juu

Thursday, 3 October 2019

Wanawake Acheni Kuwaendekeza Wachungaji na Kuvunja Ndoa zenu



Habari ya wakati huu wapendwa wetu karibuni kwenye ukurasa wetu wa mahusiano uweze kujifunza mambo mbalimbali.
Loading…
Leo nina jambo moja muhimu ningependa tuelimishane hasa kwa wale wanawake wenzangu ambao wameokoka na kujifanya wapo bize na wachungaji kuliko mume.

Yaani huyu kila kitu ni mchungaji nafasi ya mume ameshaitoa yupo radhi asimpikie mumewe aende kwa mchungaji.

Kuna baadhi ya wanawake yaani ni kero katika ndoa zao ama katika familia zao yaani ulokole wake unapitiliza hadi anasahau majukumu yake ya nyumbani.

Sijasema usiwe mlokole. Ulokole ni jambo nzuri mbele za Mungu na uenende kwa matendo mema na sio ulokole wako uwe kero kwa mumeo.
Kuna wengine utakuta anarudi nyumbani saa tano usiku akiulizwa anamtaja mchungaji hapo hajui mume amekula au la na hata chakula hakijapikwa huo muda.



Wanawake wengine utawasikia wakisema mchungaji wangu ndio kipaumbele sawa wewe umeolewa na mchungaji au? Acheni kusahau majukumu yenu. Hata vitabu vya Mungu havisemi hivyo.

Wapo wengine wanalala hadi wiki kanisani wakiulizwa maombi hajui cha mume wala watoto. Masuala ya nyumbani kwake hayaelewi yeye ni bize na mchungaji na kanisa.

Kuna wengine mpaka ndoa zimevunjika kisa wachungaji embu badilikeni wanawake wenzangu. Msiwatafutie dhambi wanaume zenu kuwatafutia nyumba ndogo kwa kushindwa kutekeleza majukumu yenu.



Ifike pahala usimamie familia yako kama inavyotakiwa hata vitabu vya Mungu vimeeleza mwanamke huivunja ndoa yake kwa mikono yake. Hata huyo mchungaji unayekwenda kukesha naye anajua hilo jambo.

Jamani kuna wengine sijui wanalogwa na hao wachungaji wao yaani hata siwaelewi unakuta wanawapelekea hadi hati za nyumba ama viwanja kwa wachungaji wao baada ya muda utasikia wakilalamika wametapeliwa.

Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa huko ndio kukosa maarifa hivi kweli unatoaje hati zako na kumpatia mchungaji kisa tu amekupatia unabii wako.

Watu wengi wanaangamia kwa kupenda unabii huo unabidii mnaouendekeza hadi mnavunja ndoa zenu pasipo na sababu za msingi.



Hivi jamani huko kwa wachungaji wenu wana maombi tofauti na ninaowajua mimi ninaoenda au?

Maana napatwa maswali mengi mbona mimi sichelewe kurudi nyumbani kwangu na wala si mkeri mwenzangu nafika nyumbani kwangu kwa wakati na kutekeleza majukumu yangu.

Vipi wanawake wenzangu mnaochelewa majumbani kweni mnakuwa na maombi mapya kila kukicha au? Maana sioni sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani kwako ama kulala kanisani wiki nzima bila kujua kinachoendelea nyumbani kwako.

Hata mchungaji wako anapaswa kuwa na huruna na ndoa yako ikiwezekana hata kukumbusha majukumu yako lakini anavyokaa kimya napatwa na mashaka.

Wanawake wenzangu ulokole una nafasi yake na mume ana nafasi yake acheni kuwaendekeza wachungaji weni ndoa zao zinadumu yako inavunjika kwa kukosa maarifa .



Hivi kweli mume akichepuka utamlaumu nani? Jirekebisheni hiyo tabia mnawakwaza sana wanaume zenu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yenu ukiulizwa nimeokoka

Kwani kuokoa ndio kigezo cha kushindwa kusimamia ndoa yako. Ndoa ni agano na mwenzako sio kitu cha mchezo mchezo kama unavyochukulia, hivyo unapaswa kuheshimu hilo agano.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger