juu

Tuesday, 7 January 2020

Jambo muhimu la kufahamu pale unapoachwa na mpenzi wako



Watu wengi, wanaume kwa wanawake wakiachwa na watu wanaowapenda kitu cha kwanza kufanya ni kuangalia kasoro zao. Kujiangalia wamekosea wapi na wanamapungufu gani ambayo yamewapelekea kuachwa.

Hali hii huwafanya kutokujiamini na kujiona kama wana kasoro flani hivyo kuwawia vigumu wanapoingia katika mahusiano mapya. Lakini hembu nikuulize kama ulishakutana na hali hii je ulishakaa kitambo kidogo na kujiuliza labda tatizo sio wewe.




Kwamba kweli kakuacha lakini inawezekana kakuacha kwakua hakuwezi na sio kwamba hufai. Kwamba ingawa wewe unamuona wamaana, unamuona anajiamini lakini yeye hajiamini kuwa na mtu kama wewe.

Anajidharau na anaona kama akiendelea kuwa na wewe ipo siku utamuacha na ataumia sana. Sasa nikuambie kitu Kama mpenzi wako kakuacha Kwa matusi, kejeli na vitu kama hivyo.

Kuna uwezekano mkubwa hajiamini au alishaona dalili kuwa unaelekea kumaucha na kaona akuche mapema ili aibu iwe kwako. Kwamba usije ukaringa kuwa umemuacha kwakua yeye ndiyo kakuacha!

Unapoachwa hasa wale ambao mnaachwa bila sababu yoyote, taratibu mtu anakuambia kua hakutaki, hujamfumania, hajakufumania na hakuna mabaya yoyote mliofanyiana.

Lakini kuna wale ambao wanakuacha kwa dharau, utasikia kuwa wewe si wahadhi yangu, siwezi kuishi na mwanaume wa namna hii, au wewe mwanamke una matatizo, kabla ya kuangalia kasoro zako hembu angalia inawezekana labda ni yeye kaona kuwa ana tatizo na hakuwezi.

Acha kujiwazia mabaya kwanza, inawezekana kweli unamapungufu lakini wewe si malaika, kama hawezi kuishi na mapungufu yako basi si wa hadhi yako. Lakini inawezekana hata hayo mapungufu si sababu, sababu kubwa ni yeye kutokujiamini.

Inawezekana aliyekuacha anakuona kuwa wewe si wa hadhi yake kweli, lakini haimaanishi kuwa wewe ni wa hadhi ya chini hapana inamaanisha kuwa wewe ni wa hadhi ya juu na hakuwezi. Jitambue na acha kulialia kwani wewe ni bora.
Share:

Saturday, 4 January 2020

FANYA HAYA! UNAPOTOKEA KUMPENDA MTU ALIYE NA MPENZI WAKE,.

Tumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha kuonana tena wiki hii tukiwa wazima. Lakini pia tumshukuru kwa kutuletea kitu kinachoitwa mapenzi.

Mapenzi yamekuwa yakichukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku na yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa furaha kwa kila mtu.

Kama huamini, angalia wale waliotokea kupenda na wao wakapendwa, utabaini nyuso zao zimetawaliwa na furaha isiyo na kifani. Lakini mapenzi hayo hayo yamekuwa ni chanzo cha vilio kwa baadhi ya watu.

Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda.

Ilishawahi kutokea msichana akampenda kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake wakafunga ndoa.

Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyopendana lakini huko nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye na mbele wala nyuma.

Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume anaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake.

Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?

Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako.
Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.

Chunguza
Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye. Ndiyo maana nikasema chunguza uhusiano wake kwanza.

Usitafute uadui
Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.

Una nafasi kwake?
Sawa umetokea kumpenda msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.

Ni rahisi kubadili uamuzi wake?
Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.

Pingana na moyo wako
Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na demu ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.

Kwa hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha kumng’ang’ania msichana mwenye mpenzi wake licha ya ukweli kwamba, huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya kuwa mume wake na siyo huyo aliye naye.

Urafiki ni poa?
Umempenda sana na hauko tayari kumkosa katika maisha yako lakini imetokea kwamba tayari yuko na mtu na umebaini huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba angalau urafiki. Siyo urafiki wa kivile sana ila angalau pale unapotaka kusikia sauti yake kwa kumsalimia tu, upate nafasi hiyo.

Usiumie, yupo mwingine
Haina haja ya kujitafutia vidonda vya tumbo bure kwa kuwa tu umebaini uliyetokea kumpenda tayari ana mtu. Chukulia ni hali ya kawaida, mademu wazuri ambao wanaishi singo wapo kibao huko mtaani, ni suala la wewe kutulia tu. Amini yupo mwingine ambaye atayafanya maisha yako yawe ya furaha.

Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana kuhakikisha unampata kwa sababu ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa gizani. Ila pale utakapoona uwezekano wa kuwa naye haupo, usilazimishe ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha tu!
Share:

WEWE UNAWEZA KUWA MCHAWI WA MAPENZI YAKO

WATU wanaamini mno katika uchawi. Wanamaliza fedha kwa waganga wa kienyeji wakiamini kwamba wamerogwa, hivyo wanatafuta ufumbuzi kutoka kwa wataalamu wa mambo ya asili. Wapo wanaoita mambo ya Kiswahili.

Kwangu napinga kuita hivyo kwa sababu nami ni Mswahili na kwa uzoefu wangu, sisi Waswahili hatuna utamaduni wa kutegemea mitishamba kuamua hatma za uhusiano wetu wa kimapenzi. Ila baadhi wapo, tena wengi haswaaa!

Shika hili kwamba wewe mwenyewe pengine ndiye mchawi wa mapenzi yako. Hujiulizi kwa nini wengine wanadumu? Ni vipi wenzi wengine wanaheshimiana? Inakuaje kwako imekuwa kinyume? Siyo suala la upepo, wakati mwingine ni kujitakia.
Kivipi mwenzi wako hakuheshimu? Ni makosa gani ambayo wewe umefanya? Ukishapata majibu ya maswali hayo, utaweza kujua faida za wewe kujitambua. Nakuasa ushike moja kuu kwamba mapenzi ni nidhamu.

Yapo kama kioo, ukiyaheshimu nayo yatakuheshimu na utayaona murua. Endapo utayachukulia kwa mzaha, nayo hayatasita kukufanyia mzaha. Mwisho utakuja kugundua kwamba yanakutesa, ukifika hapo usiache kukumbuka nawe ulivyoyatesa.
Baadhi ya watu wanaamini mazoea ndiyo yanasababisha mapenzi kupungua au kuchokana. Hilo siyo kweli hata kidogo, tena nakataa kwa herufi kubwa kwa sababu wapo mabibi na mababu waliopendana tangu enzi hizo mpaka hivi sasa.
Mapenzi ni kitu tofauti sana kwenye hii dunia na hata nje ya sayari, husababisha mambo kwenda sawa au kuharibika, kuna baadhi ya vifo hutokana na mapenzi, kuna magonjwa watu nwanaumwa kisa mapenzi.
Ukipata mpenzi anayekuelewa, anakujali na anakupenda, hata dunia iwe ya tabu kwako kwa kiasi gani, utaiona inasogea kama kawaida na maisha yanaendelea vizuri tu, naamini hapo unakubaliana na mimi.
Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au kutopata mtu wa kukujali, kutosikilizwa basi hata kama dunia kwako ina raha, utaiona ni chungu na kama kwako dunia ni chungu tangu awali halafu ukaja kuumizwa, ndio hapo watu wanapowaza na kufikiria kujiua kwa sababu haoni hata umuhimu wa yeye kuishi.
Baadhi ya sababu zinazoweza kufanya mapenzi kupungua au mwenza wako kubadilika ni hizi;

1. KUTOSEMA KWELI
Katika mapenzi uongo ni kitu kibaya sana, uongo wa aina yoyote ile ni mbaya katika mahusiano yoyote yale na huweza kupunguza mapenzi ya dhati na uaminifu kwa kiasi kikubwa hasa kama mmojawapo atagundua kuwa mwenzi wake ni muongo, anamdanganya.
Wapo ambao wakigundua mpenzi wake ni muongo wanauliza au kuongea nao ambacho ni kitu kizuri na siku zote napenda sana kusisitiza suala la wapenzi kujadili vitu mbalimbali vinavyotokea kwenye mahusiano yao, lakini wengine wanaamua kunyamaza au kuacha kabisa.

2. KUTENGENEZA PENZI LA PEMBENI
Moja ya jibu nililolipata kwa watu wengi niliojaribu kujadiliana nao mada hii walisema kuwa, mahusiano mengine yanasababisha mapenzi kupungua, inaumiza sana kugundua yule unayempenda kwa dhati ana mpenzi/wapenzi wengine. Kubali au kataa, hii ni moja ya sababu kubwa zinazofanya mapenzi kupungua au kuvunjika kabisa.
Kamwe usimuumize moyo akupendaye kiukweli, usimfanye ajutie penzi lako,usimfanye anung’unike kwa unayomtendea, ipo siku utahitaji mapenzi ya kweli kwa mwingine na hutayapata, ukimuumiza ipo siku nawe utaumia, mapenzi ya kweli yanawezekana kama kunakuwa na uaminifu.

3. UPUUZI
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa hali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani. Hata kama mwenzi wako ana uwezo mdogo kuliko wewe, hiyo isiwe sababu ya wewe kumdharau.

4.MSEMA HOVYO
Hakuna kitu kinachoweza kumfanya mwenza wako kukukimbia au hata kukosa uaminifu na wewe kama akija kugundua wewe ni mropokaji na huna ‘kifua’ hasa kwa yale mambo ambayo ni ya chumbani na hayakutakiwa kutoka nje. Hakuna mtu anayependa siri zake kutoka hadharani na huwa inaumiza sana kwenye mapenzi kumpa mtu siri zako halafu yeye anaenda kusimulia.
Mambo mnayafanya mkiwa wawili tena ndani lakini kesho unaenda kusimulia kwa watu, si jambo la busara hata kidogo
Share:

WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII


WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII
Habari za wiki hii mpenzi msomaji. Mimi namshukuru Mungu kwa kuweza kunikutanisha na nyinyi kupitia safu hii ambayo pamoja na mambo mengine nazungumzia juu ya mada mbalimbali ambazo zinagusa maisha yetu ya kila siku.

Wiki hii nitazungumazia juu ya aina ya wanawake ambao wanaume wengi hupendelea kuoa. Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.\
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.

Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.



MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake. Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingi utamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.

Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.

Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.

WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya. Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.

WENYE UCHU NA MAENDELEO

Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini. Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.

WASIOPENDA MAKUU

Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?" Akimuona rafiki yake kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia, "mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.



Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo amemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitaji upo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulani wakati inawezekana uwezekano haupo.

WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?

Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.

Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali jijini Dar-es-Salaam. Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.
Share:

FEDHA, UZURI SI KINGA YA MAPENZI, KUNA KITU CHA ZIADA


WAKATI akili yangu ikianza kupata ufahamu, nilikuwa natatizika na kuwaza kitu gani hasa katika mapenzi kinaweza kumfanya mtu atulie ndani ya penzi lake. Niliamini kuwa na fedha ndiyo dawa ya mtu kumtuliza mpenzi wake au kwa mwanamke kuwa mzuri na mwenye sifa zote, ndiyo dawa ya kumfanya mpenzi wako atulie.

Baada ya kukua na kuingia katika dunia ya ufahamu wenye mitihani mingi ya mapenzi, nimegundua kuna utofauti mkubwa katika vitu nilivyoviwaza.
Wakati nakua, nilikutana na matukio ambayo niliona kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano, lakini baada ya kupevuka, nilipata majibu ya maswali yaliyonisumbua kipindi kile cha utoto.
Sikuamini mke wa tajiri kufanya mapenzi na muuza mchicha, mwanaume mwenye mke mzuri kutembea na changudoa au msichana wa kazi asiyejua kuvaa wala kuoga.
Baada ya kuingia katika kazi hii ya kukumbushana mambo ya mapenzi, nilipata maswali mawili ya watu wawili tofauti lakini yalikuwa na jibu moja.

Mmoja alilalamika ana mke, anamhudumia kila kitu ikiwemo familia yake lakini alichomlipa ni kutembea na mtu asiye na mbele wala nyuma. Mwingine alilalamika kuhusu mpenzi wake kutembea na mwanamke wa nyumba ya pili ambaye haufikii hata mguu wake kwa uzuri.
Kabla ya kulizungumzia hilo, nirudi kwao kuwaeleza kukosa uamini hakuangalii katembea na tajiri au mwanamke anayekushinda uzuri, kutoka nje ya uhusiano au ndoa ni kosa kwa vile penzi ni la watu walioridhiana au kuoana wakiwemo waliooa wake zaidi ya mmoja.

Leo nawajibu wote kuwa fedha au uzuri wa mtu havibebi ndoa au uhusiano. Nimekuwa muumini mzuri wa kuwaeleza penzi la kweli lipo vipi, mapenzi ni upendo wa dhati kutoka moyoni, kuwa tayari kujilinda na kujiheshimu bila kujali una fedha au ni mwanamke mzuri.
Mapenzi ni mbegu inayohitaji udongo wenye rutuba ya upendo ili mbegu hiyo imee. Siku zote mwenye mapenzi ya kweli humuangalia mtu, si kitu.

Tajiri na fedha zake asipopendwa huwa katika mateso na kukonda wakati ana kila kitu. Penzi la kweli halinunuliwi kwa gharama yoyote.

Tabia ya asili huwa sawa na moto unaowaka kwenye pamba, ukitoa moshi ujue hakuna kilicho salama. Wapo watu wasiokuwa na mapenzi ya dhati, utakuta mtu anajifanya anakupenda ukiwa naye lakini mkiachana hana habari na wewe, hata kama mnakaa nyumba moja na kulala kitanda kimoja.
Mtu anapoamua kutoka nje ya ndoa wakati ndani ana mke mzuri au mume wa ukweli anayempa kila kitu, kuna mawili:

Mosi:
Huenda mwanamke aliyenaye alimtamani kutokana na sura na umbile lake na hakumpenda kwa dhati. Matokeo yake baada ya kumchoka, mwanamke huonekana hafai na hukaa naye kimazoea.
Upande wa mwanamke, naye huenda amekwenda kwa mwanaume kutokana na kujua ana fedha lakini anakuwa hana mapenzi naye. Hapo lazima atatafuta penzi la nje ili afurahishe nafsi yake, kwa hiyo watu hawa kutoka nje sishangai.

Pili:
Tabia ya kutoridhika na mpenzi mmoja, watu wa aina hii huwa hawajisikii kula kitu cha aina moja kwa muda mrefu, lazima atatafuta mtu wa kumfanya abadili mboga.

Vitu hivi vyote huwa vinawachanganya watu, hasa wale wanaoamini kuwa mwanaume anapokuwa na fedha au mwanamke anapokuwa mzuri, ni kila kitu katika mapenzi.
Mapenzi ni bahati, hasa kumpata uliyemkusudia, basi muombe Mungu utakayemchagua naye awe kweli amekukubali, hata ukiwa mbali kila mmoja amlindie mwenzake heshima, kwa kutanguliza uaminifu mbele.
Share:

Jitahidi kumuonyesha kuwa unampenda mfanyie hivi


awezekana hii ndiyo sababu mapenzi ya sasa yamekuwa na changamoto, mateso na maumivu sana kwa sababu mtu anamuaminisha mwenzake kwamba anampenda kwa kutamka ‘nakupenda’ nyingi wakati ndani ya moyo wake, hana mapenzi hata kidogo bali anasukumwa na tamaa za kimwili.

Swali la msingi ni je, utajuaje sasa kwamba anayekwambia ‘nakupenda’ anamaanisha kutoka ndani ya moyo wake na utamjuaje ‘anayekuzuga’ kwamba anakupenda? Swali hili pia lina upande wake wa pili, kwamba ukimfanyia nini mpenzi wako ataamini kwamba unampenda kwa dhati na si kwamba unaongozwa na tamaa zako za mwili?

Je, utamfanyia nini mpenzi uliyeishi naye miaka mingi aamini kwamba bado upendo wako kwake haujachuja na kwamba unampenda leo kuliko jana? Majibu ya maswali haya ni mepesi sana, twende pamoja kuchambua mbinu moja baada ya nyingine kama ifuatavyo:

MSAIDIE BILA MASHARTI YOYOTE

Kihulka, mtu yeyote huwa anafarijika sana anapomuona mtu mwingine akimsaidia kufanya jambo fulani, hata kama ni dogo kiasi gani. Siyo lazima umsaidie kitu kikubwa, hapana! Kumsaidia tu unayempenda kubeba mkoba wake kuna maana kubwa sana katika mapenzi.

Hii inawahusu wote, wale ambao wapo kwenye hatua za mwanzo za safari yao ya mapenzi au walioishi miaka mingi pamoja! Ukiwauliza wanawake wengi, watakwambia hakuna kitu kinachowafurahisha kama kusaidiwa kazi ndogondogo na wanaume wanaowapenda. Kama ni mkeo hebu siku mfanyie sapraizi kwa kumuoshea vyombo au kuwaogesha watoto (kama mnao) au mfulie nguo zake.

MPE KIPAUMBELE MNAPOKUWA PAMOJA

Ukimpenda mtu kwa dhati, hata mnapokuwa kwenye mkusanyiko wa watu wengi, akili yako yote itakuwa kwake, utataka kila anachokiongea ukisikie na umjibu kwa haraka, utapenda akicheka na wewe ucheke, akiumizwa na kitu uwepo karibu yake na hisia nyingine za aina hiyo.

Mkiwa wawili utapenda muda wote umtazame, mfurahi pamoja na ukaribu wenu usiingiliwe na chochote, huo ndiyo upendo wa dhati unavyopaswa kuwa. Cha ajabu siku hizi mambo ya teknolojia yanawafanya wengi wawe washamba wa mapenzi.

Umetoka out na mpenzi wako lakini cha ajabu, muda wote upo bize na simu, mara WhatsApp, mara Instagram au Facebook! Inawezekana vipi ukawa makini kumsikiliza anachokizungumza na muda huohuo ukawa unaendelea kuchati.

Unapochati mbele yake ni kwamba umeona simu ni ya muhimu kuliko yeye, sasa ataamini vipi kama unampenda wakati unashindwa kumpa kipaumbele hata katika kitu kidogo kama hicho?

Wanandoa wengine unakuta muda pekee ambao wanakutana pamoja, ni jioni baada ya shughuli za kutwa nzima kuisha lakini cha ajabu sasa, jioni ikifika wakikutana, baba yupo bize na simu mama yupo bize na tamthiliya, au baba yupo bize kutazama mpira kwenye runinga mama yupo bize na simu!

Kwa namna hiyo unafikiri hata ukimtamkia ‘nakupenda’ elfu kumi kwa siku atakuamini? Hakuna mapenzi hapo na hata ukisema nakupenda, ni maneno tu ya kawaida ambayo yanatoka mdomoni na siyo moyoni.

WAONESHE WATU WENGINE KWAMBA UNAMPENDA

Watu wengi huwa wagumu sana kuonesha hadharani kwamba wanampenda mtu fulani. Yaani kama ni mwanaume, akiwa na mpenzi wake mbele za wenzake, hakuna chochote anachoweza kukifanya mpaka kila mtu akajua kwamba huyo aliyenaye, siyo dada yake wala ndugu yake, bali mpenzi wake.
Share:

Siri ya mapenzi ya wizi kuwa matamu, kuliko halali.



Ni swali ambalo wengine pia inawezekana wamekuwa wakijiuliza. Inakuaje mapenzi ya kuiba, mapenzi ya juu juu yanakuwa matamu sana kuliko mapenzi ambayo yamehalalishwa.

Mapenzi kiufupi kuwa mazuri yanabebwa na mambo mengi sana.moja kuu katika hayo ni adventures(matukio) binafsi nilishawah kuwa na mpenzi wa toka miaka ya late 90 ambaye kuna matukio mengi sana yashawahi kutukuta sote.tushawah mpaka kukamatwa na polisi tuki make love, tumeshawah kukamatawa tena jumba bovu.tumeshawah kupelekana polisi mpaka ameolewa yule dada amekuwa aki miss matukio tena makubwa makubwa.tushapelekana sana polisi na mumewe sometime akihusika lakini mwishone naendelea ku mgegeda yule dada.adventures na sisi wengine adventures zinatusisimua zaidi.

Mapenzi ya namna hii yananikumbusha kisa cha wapenzi wawili ambao walianzia mapenzi yao chuo.ikafika wakamaliza masomo.wakarudi kwa wazaz wao.ikawa hali ni ngumu sana kiuchumi.bas wanapitiana wanaenda kutafuta kazi.wakiwa wanarud late sometime wanakuwa hawana naul wanalazimika kupita njia short cuts na wakiwa huko wakati mwingine wanajiwa na hamu ya mapenzi wanatafuta sehem ya giza wanafanya mapenzi.

Wakawa wakati mwingine wanafanya mapenzi hadi kwenye majumba mabovu au dampo. Sehem ambayo tu watapata privacy.wakawa waki enjoy sana maisha hayo.

Siku zikaenda wakapata kazi wakaoana wakawa na nyumba nzuri.wakaona tofaut.hawa enjoy maisha.no fire burning inside them,no passion.ingawa sasa wana kitanda kikubwa na nyumba nzuri n.k

Iliwachukua muda sana kuweza kugundua tatizo ni nini na mwishowe waliamua kuweka ustaarabu pembeni.wakaanza kuishi maisha ya no care na kuweka ustaarabu pembeni.wakajikuta wana enjoy tena mapenzi.

Inatokea unakuwa na mpenzi ambaye mnapenda sana.unapokuwa naye mnakuwa kwa kificho. Unaenda kumchukua anakaa nyuma ya gari amelala kwenye seat ili asionekane.mnaenda hotel ambayo inabidi kwnza uka check usalama then anachomoka kuingia room.ndani mnaenjoy sana.trust me.halaf anatoka tena kigaidi amevaa ushungi au kofia kubwa na miwani.

Fikiria huyu mpenzi ambaye pengine ni married.ametoroka kazini kaja ukamgegede mara moja alijawa na hamu au katoka jioni kazin mnaonana mnaenda bar flani nmnapark gari mnagegedana kwenye gari.halafu mnaagana.akirudi anachat nawe alivyo enjoy n.k

Fikiria mpenz ambaye kaaga ameenda kwenye msiba kumbe kaja ukamgegede sehemu au kwako kwa masaa kadhaa. Huwa ni mapenzi real na yenye mashamushamu sana.yana raha yake.

Mapenzi anayokwambia now baby usipigie usitume text ndo nafika home.ntakutafuta kesho.kesho yake anakupigia akiongea kwa sauti ya chini kuwa yupo chooni ametamani tu asikie sauti yako.halaf ana kata.jion anakuuliza upo wapi.anakwambia anakuja angalau umpige kimoja.huwa yanakuwa ya ajabu sana na yenye hisia kali.

Mapenzi ya wizi siku zote ni matamu. Anyway ngoja tu nifanye mchakato nioe. Maana mwaka huu jamaa nliotembea na wake zao wote wananisaka hasa.
Share:

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger