanya jitihada za kuweka mambo sawa, lakini imeshindikana, basi ni bora kujitoa. Nasema jitoe pale tu unapoona umefanya jitihada za muda mrefu, halafu unaona matatizo makubwa yamekuwa yakikuandana, basi huo ni muda wa kujitoa. Nasema jitoe kwa sababu haiwezekani ukawa mtu wa mateso maisha yako yote.

Wahenga walisema, mapenzi yanaua, upo tayari kufa kwa ajili tu ya kumpenda mtu? Mathalan unayempenda anakudunda kila kukicha, anakutishia kukuchinja, anatamani kukuwekea sumu ufe, sasa hapo kuna maisha tena?

Ndiyo maana nikasema inapofikia hatua kama hiyo niliyoianisha hapo juu, penzi la kujitoa linakuhusu. Unapoishi na mtu halafu akawa anakutamkia mara kwa mara juu ya suala la kukutoa uhai, eneo hilo siyo salama kabisa.

Penzi bora ni lile ambalo lina amani. Penzi ambalo wote mkionana mnafu-rahiana. Kila mmoja anakuwa na hamu na mwenzake, mnaishi kama marafiki na hamgo-mbanigo-mbani mara kwa mara. Mnapo-ishi kwenye furaha namna hiyo, basi hata maisha yenu yata-stawi.

Mapenzi yanaleta maendeleo kwenye nyumba. Kama unaishi na mtu ambaye mnasi-kilizana na mnape-ndana, basi hata mafanikio yatakuja. Maana mtaelekezana kwa upole, mtatiana moyo na kuwekeza akili yenu katika masuala ya maendeleo.

Mnapokuwa kwenye mbilinge za ugomvi kila siku mtaendelea lini? Ni vyema sana kuwa makini na hili hususan mnapokuwa kwenye kipindi cha awali. Mtu ambaye ana matatizo ya kila siku, umempa muda mrefu wa kubadilika imeshindikana, lakini mbaya zaidi anakuwa tishio baya kwako, basi ni bora mkaachana mapema na kwa amani.

Usingoje kutokea kwenye vyombo vya habari kama marehemu kutokana na ugomvi wa mapenzi. Ishi na mtu ambaye mnazungumza lugha moja, mnapendana kwa dhati na mwenye hofu ya Mungu. Hapo ndipo utayaona mapenzi ni matamu! Instagram& Facebook: Erick Evarist, Twitter: ENangale. Watu wengi wamekuwa wakikutana na changa-moto ya kuanzisha uhusiano mpya kila…






Share:

Tofauti ya Harmonize na RICH Mavoko ni Ndoto na Uhalisia








Share:

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger