juu

Saturday, 5 October 2019

Zifahamu faida za kukusahau na kusamehe mpenzi wako wa zamani

Image may contain: 1 person, smiling, standing and text
Una hasira, una uchungu, una maumivu makali katika moyo wako, unatamani kulipa kisasi, unatamani kumuacha, unatamani kupata mtu anayekupenda na kukujali ili aumie! Je, ukimuacha hasira yako itaondoka, na je, inawezekana kupata mwingine ambaye mtaishi bila kukoseana pasipo jitihada zozote?
Ngoja nikwambie kitu, mahusiano mazuri yanatengenezwa. Hasira, uchungu na kisasi vinakutafuna na havitakuacha salama. Kilichopo ndani lazima kitajidhihirisha nje na bila shaka utapata magonjwa usostahili. Hakika nakwambia, huwezi kutengeneza ukiwa na chuki, hasira na uchungu vitu hivyo ni lazima vitajidhihirisha ktk matendo yako. SAMEHE kwaajili ya Mungu wako, samehe kwaajili ya afya yako, samehe kwaajili ya furaha yako, samehe kwaajili ya future yako, samehe saba mara sabini, samehe na utengeneze furaha yako upya.
Mungu hawezi kukupa mtu wa kukupenda ili ulipe kisasi, kisasi si cha mwanadamu, kisasi ni cha Mungu. Na hatakaa akupe kwasababu hujui kusamehe ni UTII. Samehe na mwachie Mungu atengeneze, kama moyo wake anaufanya kuwa mgumu basi kisasi cha Mungu ki mlangoni kwake.
Sio rahisi kusamehe kama umebeba uchungu mwingi, mwambie Mungu akusaidie na kukufundisha kusamehe. Inachukua muda lakini usijali kwamaana kadiri unavyosamehe ndivyo unavyojiponya.
Hasira na uchungu ni sawa na saratani inayosambaa ndani ya mtu kidogo kidogo, inaathiri nafsi yako na mwili wako. Maandiko husema, “usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu. Mwenye kutunza hasira ni mpumbavu kwamaana hasira inamdhuru yeye na si aliyekasirikiwa”.
Share:

Ukitongoza Mwanamke Mrembo Usithubutu Kumwambia Unafanya Kazi Hizi, Atakukataa Mchana Kweupe!



1.Ualimu
2.Askari magereza
3.Fundi ujenzi
4.Kondakta/utingo
5.Mgambo

Ila ukisema unafanya kazi maeneo haya, utakubaliwa asubuhi na mapema
1.Migodini
2.Siasa
3.Ikulu
4.Bandarini
5.Viwanja vya ndege
6.Bank
7.Mahospitalini.
6.Ubalozini.
Share:

Hatua Za Kufanya Kama Mwanamke Hataki Kujibu Texts Zako



Unafukuzia mwanamke mzuri mnaanza kuzungumza. Mnachukua muda wa dakika 20 hadi 30 kuongea na yeye mara ya kwanza. Anapendeza na kuvutia, na unaona kama ni mwanamke ambaye ni yule aliyekuwa ndotoni mwako maishani mwako. Mazungumzo yenu yanaenda vizuri mpaka ukwamwomba namba yake.
Baadaye unajaribu kumtumia text na hazijibu. Labda mnaeza kuchat kwa madakika halafu baada ya hapa anakataa kujibu texts zako. Unabaki ukijiuliza maswali ni kitu gani ambacho umefanya ambacho umekosea. Ok labda anaweza kuwa yupo buzy unampa muda kiasi ajibu text zako…unangojea masaa, siku, wiki mpaka inafikia wakati unagundua kuwa amekupuuza. Kwa nini hajajibu text zako?

So kwa nini hakujibu text zako?
Katika situation nyingi ni kuwa sababu kuu ambayo amekataa kujibu texts zako ni kuwa haukumpendeza mara ya kwanza ulipokutana naye. Ok labda sababu nyingine inaweza ni kuwa ameibiwa simu yake wakati alipokuwa akitext na wewe barabarani ama kitu kingine kama hicho, lakini hapa acha tumakinike na hatua ya kwanza uliokutana naye…yaani first impression ambayo unakudana na mwanamke yeyote.

1. Hakikisha unampendeza mara ya kwanza unapokutana naye
Anaweza kuwa hana muda mrefu wa kukaa na wewe ili akutambue zaidi so kile kitu ambacho unahitaji kufanya ni kuwa lazima uuonyeshe upendo wako kwa kuwa mpole, mkarimu na mtulivu. Hii itamfanya yeye kumakinika na labda kutaka kukufahamu. Hakikisha kuwa wakati unapoongea na yeye tumia mbinu za kuonyesha kuwa ungependa kukutana na yeye wakati mwingine. Kama hakuonyesha dalili zozote za kukuelewa basi hata kama atakupatia namba yake ya simu fahamu ya kwamba itakuwa ni kazi bure.
2. Taja sababu zako za kuongea na yeye
Mfano: Nimefurahia sana kuongea na wewe. Kusema kweli nimependa maonezi yetu machache. Nataka kwenda lakini naonelea wikendi nitakutext tukutane ili tuongee tena. Hapa utakuwa umeeleza ajenda yako kwake hivyo ukianza kuchat na yeye baadae haitakuwa vigumu kwake kukujibu.
3. Hakikisha kuwa unamtumia text wakati ufaao
Ukiomba namba ya simu kwa mwanamke inamaanisha kuwa wewe umeonyesha intrest kwake vilevile mwanamke akikupatia namba yake ya simu inamaanisha kuwa labda itakuwa amependezwa na wewe. Lakini je, ni muda upi unaotakikana hadi umtext mwanamke huyo.
Wanawake wanapenda kuona wanababaikiwa na kufukuziwa. So usijaribu kumtext hapo hapo wakati amekupatia namba yake. Hakikisha umejibatia shughli nyingi ili usahau kabisa kama uchukua namba kwa mwanamke. Masaa mazuri ambayo yangekuwa sawa ya kumtext ni baada ya masaa 24 baada ya kuchukua namba yake. Hii itamfanya mwanamke yeyote kujiuliza maswali ya kwa nini umechukua muda mrefu kumtext. Itamfanya kuingiwa na maswali ya kama: kwani hajapenda chat yangu? yuko na mwingine? nk. Ukichukua muda huu mrefu hadi kumtext, itakuwa rahisi kwake kukujibi.
ONYO: Hakikisha ya kwamba haupitishi zaidi ya siku tatu kwani anaweza kukusahau kwa haraka ama kuona unampotezea wakati wake.
4. Kitu cha kuandika kwa text yako ya kwanza
Messages za kwanza ambazo utazituma kwa mwanamke zitachangia pakubwa kuona kama wewe uko uko interesting ama unaboa. Unaweza kuuharibu mchezo mzima kama iwapo utaanza kumtext na mambo ambayo hayana manufaa kwake. Kile kitu unachohitajika kufanya hapa ni kuonekana hauna haraka na ujaribu kutumia lugha za kirafiki. Mfano unaweza kujaribu kumtext swala ambalo aliligusia kwa chat iliyopita. Labda aliongea kuhusu kwenda shopping na nduguyake, so swali lakini linaweza kuwa: Je ile shopping yenu na nduguyako iliendaje?. Hii itamfanya kuwa interested na wewe manake ataona ya kuwa ulikuwa umemakinika wakati mlipokuwa pamoja. Hii itamfanya kujibu text zako mara kwa mara bila yeye kuchoshwa.
5. Jaribu kuhepa stori ambazo hazitafikia popote
Mara ya kwanza anaweza kukujibu lakini itafikia pahali atanyamaza. KUMBUKA: Siri kuu ya kumfanya mwanamke ajibu texts zako ni uwe makini kwake, yaani unamtext vtu ambavyo unajua yuko intrested navyo.
6. Weka wazi kuwa unataka mkutano
Acha stori za kumzungusha huku na huku kama wanaume wengine. Ukitaka akujibu text zako hakikisha ya kuwa unadhihirisha azma yako kwa kumwambia kuwa unataka kukutana naye.
7. Usikate tamaa
Kuna wanaume wengine kama wamekataliwa kujibiwa texts zao mara moja basi wanakasirika na wanaachana kabisa na kushungulika tena. Tatizo labda linaweza kuwa mwanamke anakupima akili aone bidii yako kwake. Kama tujuavyo tabia za wanawake ni kuwa hawapendi kuonekana kama ni watu wa kukubaliana na kila kitu hivyo basi wakati mwingine wanakuwa hawaeleweki. 
Ukiona mwanamke amekataa kujibu text yako kwa siku tatu, fanya kumtext tena huku ukionyesha kuwa hauna intrest naye sana vile halafu achana naye. Hii itamfanya yeye kuona una interest na yeye lakini hauna haraka. Baadaye anaweza kuanza chat yeye mwenyewe.
KUMBUKA: Kuna sababu tofauti tofauti ambazo zinaweza kumfanya mwanamke kukataa kujibu texts zako. Labda umemtusi, hujampendeza, ni mwanamke mwenye haya nk. So hizi hatua zitategemea na vile imetokea katika situation yako
Share:

SIRI YA NDOA BORA/PENZI

Image result for siri za mapenzi blog
Upendo wa kweli,nguzo muhimu ya kuwa pamoja ni upendo.Kama miongoni mwenu(wenza au wanandoa) kuna upendo wa kweli ni rahisi sana kuweza kusawazisha mambo yanayowakabiri au vikwazo mnavyopitia kila siku.Kukubaliana na hali mbalimbali katika maisha kama vile shida na raha yote hiyo hutokana na upendo wa dhati baina yenu.Inaeleweka kuwa ni vigumu sana kwa wanandoa au wapenzi kutambua upendo au mapenzi ya kweli,lakini hiyo siyo shida sana maana njia rahisi ni kupitia matendo au maongezi anayo toa mwenza wako unaweza ukatathimini na kujua nini anamaanisha.
Ushirikiano(nafasi ya kujieleza),hii inahusu zaidi wakati wa kutoa maamuzi au uchangiaji wa mawazo katika kujenga wazo fulani.Kweli kuna wakati hutokea mmoja baina yenu humhitaji kutoa wazo lisilojadiliwa(ni kama kusema anataka kufanya kitu ambacho ni lazima kifanyike kama kilivyo bila nyongeza au punguzo lolote lile),lakini siyo kila muda inatokea hivyo au mara nyingi itokee hivyo.Kutokupata nafasi ya kujadiliana au kuchangia inaweza kutafsiriwa kuwa wewe huwezi chochote au mawazo yako hayana maana yoyote kwake, na ndipo uhusiano unapoanza kutetereka zaidi.
Umoja/mshikamano,kusimama pamoja wakati wote iwe wakati wa furaha au shida inaleta uhamasisho wa kuamini nia ya mwenza wako.Ni muhimu kusaidiana wakati wote wa maisha ingawa mnajuana namna mnaendesha maisha yenu,kosa kubwa ambalo wengi tunalifanya ni kufanya maisha ya kimazoea kwa mwenza wako kwa vile labda mnaishi pamoja(kwa wanandoa) na kuona hakuna umuhimu wa kumfariji au kumshauri.Ndio maana inapotokea mmoja wenu akachepuka(kutoka nje ya ndoa) atamwona mchepuko anamthamini sana kuliko aliyenaye ndani siku zote.
Imani na kuaminiana,ni muhimu  na vyema kujenga imani ya kuwa mwenza wako anakupenda na anakuthamini kabla ya kuanza kukusanya mabaya yake tu.si kazi rahisi kuja kukubaliana na hoja hii,lakini cha muhimu ni kama ukishajua mwenendo wake wa kawaida unaweza kutatua matatizo yote yanayo kukabili kisaikolojiaau kifikra.Kumwamini mwenza wako ni njia pia ya wewe kuwa na msimamo makini pale unapokutana na vishawishi toka upande fulani ikiwemo kwa maisha ya kawaida, marafiki, wazazi au kimapenzi.Mara nyingi kutokuaminiana matokeo yake huwa ni kutoka nje ya ndoa au uhusiano kwa madai ya kukomoana na mwenza wako.Hilo huwa siyo suluhisho bali ni kuongeza tatizo jipya lisilo na majibu hasa pale itakapothibitika kuwa huyo mwenza wako hakuwahi kufanya hivyo.
Kipato,suala la kipato katika uhusiano au ndoa ni jambo lenye kipaumbele kikubwa na inaweza ikavuruga au ikajenga ndoa bora sana.Kwanza kipato hupunguza kuangukia katika vishawishi hasa kimapenzi(mapedeshee na mashuga mami<sugar mumy>).Pili huondoa migogoro ya wapenzi kama vile kugombea mahitaji muhimu(chakula, mavazi, malazi, afya).Tunaposema kipato haijalishi ni cha mtu mmoja au kwa ushirika wenu wote wawili,ili mradi inaweza kukidhi mahitaji yenu.
Uwazi na ukweli,kusema ukweli mbele ya mwenza wako kunadumisha sana uhusiano wenu na kuaminiana zaidi.Maana kama leo umedanganya na ukagundulika basi hata kesho ukisema chochote italazimu mwenza wako afanye upelelezi wa hilo jambo kwanza ndio akupe jibu.Kitu ambacho hata wewe mwenyewe kitakupa karaha na kuona unaonewa au hupendwi.
Uvumilivu na utulivu,katika uhusiano kuna milima na mabonde ya vikwazo mbalimbali.Kustahimili vikwazo ni lazima wewe mwenyewe kwanza uwe tayari kutokuwa mropokaji wa mambo hasa kwa mwenza wako.Ukipokea jambo lo.lote linalohusu mwenza wako ni vema ukatulia na kulichambua ukweli wake kabla ya kumparamia kwa ugomvi wakati hujui aliyekupa taarifa hiyo alilenga nini.Wapo watu ambao hutamani sana mgawanyiko wenu na siyo umoja mlionao,kwa hiyo ni muhimu kuchunguza sana mambo na siyo kukurupuka mana unaweza ukakosa hata ukweli wa jambo la kweli na ukaonekana ni mkorofi tu.
Kusamehe,upendo wa kweli hubebwa na kitu kinachoitwa msamaha.kukosekana kwa msamaha katika uhusiano ni wazi penzi lenu litaishia SHUBIRI.Hakuna binadamu mkamilifu,hivyo ni ukweli kuna wakati kosa litatokea lakini kama inawezekana jaribu kusamehe maana hata mwenza wako kuna mambo ambayo huwa anasamehe pengine hata kabla ya kukuuliza.Kumbuka kuwa kinara wa kupaisha mambo kwa mwenza wako inaweza ikamfanya naye aone kuwa ndio utaratibu au njia bora ya kufanya na siku ukikosa kidogo tu utaona namna anavyokuja juu hata utajiona labda hupendwi.
Kutunza na kupambanua mambo,unapopokea jambo lolote ni muhimu kulipambanua wewe binafsi na uchukue hatua za kufanya.Kupambanua ni kujiridhisha ukweli wa kitu husika na kupata suluhisho lake.Ni hatari kutunza matukio mengi akilini mwako bila ya kuyatolea utatuzi wake maana hupelekea kuleta hasira za haraka sana wakati unapopokea tukio jipya, hii inaweza kuleta mtafaruku wa haraka sana dhidi yenu.
Pia ni muhimu sana kujitambua na kutambuana baina yenu wenza au wapenzi,maana tumetoka familia mbili tofauti na kufanana kwenu mara nyingi ni kwa vitu muhimu tu kwa jamii.Kuna watu asili yao ni wasiri na wengine ni wepesi wa kujitangaza hasa kiuchumi au mipango,unapo kutana na mpenzi ambaye ni msiri ni vizuri ukaendana naye mtindo huo mana kutoa mambo yake hadharani kutakuletea migogoro muda mwingi na hata inaweza kuleta uvunjikaji wa uhusiano.
Share:

Jinsi ya kuamsha mahaba na mapenzi katika mahusiano

Hizi hapa njia za kuamsha na kudumisha uhusiano mzuri kati yako na mpenzi wako hasa baada ya kuwa mmeshazoeana sana na kuhisi kuchokana.
Dumisha faragha katika mahusiano yenu
Hakikisha kunakua na faragha katika mahusiano yako na mpenzi wako. Vile vile itahakikisha kuwa wewe na mpenzi wako mnakuwa na wakati wa kutosha kustarehe bila wasiwasi. Usiruhusu siri zako na mwanamke zitoke nje kati yenu.
Tenga muda wa kustarehe pamoja
Ili kudumisha mahusiano na mwanamke lazima kuwepo na mda wa kuwa pamoja na kufanya mambo yenu mnayoyataka kwa kuridhika bila kupungukiwa na muda. Kwa mfano ni muhimu kupumzika mapema kitandani ili kuhakikisha mnakuwa na wasaa wa kutosha wa kufanya mapenzi.
Ongeeni pamoja kwa uhuru kuhusu suala la tendo la ndoa
Ni muhimu kujadili na kukubaliana na mwanamke kuhusu swala la kufanya mapenzi. Ni vyema muongee kuhusu suala la mapenzi na jinsi ya kuwasha moto wa mapenzi baada ya kuchokana. Mwanamke anatakiwa apewe uhuru wa kusema kile anachokihitaji.
Pangeni miadi ya usiku
Mwanamke huridhika zaidi katika mapenzi kwa kuandaliwa ipasavyo hii ikiwa ni pamoja na kuwa na utayari wa kufanya mapenzi. Hivyo ni vyema kupanga miadi ya usiku ili mwanamke awe tayari na ili kumridhisha mwanamke.
Badilisha mazingira
Njia nyingine ya kuamsha mapenzi ni kubadili mazingira ya kufanyia mapenzi. Kwa mfano mnaweza kuacha kitanda chenu cha nyumbani na kulala katika chumba cha hoteli iwapo uamuzi huo utaboresha mapenzi kati yenu.
Share:

Mambo yanayoweza kuteka moyo wa mwanamke .



Upweke, kwa hakika, huzaa migogoro isiyokwisha inayowafanya wanaume [ambao kimsingi ndio wasababishi wa upweke huo] washindwe kuwaelewa wanawake. Kwa mtazamo wao, ni vigumu kumridhisha mwanamke. Wengine wanaenda mbali na kufikiri , ‘mwanamke ni kiumbe mgumu kueleweka’ kwa sababu, ‘hata ufanye nini…hata umpe nini hawezi kuridhika’.
   Lakini wanachosahau wanaume wenye mawazo haya ni kuwa mwanamke kwa asili yake anayo mahitaji ya msingi ambayo yanapopuuzwa, chochote kinachofanyika kama mbadala wa mahitaji hayo hakiwezi kuwa na maana yoyote. Usipoweza kujua mahitaji yake halisi, unaweza kumpa chochote kile unachodhani anakihitaji na bado mambo yasiende kama unavyotamani iwe.
Kusema hivyo, haimaanishi sielewi kuwa wapo wanawake wengi wanaopenda kujipatia fedha kwa wanaume. Hawa ni wanawake wanaofanya biashara ya mahusiano.  Kwao, hakuna sababu yoyote ya kuwa na uhusiano imara na wenzi wao isipokuwa mpangilio wa kujipatia vitu na fedha.
Hatuzungumzii uhusiano huo wa kibiashara kati ya mwanamume na mwanamke bali uhusiano wa dhati unaojengwa katika misingi ya upendo, uaminifu, kuelewana na ahadi ya kuwa pamoja katika dhiki na raha.
Hebu na tutazame mahitaji makubwa ya kihisia aliyonayo mwanamke mwenye upendo wa dhati kwa mwenza wake.
Kupendwa kwa vitendo 
Tulishaona kuwa hadhi ya mwanaume inategemea kwa kiasi kikubwa namna anavyoheshimiwa. Kwa mwanamke hali ni tofauti. Hadhi yake inategemea namna anavyopendwa na mwenzi wake.
Upendo kwa mwanamke unaeleweka anapoambiwa bila kuchoka na kuthibitishiwa kwa kutendewa vitendo kuwa anapendwa. Katika lugha ya kiingereza, hapa tungetumia neno affection, yaani matendo yanayoonesha mapenzi kwake.
Hata hivyo, lugha ya mapenzi hutegemea mambo mengi. Kuna athari za utamaduni, desturi na imani zilizopo katika jamii aliyokulia mwanamke. Hata hivyo, yapo matendo yaliyothibitika kuvuka mipaka ya kiutamaduni.
Mfano, kumwambia mwanamke unampenda mara nyingi iwezekanavyo, ni hitaji la msingi. Kwa mwanamume, kuambiwa anapendwa inaweza isiwe jambo la maana, lakini si kwa mwanamke.
 Mwanamke anatamani kusikia mara nyingi kadri inavyowezekana kuwa anapendwa.
Pia kuna vitu kama kupewa zawadi asizotarajia, kutumia muda wa mapumziko pamoja nae, kutoka naye kwenda mbali na nyumbani na mambo kama hayo yanayoonesha kuwa kweli unampenda.
Ndio kusema, ikiwa unataka kuugusa moyo wa mwanamke, akupe heshima unayoihitaji kama mwanaume, unawajibika kujua vitu gani mahususi ukimfanyia vinatuma ujumbe wa wazi kuwa unampenda. Usipoweza kumfanya mwanamke ajisikie kupendwa, anapoteza hamu ya uhusiano.
 Huchoka kihisia na anaweza kufanya mambo yasiyotarajiwa ili tu kuhujumu mahusiano.
Anataka kuwa kipaumbele chako
Mwanamke hapendi kujikuta katika mazingira ya kushindania nafasi ya kwanza na kitu kingine chochote iwe ni kazi, mtu au chochote kile unachokipenda wewe mwanamume.
Tulishaona kuwa kwa mwanaume, hadhi yake hutegemea zaidi namna uwezo wake unavyotambuliwa. Hali hiyo humfanya mwanamume atumie muda mwingi kufanya mambo yanaweza kumpa heshima katika jamii. Inaweza kuwa kazi, biashara, mamlaka na namna zozote zile zinazomwongezea uwezo.
Lakini wakati anapotumia muda mwingi katika mambo hayo, ni rahisi kuonekana ameyafanya mambo mengine kuwa ya muhimu kuliko uhusiano wake na mwenzi wake. Wanawake wengi hawapendi kujikuta katika hali hii. Hapa ndiko iliko tofauti.
Mwanamke hatamani kuwa kwenye nafasi ya ‘mengineyo’, ‘ziada’, ‘baadae’ ‘nikipata muda’. Unapomweka ‘akiba’ mwanamke hawezi kufurahia kwa sababu anatamani awe kipaumbele chako.
Mambo mengi huthibitisha kuwa umempa nafasi ya kwanza. Mfano kuwa na muda wa kuwa naye mara nyingi kadri inavyowezekana, kuahirisha mambo mengine ya muhimu kwa ajili yake, kuwahi miadi unapoahidi kukutana nae, kuwasiliana naye kwa karibu na mambo kama hayo. Unaposhindwa kufanya hivyo, mwanamke hupata ujumbe kuwa yeye ni mtu wa ziada baada ya mambo ya muhimu.
Kadhalika, ili kumwambia yeye ni kipaumbele, mwanamke anatamani kila unapoongea nae akili yako yote iko pamoja naye. Kuwa pamoja naye maana yake ni kuachana na vyote vinavyokuondolea uzingativu na kumsikiliza kwa makini.
Mwanamke anatamani unapozungumza naye ufuatilie anachokisema, umpe mrejesho kuwa unamwelewa na uonesha kuwa mwili, akili, hisia ziko pamoja naye kumsikiliza. Vinginevyo, mwanamke anakuoana kama hujaweza kumpa nafasi yake anayoistahili.
Share:

Njia nyepesi ya kukonga moyo wa mwanamke pasipo gharama.

Mawasiliano mazuri kati ya mke na mme ni muhimu sana kwa ajili ya ustawi wa mahusiano ya wawili wapendanao. Inasemwa kuwa kuvunjika kwa mawasiliano pekee katika mahusiano kunasababisha mifarakano au kuvunjika kwa mahusaiano kati ya mke na mme kuliko sababu nyingine.

Wataalamu wa mapenzi na hisia za binadamu wanaeleza kuwa wanawake wanaguswa sana kwa maneno kuliko vitendo. Sauti na maneno mazuri ni vitu ambvyo vinawafanya wawe katika wakati mzuri sana kihisia. Wanaume wao wamefahamika kuwa wanavutwa zaidi kwa kuona kuliko kusikia.

Kwa msingi huu basi ni muhimu sana kwa wanaume walio katika mahusiano ya mapenzi kufahamu siri hii juu ya wenza wao wanawake. Ukitaka kuifanya siku ya mpenzi wako nzuri basi zingatia maneno yako na sauti yako iwe katika kiwango kinachofaa.
Yafuatayo ni maneno manne muhimu kuyasema kila siku kwa mkeo na yataleta mabadiliko makubwa katika mahusiano yenu. Maneno haya yanalainisha moyo,yanajenga uaminifu,yanazidisha upendo,yanaponya majeraha ya mapenzi na yanaleta furaha kati ya wapenzi:
Wewe ni Mwanamke Mzuri
Inawezekana uzuri ni sababu mojawapo ya kumuoa au kuwa naye. Basi hakikisha unamkumbusha kila mara. Wanawake wanahitaji sana kuhakikishiwa kuwa ni wazuri na wanavutia. Ni hatari sana kama hufanyi hivi kwa mkeo,n akuhakikishia wanahitaji kusikia maneno haya. Usipomwambia kuna mtu atamwambia barabarani au kazini na hii ni hatari.
Wanawake wasio ambiwa mara kwa mara kuwa ni wazuri huhangaika sana juu ya kubadilisha mavazi yao na vipodozi. Ikibidi wanaweza wakafikia kuvaa mavazi yasiyo na heshima sana kwa mtazamo wa jamii anayoishi. Hii ni katika kutafuta mrejesho kuwa ni mzuri.
Kama anatumia sana vipodozi na wewe hupendi basi mwambie ni mzuri hasa akiwa asilia,hivyo hahitaji vipodozi vingi.
Umependeza
Hili linaendana na la kwanza hapo juu lakini kupendeza sio lazima uwe mzuri. Uzuri unaweza ukawa wa sura,umbo au tabia zake. Kupendeza ni kutokana na mapambo na mavazi ambayo mtu anavaa.
Kama kuna mambo makubwa ambayo yanawachukulia muda mwingi wanawake wengi basi ni urembo hasa wa mavazi, nywele na vipodozi. Wafanya biashara wajanja wanaweka nguvu zao eneo hili kutoa huduma za wanawake.
Wanawake wanahitaji sana kuonekana wamependeza hasa toka kwa wapenzi wao. Mrejesho huu ni muhimu kwao na kunawafanya wajisikie vizuri , kujiamini na kujiona wa thamani. Mwambie mkeo kila siku asubuhi akitoka nyumbani au kila mnapotoka pamoja. Mwambie kila akibadilisha aina ya ususi wa nywele zake.
Asante
Kwa kweli mke ndiye mtendaji wa mambo mengi nyumbani. Hata kama kuna wasaidizi bado kunahitaji uongozi na bila shaka mke ni kiongozi wa yote haya nyumbani kwa walio wengi.
Utakuta nguo ni safi,chakula ki tayari,watoto wameoshwa na kuvalishwa na mengine mengi. Kuna kila sababu ya kusema “asante”.
Asante ina maajabu makubwa kama ikitolewa kwa jinsi inavyostahili na kwa dhati. Kwanza humfanya anayeambiwa ajione wa thamani sana kwako. Pili humfanya anayefanya aongeze bidii kwa yale anayoyafanya.
Hivyo usiache kushukuru kila siku kwa yale mkeo anayoyafanya. Kunawezekana mengine yakawa si mazuri,lakini hakutakosekana zuri la kushukuru.
Mwambie “Asante Mpenzi” , “Asante Mke Wangu” na maisha yenu yatakuwa mazuri na yenye furaha.
Fanya kwa vitendo pia,mfano nunua hata kitenge tu na umshangaze kwa zawadi. Mwambie “asante kwa kuwa mama mzuri wa watoto wetu” au “Asante kwa kuwa mke mzuri na rafiki mzuri kwangu”.
Nakupenda
Kupendwa ni mojawapo ya vitu ambavyo binadamu anahitaji sana. Chukulia mtoto mfano,toka tukiwa watoto kupendwa ni kitu kinachohitajika sana na kinapokosekana kuna madhara makubwa yanayotokea ikiwemo mtoto kutojipenda mwenyewe na kutojiona wa thamani. Kwa wanawake halikadharika, japo ni wakubwa tayari lakini kasumba ya utotoni imo bado ndani yetu na mahitaji ni yaleyale.
Ukiangalia vizuri mahangaiko yote ya mwanamke juu ya urembo na mavazi utaona kuwa ni kutaka kuhakikisha kuwa anapendwa. Au kujinyima na kuishi katika mwenendo ambao wewe kama mume unafikiri ni vizuri au jamii inafikiri ni vizuri ni kutaka kuhakikisha kuwa anapendwa. Basi kwa kumtamkia kuwa unampenda mara nyingi kadili utakavyoweza inampa kujiamini kwa jinsi alivyo na kwa yale anayoyafanya.
Kumwambia mkeo kuwa unampenda na kuonyesha kwa matendo kunamfanya naye akupende zaidi.
Neno hili likitumika kwa dhati na sio kusema tu lina maajabu makubwa katika kuboresha mahusiano ya wenza wapendanao.
Bila shaka umeelewa vyema, naomba nikutakie utekelezaji mwema katika hilo.
Share:

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger