juu

Wednesday, 31 July 2019

kelele za mbu hazinyimi usingizi

WALETEEEE KELELE shogaa wanakwambia chakula cha harusini hakishibishi na ukitaka kujua masikini na tajiri ufike muda wa zawadi kwa maharusi, wareeee reeee! Miye tena niliokosa zipu kwenye mdomo, linalopita mbele yangu naongea tu kwani uongo jamani! Heri yetu tukiamka midomo inanukia wewe je, ukiamka tunaanza kutafutana kama siyo kuulizana shimo la jalala limefukuliwa upya? Au gari la taka limeangusha uchafu!  Ona sasa hadi nimesahau kukusalimia, mzima msomaji wangu wa kona hii ya Shangingi Mstaafu Anti Naa? Kwa uwezo wa manani nina imani wote hamjambo wazima wa afya kama kuna wagonjwa basi tuwaombee na kama kuna aliyetangulia mbele ya haki vilevile, tumuombee apokelewe kwa amani pia apate huruma ya Muumba.

Jama-ni leo nataka kuzung-umza na watu wazima wenzangu. Kwa vile ni watu wazima tutazungumza kwa lugha ya kiutu uzima lakini vikinipanda mtaniwia radhi kwa vile siwezi kuuzuia mzuka kama chafya ikija lazima niiachie mwenzangu! Naanza kuongea na wewe unayemnyima raha mwenzako kutokana na vitimbi unavyomfanyia.

Tena usinitumbulie macho kama wasindikizaji wa bibi harusi waliokosa sare za madera! Nachukia sana kama siyo kukereka! Jamani huu siyo wakati wa kuwapa nafasi wanawake waliokosa heshima na kujua nini thamani ya ndoa.

Wewe kama hujaolewa hebu heshimu ndoa za wenzako. Hata kama makosa kafanya mumewe kutoka nje ya ndoa, yeye ana kosa gani? Nyie wanawake mnaoingilia uhusiano wa watu, jaribuni kuziheshimu ndoa za wenzenu, si busara kumtukana mke wa mtu, kama ungekuwa bora ungeolewa wewe basi, upo?

Wengi wenu huwa hampendi ndoa, mnatanguliza starehe mbele na kufanya ugeuzwe chombo cha starehe na si mwanamke wa kuolewa. Hebu nikuume sikio muolewaji, kelele za mkosaji wala haziumizi masikio, shosti ni kosa kubwa kujibizana au kutukanana na mtu aliye nje ya ndoa yako, hiyo ni kumpa kichwa na kuamini ameweza kukuchokonoa na likakugusa.

Nikuibieni siri, wote walio ndani ya ndoa, kupatwa na masaibu ya kusumbuliwa na mahawara za waume zao. Hizo ni kelele za mkosaji, kupenda kwake starehe leo kumemfanya awe jamvi la mtaa, kapata raha kidogo kwa mumeo kachanganyikiwa sasa anataka kuingia ndani kabisa.

Hebu zichukulieni kelele zao kama mbu walio nje ya chandarua, wasio na uwezo wa kuwauma zaidi ya kupiga kelele, siku zote kelele za mbu hazikunyimi usingizi. Ushauri wangu kwenu kila anapotokea mtu wa kukutukana kwa vile tu wewe umeolewa na yeye kuachwa solemba hiyo si juu yako bali ya mumeo.

Kujiepusha na mtu huyu kwa kukaa kimya usimjibu kwa vile wewe umeishapata, ukimya wako ni pigo zito kwake kuliko kutukanana naye. Muache abwabwaje mwisho wake atachoka kama mbu nje ya chandarua, atakufa kwa kihoro, ukiona linakukera litue kisha lihifadhi! Haloo eeeh!

Mwisho nazungumza na ninyi wanaume msiojua thamani ya mwanamke ndani ya ndoa. Ni kosa kubwa kumlinganisha mkeo na hawara, kufanya hivyo ni kumdhalilisha mkeo. Mkomeshe hawara yako amheshimu mkeo kwani kama angekuwa yeye ni bora ungemuweka ndani.

Mwanaume mwenye tabia hizo ni zaidi ya mnyama, hufai kuwa baba wa familia. Kama ulikuwa bado una tamaa zako za mwili kwa nini ulikimbilia kuoa? Mjengee heshima mkeo ambaye ana dhamana kubwa mbele ya Mungu. Na wewe uliye nje ya ndoa heshimu ndoa ya mwenzako, kuiba penzi si kibali cha kuingilia ndoa ya mtu, uwe mtu wa aibu kama mbwa koko aliyekatwa mkia. Kwa leo niishie hapa, ni mimi Anti Nasra, Shangingi Mstaafu.

The post kelele za mbu hazinyimi usingizi appeared first on Global Publishers.




source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/07/kelele-za-mbu-hazinyimi-usingizi.html
Share:

Tuesday, 30 July 2019

MBINU ZA KUAMSHA NGUVU ZA KIUME MARADUFU

Wanaume wengi wa sasa wamekuwa wabovu kabisa katika kusimamisha mashine zao kiasi cha kuwa hata mdada awe mkali na mwenye mvuto namna gani amejitahidi sana kumtandika basi bao tatu kisha kitu inalala kabisaaa,tena kila bao huchukua dakika mbili tayari amekojoaLoo!
Zifuatazo ni njia chache na salama kabisa za kuamsha nguvu za kiume maradufu.

*AINA ZA VYAKULA
Tusidanganyane chakula ndio kila kitu mwilini,vyakula vya nafaka zisizokobolewa ni vizuri sana kuupa uume nguvu kuliko unavyodhani. Hivyo kama ni ugali basi penda sana kula ugali wa dona na sio sembe kwani sembe huwa haina kiini cha njano chenye protini na wanga ambacho ni silaha sana katika kuutia nguvu uume na mwili kwa ujumla.
Matunda pia kama matango,karoti ni muhimu sana katika kujenga nguvu za kiume.Vyakula vingine ni kama mihogo mibichi,magimbi nk. Lazima uwe na utamaduni wa kutumia aina hii ya vyakula katika maisha yako ya kila siku, sio eti leo una mechi na mdada ndio unajifanya kufakamia mamihogo loo siku hiyo!
*MAZOEZI
Mazoezi ya viungo ni muhimu sana kwani hufanya mwili uwe fit na hivyo huimarisha hata uume na kuufanya usilale kirahisi pale unapokuwa katika show na mrembo. Push up, kukimbia, kurukaruka na mazoezi mengine mengi ni muhimu sana.

*ACHANA NA UNYWAJI WA POMBE ULIOPITA KIASI
Pombe ni hatari sana na inadhoofisha sana nguvu za kiume hivyo chunga sana unywaji wa pombe uliopitiliza kwani ipo siku utajikuta unamwangalia tu mkeo kama dada ako vile wakati yeye nyege zimempanda balaa,matokeo yake itabidi achapwe na njemba zinazojua shughuli huko nje.
*ACHANA NA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME
Hizi dawa ni hatari sana hasahasa zile za hospitali kwani maranyingi zimetengenezwa kwa kemikali ambazo huamsha vichocheo mwili kwa muda flani lakini baada ya muda tatizo litaongezeka maradufu kwani ni tiba kwa muda mfupi tu.

*UWE MAKINI NA UPIGAJI PUNYETO
Hii kitu ni hatari sana hususani kwa wale wanaosugua sana mishipa ya uume hivyo huifanya isiwe ngangari kiasi cha kukusaidia kumshughulikia vizuri mtoto wa kike mwenye nyege zake. Hivyo kama unafanya haka ka mchezo inabidi uwe makini sana usijejutia.


source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/07/mbinu-za-kuamsha-nguvu-za-kiume-maradufu_30.html
Share:

UMUHIMU WA KULA NDIZI KATIKA KUJITIBU TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

Share:

KANUNI ZA KUISHI NA MWANAMKE

Naomba nizungumze na wewe kidume mwenzangu, ambaye huelewi namna ya kuishi na mwanamke kwa akili. Nimesema kuishi na mwanake kwa akili, naam, ndiyo ewe mwanaume unayesoma makala haya ni kwamba katika maisha yako utakayoishi hapa dunia hakuna kiumbe unachotakiwa kuishi nacho kwa akili kwa mwanamke.

Ni kweli usiyohitaji mwanga wa jua juu ya hilo. Mwanamke usipoishi naye kwa akili ni kwamba mahusiano yenu hayatadumu hata iweje labda ukatambike. Pamoja na maudhi waliyoumbwa nao viumbe hawa unatakiwa kuyaelewa na kwenda  nayo sawa kwani pindi utakapofanya  kinyume chake ni kwamba hautadumu na kiumbe huyo.

Labda twende tukaone kanuni za kuishi na Mwanamke kama ifutavyo;

Kwanza usimpige mwanamke, Naam nazungumza na wewe hakuna mwanamke ambaye anapenda kupigwa na mumewe, labda uende mkoa wa Mara, kwani huko ndiko wanakosema ukipigwa ndiyo upendo, sina ushahidi na hilo kwani hayo ni maneno ya kuambiwa tu.

Kuna baadhi ya wanaume hudhani kumpiga mwanamke kunasaidia, hapana kitendo hicho hakisaidii hata iwaje kwani hata kisheria ni tabia isiyofaa hata chembe. Upendo wa kweli hujengwa na misingi imara ya upendo wenyewe na si kupigana.

Usimtukane na kumshushia heshima, Kila wakati hakikisha ya kwamba unapambana ili kuukuza upendo baina yako na mpenzi wako. Hautakiwa kuonesha unamjali mpenzi wako mkiwa wawili wakati mwingine ukiwa na marafiki zako unamshushia heshima mpenzi wako kwa kusema maneno yasiyo na heshimam kumuhusu yeye mbele ya marafiki zako. Mambo yenu wawili basi yabaki kuwa ni ya kwenu pekee, usiwalishe marafiki chakula ambacho mlipaswa kula wewe na mpenzi wako. Kila wakati unatakiwa kuhakikisha heshima inafuata mto msimbazi, hapa nimetia chumvi ila huo ndiyo ukweli halisi.

Usimfanye ajihisi hapendwi na anamkosi, kila mwanamke anapendwa kupendwa, hivyo kila wakati unatakiwa kuonesha kwamba unampenda  mwanamke uliyenaye katika mahusiano yenu, usioneshe kwamba humpendi kwani kufanya hivyo kutamfanya ajihisi ya kwamba dunia hii haina usawa kwani atajihisi hakuna anayempenda na kila wakati ana mkosi katika sayari hii.

Usimsaliti na kujionyesha kabisa kwamba una saliti, usaliti ni mbaya na maumivu yake hayana dawa, kama unalitambua hilo basi kila wakati  tulia na huyo mwanamke uliyenaye kwani kufanya hivi kutamfanya mwanamke huyo naye atulie na wewe. Usaliti huleta magonjwa na pia huleta mitafaruko mikubwa katika mahusiano ya kimapenzi hivyo ili uweze kuishi vyema na mwanamke hatimaye mfikie malengo yenu  mnatakiwa kuhakikisha ya kwamba hamsalitiani hata iwaje.

Mpe zawadi, hata kama ni ndogo kiasi gani kwake ni alama tosha. Zawadi ni zawadi hili ndilo unapaswa kulielewa. Zawadi ni surprise kwa huyo unayempenda. Hakuna kitu ambacho huongeza alama kubwa kwa mwanamke kama ukimpa zawadi. Pindi unapompa zawadi mwanamke uliyenaye ni kwamba  mwanamke huyo ataona uthamani wako kweke na pia ataongeza mahaba na wewe.

Mpaka kufikia hapo Muungwana blog hatuna la ziada tunachotaka tu kukusihi ni kwamba kila wakati hakikisha unayazingatia hayo vyema kama kweli unataka kuwa mtu mwenye maisha bora na yenye furaha katika mahusiano yenu ya kimapenzi. Tukutakie siku njema na mafanikio mem

source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/07/kanuni-za-kuishi-na-mwanamke.html
Share:

FAHAMU MISINGI HII YA UVUMILIVU KATIKA NDOA

Share:

Monday, 29 July 2019

KWA MPENZI ULIYENAYE UMEPATA , UMEPATIKANA?

MAPENZI huweza kumfanya mtu akaishi maisha ya raha mustarehe hasa pale anapompata mtu mwenye penzi la kweli lakini pia usipoyajulia mapenzi yanaweza kukutoa roho.  Wangapi leo hii wamechanganyikiwa kutokana na kukataliwa penzi na watu waliotokea kuwapenda? Wangapi wamejiua baada ya kuachwa na wapenzi wao? Wangapi wanashindwa kufanya kazi zao kwa ufasaha kwa sababu wamekorofishwa na wapenzi wao?

Hakika ni wengi na kwa maana hiyo basi kama unataka kuishi maisha ya raha, pamoja na mambo mengine hakikisha huchezi kamari kwenye mapenzi, ingia katika uhusiano unaofaa ili mwisho wa siku furaha ichukue nafasi katika kila siku iendayo kwa Mungu.

Wiki hii naomba nizungumzie swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza bila kupata majibu sahihi kiasi cha kuwafanya washindwe kuishi maisha ya furaha na wapenzi wao. ‘Nimepata au nimepatikana?’ Hili ni swali wanalojiuliza wengi walio katika uhusiano.

Huenda hata wewe ulishawahi kujiuliza swali hili na mpaka sasa hujabaini ukweli wa penzi lake kwako na kama hujawahi kujiuliza swali hili basi hauko makini katika uhusiano wako. Hivi wewe ambaye unajiamini kwamba umepata mtu ambaye anakupenda wa dhati una kipi cha kushika? Unajiridhishaje katika hilo?

Labda niseme tu kwamba, mapenzi ya sasa yamejaa ulaghai wa kupitiliza. Unaweza ukajikuta uko na mpenzi ambaye anaonesha kukupenda sana kiasi cha kukufanya uamini kwamba umepata mtu sahihi lakini kumbe anajifanyisha.

Yaani huo ndio ukweli wenyewe na usishangae hata huyo uliyenaye akawa anakupotezea muda wako tu. Unachotakiwa kukifanya ni kumfanyia uchunguzi wa kina kubaini ukweli wa penzi lake kwako. Niseme tu kwamba, hakuna mtu anayeweza kuwa na uhakika wa asilimia mia moja kuwa mpenzi aliyenaye amepata mtu kwa maana ya mtu kwelikweli na kama unaamini hivyo, unaifurahisha tu nafsi yako kwa kuwa ukweli unaweza usiwe huo.

Huyo uliye naye ndiye mwenye siri moyoni mwake na ndio maana unaweza kukuta mpenzi wako anakusisitizia kwamba anakupenda lakini bado unashindwa kuamini. Wataalam wa masuala ya mapenzi wanasema, kumdhihirishia mpenzi wako kwamba unampenda sio lazima umwambie NAKUPENDA! Vitendo vyako ndivyo vitamfanya aamini hivyo.

Hata hivyo hukatazwi kumpenda mtu lakini bahati mbaya inakuwa pale utakapotokea kumpenda mtu asiyekupenda na ukalazimisha akupende ili kujiridhisha.

Walio katika aina hii ya mapenzi wako wengi. Mtu anaona kabisa mwanaume hamuoneshi kumpenda kwa dhati, hamjali lakini mwanamke anamng’ang’ania tu eti kwa sababu anampenda. Hivi mwanamke kama huyu anashindwa kubaini kuwa mwanaume aliyenaye hana penzi la dhati kwake?

Ifike wakati basi ukae chini na utafakari penzi analokupa mpenzi wako na kuchukua uamuzi sahihi, kumuacha au kuendelea naye. Usikubali hata siku moja kupotezewa wakati na mtu asiyelithamini penzi lako. Ni wakati muafaka wa wewe kujiuliza kama umepata au umepatikana, na kama umepatikana, jinasue lakini kama umepata basi tulia na uyafurahie maisha yako.

 

The post KWA MPENZI ULIYENAYE UMEPATA , UMEPATIKANA? appeared first on Global Publishers.




source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/07/kwa-mpenzi-uliyenaye-umepata-umepatikana.html
Share:

Sunday, 28 July 2019

HAKURIDHISHI FARAGHA ? JIFUNZE!

UZURI wa mapenzi ni kuridhishana. Kila mmoja ‘ainjoi’ kukutana na mwenzake, alifuarahie tendo katika hali ambayo hawezi kuwa na hamu ya mapenzi pale anapokuwa amemaliza tendo. Kinyume na hapo, kukiwa na tatizo katika upande mmoja, furaha ya tendo inaondoka. Mmoja kati ya wapendanao anakuwa na shauku ya tendo wakati mwingine hana. Kitakachofuata hapo ni yule ambaye hajaridhika kutafuta njia mbadala ili kupata tiba ya mapenzi. Kwa kizazi cha sasa, watu wengi sana wamekuwa wakiteswa na tatizo la kutoridhishwa au kutomridhisha mpenzi wake.

Mwanaume anaweza kuwa anataka kumridhisha mpenzi wake, lakini anashindwa au mwanamke anataka kumridhisha mpenzi wake, lakini inashindikana. Wanapokutana  faragha, kila mmoja anakuwa na nia njema kabisa kutaka kukamilisha tendo la ndoa, lakini kwa tatizo linakuwa kwa mmoja wao na kuwafanya washindwe kufurahia tendo.

Mmoja kati ya wampendao anakuwa anawahi kuridhika wakati mwenzake anakuwa bado hajafikia muda wa kuridhika. Hapa ndipo zinapoibuka zile kauli za ‘mwenzangu haniridhishi’, ‘mwenzangu amekuwa gogo’ na nyingine nyingi zinazofanana na hizo.

Yule ambaye  haridhishwi huwa anakuwa katika wakati mgumu. Kutokana na desturi ya watu kutopenda kuambiana ukweli hususan katika jambo hili ambalo wengi wanaamini ni la aibu, hubaki nalo moyoni na kuendelea kuumia. Anavumilia hadi inafika wakati anachoka. Kinachofauta hapo ni kusaka suluhu. Ndiyo wakati wa kuanza kuwatafuta marafiki tofautitofauti ambao wanaweza kumshauri vizuri au vibaya.

Wapo wanaoweza kumshauri kwamba afanye vitu fulanifulani ili aweze kufanikiwa, lakini wengine huweza kumshauri atafute mtu mwingine ambaye atamridhisha. Kutokana na kero anayoipata, ni rahisi tu kufanya uamuzi wa kujaribisha kwa mtu mwingine. Usaliti ndiyo unaanzia hapo. Amani inatoweka na baadaye ugomvi huibuka, hapo ndipo watu hufikia hatua ya kushindwa kuvumiliana na hatimaye kuachana.

NINI CHA KUFANYA?

Kinachotakiwa kufanyika suala kama hili linapotokea, kwanza ni kuzungumza na mwenzako. Kama unaona kuna kitu hakipo sawa kwa upande wako, mueleze mwenzako ili muweze kutafuta suluhu. Kama pia tatizo unaliona lipo kwa mwenzako, tumia lugha nzuri kumueleza ili muweze kupata suluhisho. Yawezekana tatizo ambalo upo au yuko nalo ni la kisanaa ya tendo. Tendo hili linapaswa kufanyika kwa sanaa na ubunifu ili muweze kwenda sawa.

Yawezekana mwenzako anakurupuka, kabla hajakuandaa yeye anakuwa tayari ameshafika mbali kifikra hivyo kujikuta anakuacha kwenye mataa. Jadilini kwa kuelezana nini kifanyike ili kila mmoja afurahie tendo. Elimu ya kujiandaa inabidi kila mmoja aifahamu. Ushirikiano wa kulifanya tendo liwe na mashamsham linatakiwa.

Ujue wapi mwenzako anapenda umguse zaidi na kwa namna gani. Ni vyema mkawekana wazi ili kila mmoja asiwe mgeni na mwenzake. Ukimya wakati mwingine ndiyo unasababisha matatizo ya wapendanao kutofautiana. Yawezekana ulilonalo au alilonalo mwenzako ni la kitabibu, waweza kumshauri akaenda kutibiwa hospitalini na likaisha.

Mueleze mwenzako, mtashauriana na kupata suluhu. Hakuna sababu ya kuhangaika kwa kutafuta suluhu ya kuridhishwa na mtu mwingine. Unaweza kufanya hivyo kumbe nako bado ukakutana na tatizo ni lingine. Utahamia kwa mwingine bila kujua kiini cha tatizo huenda ni wewe mwenyewe, matokeo yake yatakuwa ni yaleyale.

Mheshimu mwenzako. Mtunzie siri kwani faragha inahitaji siri. Mnapokuwa wawili, elezaneni ukweli. Mueleze akutekelezee nini ili wewe uridhike. Kama kweli mmepandana kwa dhati na mna ndoto ya kufika mbali, hakika mtashughulikia tatizo na kusonga mbele. Kwa leo tuishie hapa, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri! Waweza kunifuata kwenye mitandao yangu ya kijamii, Instagram na Facebook natumia Erick Evarist, Twiter natumia ENangal

The post HAKURIDHISHI FARAGHA ? JIFUNZE! appeared first on Global Publishers.




source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/07/hakuridhishi-faragha-jifunze.html
Share:

JE WAJUA UKIMFANYIA HAYA MPENZI WAKO HAWEZI KUKUSAHAU KAMWE

Habari yako ndugu msomaji? Natumaini u mzima na mwenye afya njema.
1. KILA siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani alivyo mzuri. Kumbuka kila msichana anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye ni mzuri anaona una mthamini kuliko msichana yeyote awaye.
2. Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg kwenye simu mueleze hisia zako kiasi gani unampenda. Kumbuka wasichana hupenda kusikia zaidi kutoka kwa wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi iwe tu katika kipindi cha siku ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa unampenda. Muoneshe msichana ni kiasi gani yeye ni muhimu sana kwako.
3. Busu la ghafla na kumshika mkono wakati mkitembea pamoja itamfanya yeye kujisikia raha zaidi. Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea mara kwa mara hi humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye karibu na kumfanya kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali
4. Tambua mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa pale kwa ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na mahaba. Utashangazwa sana na kiasi gani msaada huo umeleta mabadiliko kwake. Hakikisha unamsaidia katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa wavulana wengi. Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi ambacho pesa huitajika kulinda penzi lako. Si msichana anapokuomba pesa ina maana ana nia ya kukuchuna au amekupendea pesa kuna shida nyingine inabidi akuombe wewe tena kwa kukupima kama utakuwa tayari kumsaidia.
5. Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana hupenda enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.
6. Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu. Msichana hupenda kutoa ushauri kwa mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia kuthaminiwa nawe na kukuona umemuamini
7. Ukijiona upo busy sana usithubutu kuacha japo kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au kwingineko hakikisha unapopata nafasi japo ujumbe mfupi wa kumwambia unampenda.
8. Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la kumbatizi kuna jambo kubwa sana hutokea. Si kwake tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka pamoja kifikra hata pale msipokuwa pamoja.
9. Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae. Mwanamke hupenda ustaarabu kwa mtu ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira kabla hata hujamtongoza unaweza ukamkosa msichana hivihivi wasichana huwaogopa wavulana wenye hasira na wagomvi kwa sababu hupenda kubembelezwa.
10. Mdekeze. Msichana anapenda kudeka anaenda kudeka sana na kubembelezwa sana hivyo mvulana ukidekewa usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe ndio wakati wako wa kumuonesha msuchana wako unampenda mdekeze mpaka aone aibu kudeka siku nyingine. Wasichana wameumbwa kwa jili ya wavulana ndio maana hudeka hii ndiyo silaha pekee na ya mwisho kumpata msichana hata kamasi wako ni wa rafiki yako unaweza ukatumia silaha hii kumpora msichana huyo kwa mwenzio usipojua kudekeza utaachwa pia.


source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/07/habari-yako-ndugu-msomaji-natumaini-u.html
Share:

STAILI ZA KUMLA MWANAMKE MNENE NA MREFU SOMA HAPA

mwanamke mnene husumbua sana kwenye mitindo ya tendo la ndoa kwa kua anakua na mwili mzito hvyo inakua mgumu kuji2ma ktandan na hata mwanaume inakua ngumu kumkontrow kwa mikao unayoitaka kwakua mingne hataweza kumudu na hata mwanaume hatoweza kuimudu.
unaposhughulika na mwanamke wa aina hii mikao yake ni mitatu tu ndyo anayo mudu
1).kifo cha mende
mwanamke alale chal na mwanaume aje kwa juu yake
2).mbuz kagoma kwenda
ni mtindo ambao nwanamke alale kifudifudi na kubinua kiuno chake juu huku akiegemea magot na viwko vya mikono, miguu yake akiwa ameiachanisha na kurud chni kwa kufuata usawa wa mwanaume, mwanaume nae apge magoti kwa nyuma aendelee na mchezo.
3) 71
mkao huu wa 71 wote mnatakiwa mkanyage chin na mwanamke anainama na kushka ukingo wa ktanda, meza, kiti n.k
mwanaume abak nyuma amesmama na safar ianze ya utam hyo ndyo mkao itakayo mfurahsha mwanamke wa aina hyo.



source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/07/staili-za-kumla-mwanamke-mnene-na-mrefu.html
Share:

Saturday, 27 July 2019

KWA VITU KONKI VYA CHUMBANI KWENYE NDOA ZINGATIA HAYA

M AISHA  yana changamoto nyingi sana ambazo unatakiwa uzitatue kabla hazijayaathiri maisha yako. Huna sababu ya kuchanganyikiwa eti kwa kuwa mke au mume kakuacha, huna haja ya kulia eti kwa sababu unayempenda, yeye hakupendi. Pambana kuikabili hali hiyo na kisha uyaache maisha yako yaendelee.  
Mpenzi msomaji wangu, ni ukweli ulio wazi kabisa kwamba ndoa ni jambo la msingi sana katika maisha ya kila binadamu na ndio maana wapo wanaofikia hatua ya kusema, matukio muhimu katika maisha ya binadamu ni kuzaliwa, kuoa ama kuolewa na kufa.
Hata hivyo kuoa ama kuolewa ni heshima katika jamii na ndio maana leo hii wapo wanaofanya kadiri wawezavyo kuhakikisha wanapata watu wa kuwa nao kama mwili mmoja pale wanapofikia umri wa kufanya hivyo. Ikumbukwe kufunga ndoa kuna wakati wake, sio kwamba pale unapojisikia kufanya hivyo basi ufanye hata kama mazingira, umri na hali yako kimaisha havikuruhusu.
Lakini sasa, kibaya ambacho nimekuwa nikikishuhudia katika jamii yetu kila siku ni kwamba wapo ambao huchukulia kuoa ama kuolewa kama fasheni, hali ambayo huwasababishia kuingia katika matatizo ambayo hawakuyatarajia. Ieleweke kwamba hadi kufikia hatua ya kutamka kwamba unataka kufunga ndoa ni lazima uwe umefanya uchunguzi wa hali ya juu na kuhakikisha kwamba unaingia katika maisha ambayo hutayajutia.
Suala la kuoana si la kukurupuka, ni lazima kwanza uangalie, je ni kweli unastahili kuoa ama kuolewa kwa wakati huo? Hili ni swali la msingi kujiuliza na kama jibu litakuja akilini mwako kwamba muda bado basi unatakiwa kusubiri. Suala la kuoa ama kuolewa ni la heri na halitakiwi kuharakishwa eti kwa kufuata mkumbo. Waswahili wanasema; mambo mazuri hayataki haraka.
Kwako wewe mwanamke, unapodhani umefikia umri wa kuolewa kwanza unatakiwa kuangalia mwanaume sahihi, mwanaume ambaye hata utakapoingia kwenye maisha hayo ya ndoa, utadumu na haitakuwa ndoa ndoano. Epuka sana wanaume walaghai, matapeli wa mapenzi ambao mara nyingi hutumia gia za kuoa ili wakubaliwe kimapenzi.
Anapokutokea mwanaume na kukuambia anakupenda na angependa kuwa wako wa maisha, mchunguze kwa muda mrefu kabla hujafanya uamuzi wa kumkubalia. Usimkubalie haraka ili nawe uitwe mke wa mtu kama ilivyo kwa rafiki au ndugu yako aliyeolewa hivi karibuni.
Kwa ujumla ni kwamba kabla ya kumtamkia yule ambaye ungependa umuite mke na yeye akuite mume ni lazima kwanza mtaanza kuwa wapenzi wa kawaida kisha baada ya kuona kwamba, mmependezana kitabia ndipo suala la ndoa litaingia. Kama mtaafikiana katika hilo mnaweza kuingia katika hatua.


source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/07/kwa-vitu-konki-vya-chumbani-kwenye-ndoa.html
Share:

TABIA 8 ZA WAPENZI WENYE PENDO LA DHATI

MAPENZI ni hisia. Unapompata mtu akakupenda kwa dhati, ni vigumu sana kuyatambua mateso ya wengine wanayopitia kwenye mahusiano yao. Wapendanao wanajiona wapo kwenye dunia yao, wanapokuwa pamoja wanajihisi matajiri hata kama ni kapuku. 
Unapokosea kumchagua mwenzi wa maisha mara nyingi unajikuta kwenye mateso mazito na siku zote kati ya mtihani mgumu kuufaulu katika masuala ya uhusiano wa kimapenzi ni kumpata mwenza sahihi mwenye mapenzi ya dhati.
Wengi wamejikuta wakiingia kwenye uhusiano na watu ambao hawana mapenzi ya dhati. Wanateseka, wanajaribu kuwavumilia wenzi wao ili labda pengine wanaweza kubadilika lakini wapi. Mwisho wa siku wanaishia kuachana. Ni vizuri sana kwa wale wanaokwenda kuanzisha mahusiano mapya, wakawa makini sana katika kufanya utafiti juu ya wenza wao. Jiulize, unayempenda ana mapenzi ya dhati? Atakujali? Atakuthamini? Atakupa kipaumbele? Atakuheshimu?
Hili linawezekana endapo tu utafanya uchunguzi mapema kwa wakati ule unaoanzisha uhusiano. Mwenye upendo wa dhati utamjua tu endapo utakuwa makini. Penzi la kweli halilazimishwi, linaonekana dhahiri shahiri. Mpenzi wako unamjua kama ana mapenzi ya dhati kwako hata kwa kumuangalia tu machoni, anavyokujali, anavyokuhitaji na hata jinsi anavyokuthamini.
Ili kupata picha ya watu wanaopendana kwa dhati, leo tuziangalie tabia 8 za watu ambao wanapenda kwa dhati. Ukiona tabia hizi nane hazipo kwenye uhusiano wako basi ujue kabisa haupo kwenye uhusiano ule ninaouita wa dhati, uhusiano ambao unawafanya muishi kwenye dunia ya peke yenu:
KUJUANA
Wenye mapenzi ya dhati huwa wanajuana hali zao. Mwanaume anamjua vizuri mwenza wake kwamba yupo katika hali gani. Ana furaha au huzuni? Ana mawazo au anaumwa bila hata ya kuambiwa anakuwa ameshamjua mwenzi wake.
MAPENZI SIO KIPAUMBELE
Wanaopendana kwa dhati hawakamilishi uhusiano wao kwa tendo la ndoa tu pekee bali kuna mambo mengi wanayofanyiana nje ya kufanya tendo hilo. Wataalam wa masuala ya mahusiano wanasema tendo la ndoa ni moja ya sehemu kati ya vitu mia moja vinavyofanywa na wapendanao kukamilisha uhusiano.
KUTANIANA
Wenye mapenzi ya dhati wana ‘kautani kao ka kimapenzi.’ Hako kautani kao ni ka-ndani na wanakaelewa wao wenyewe, yawezekana mtu wa nje asiweze kabisa kukabaini.
KIPAUMBELE
Wenye mapenzi ya dhati wanapeana kipaumbele. Kila mmoja anampa kipaumbele mwenzake kuliko kitu kingine chochote, hayo ndio mapenzi ya dhati.
KUAMINIANA
Tabia ya watu wanaopendana kwa dhati pia huwa wanakuwa wanaaminiana. Kila mtu anamuamini mwenzake na kila mmoja anayeaminiwa anajiheshimu na kuilinda heshima yake.
HAWAFICHANI
Wapendanao ambao wanaishi kwenye dunia ya kupendana kwa dhati mara nyingi si watu wa kufichana. Wanaelezana ukweli, wapo huru kusema ukweli kuliko kusema uongo.
WANAZUNGUMZA LUGHA MOJA
Wanaopendana kwa dhati wanazungumza lugha moja katika masuala mbalimbali yanayowahusu. Utadhani wanawaza pamoja kumbe wapi, wanashibana na mambo yao huandika kumbukumbu ya pamoja kutokana na utu, kujaliana na kuheshimiana.
WANASHIBANA TENDO
Wapendanao wenye mapenzi ya dhati wanashibana tendo. Wanajuana miili yao, kila mmoja anaujua vizuri mwili wa mwenzi wake hivyo wanalifanya tendo la ndoa kuwa kwenye kiwango cha juu pindi wanapolifanya.



source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/07/tabia-8-za-wapenzi-wenye-pendo-la-dhati.html
Share:

Friday, 26 July 2019

JINASUE HIVI NA MATAPELI WA MAPENZI

WENGI wameji-kuta kwenye majuto kwa kuwakabidhi watu wasiofaa mioyo yao. Wameambulia mateso makali, wamejikuta wamepoteza muda kwani wameachwa solemba wakati ambao hawakuutarajia.  Ndugu zangu mapenzi yanauma. Yanauma kwelikweli hasa linapokuja suala la kumkabidhi mtu moyo wako ukiamini atakupenda, atakuthamini kama vile wewe unavyomthamini. Unakuwa na matumaini kwamba nipo na mtu sahihi. Mtu ambaye nitafanya naye maisha, mtu ambaye nitadumu naye katika shida na raha, mtu ambaye nitaingia naye kwenye ndoa mwisho wa siku anaingia mitini, inauma sana.

Mapenzi ni uwekezaji. Unawekeza nguvu, unawekeza akili, unawekeza maisha. Unapokuwa na mwenzi wako unamuamini. Unapanga naye mipango ya kufika mbali kwani kila ambaye anawaza maisha, lazima atakuwa anaifikiria ndoa na mtu sahihi.

Atafikiria familia kwa maana ya kupata watoto, kusomesha na mambo mengine yahusuyo familia. Hiyo ndiyo safari ya wapendanao, inayoanzia kwenye urafiki, uchumba na hata baadaye ndoa. Wahusika wanapoikamilisha safari hiyo pamoja huwa wanapongezana kwani si rahisi kwa kila uhusiano kuweza kuwa imara hadi kufikia hatua ya ndoa, ni kwa neema tu na baraka zake Mungu watu hujikuta wamekamilisha pamoja safari yao.

Wengi sana hujikuta wakiishia njiani kwa namna moja au nyingine. Hii inatokana na sababu zifuatazo; Kuna ambao tangu awali wanaanzisha uhusiano na wenzi wao kutokana tu na mahitaji fulani, mathalani yawezekana akawa anafuata fedha au matamanio tu ya muda mfupi.

Hana mapenzi ya dhati na mhusika. Matokeo yake, ataishi kwenye uhusiano kwa kipindi fulani halafu mahitaji yake yakiisha, anamuacha mwenzake solemba na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine. Msimamo; kuna wengine huwa wanakosa msimamo. Wanakuwa na tamaa. Anaingia kwenye uhusiano na mtu lakini baadaye anapokutana na mtu mwingine, mwenye mvuto au mahitaji yake mengine, anamhama mpenzi wake wa awali na kwenda kwa mwingine.

Kuna wengine wanayumbishwa na wazazi. Unakuta mwanamke anataka kuolewa, wazazi kwa sababu wanazozijua wao, wanamkataa muoaji. Au mwanaume anataka kuoa, wazazi wake nao wanamkataa. Wapendano huenda walishajipanga lakini wanajikuta wakishindwa kuoana. Ndoto zao za kufika mbali zinafutika kulingana na matakwa ya wazazi, biashara inaishia hapo.

Wengine ushirikina, kuna wengine wanajikuta wameachana kwa sababu tu ya ushirikina. Alikuwa anampenda mtu wake, anakutana na mtaalamu wa mambo ya kishirikina, anafanyiwa mambo na kujikuta amehamia. Kiukweli ni ngumu sana kumjua mtu ambaye si mwaminifu. Inahitaji akili ya ziada na msaada wa Mungu kumtambua mtu ambaye upo naye kwenye uhusiano ni sahihi.

Suala hili wanawake wengi wanaweza kulitolea ushuhuda. Ninavyoandika makala haya, najua wengi sana wameshazalishwa na kutelekezwa. Waliwapa wanaume mioyo yao matokeo yake wameambulia maumivu. Mwanaume anaishi na mwanamke na lake moyoni. Upendo unakuwa haupo  kwa yule aliye naye. Au anayumbishwa na sababu nilizoziainisha hapo juu na matokeo yake anamuacha mwenzake.

Nimekuwa nikisisitiza sana katika makala zangu na leo nitazidi kusisitiza. Usikubali kuanzisha uhusiano na mtu ambaye huna imani naye. Mchunguze kwa muda mrefu mtu kabla ya kumkabidhi moyo wako, kabla ya kufanya naye ngono zisizo salama ambazo zinaweza kukusababishia kupoteza ‘future’ yako.

Ni kweli mtu anaweza kuficha makucha yake lakini si kwa miaka yote. Utamjua, ukigundua tu mueleze kwamba wewe si mtu wa mlengo wake. Achague moja, kubadilika au akuache umpate mtu sahihi. Muombe Mungu akuoneshe mtu sahihi. Fungua macho yako kumtambua kulingana na tabia zake, mapito yake na mwenendo wake. Mtu mwovu utamjua tu, muache mapema kabla safari yenu haijafika mbali. Instagram na Facebook: Erick Evarist, Twitter: ENangale.

The post JINASUE HIVI NA MATAPELI WA MAPENZI appeared first on Global Publishers.




source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/07/jinasue-hivi-na-matapeli-wa-mapenzi.html
Share:

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger