juu

Tuesday, 4 February 2020

Tuambizane tu ukweli ili tupate kilicho bora katika mahusiano ya kimapenzi

Kwenye swala zima la mahusiano ya mapenzi pesa haina chochote cha kuthibitisha. Na anayetanguliza pesa mbele katika mapenzi hana upendo wala mapenzi ya kweli.

Wanawake
Usikimbilie kumpima imani mpenzi wako kwa kumuomba pesa ili ujue kama anakupenda au laa mwanaume ni kiumbe anayeweza kufanya kila unachotaka akamilishe malengo yake.
Be careful utachezewa na utatumika sana lakini kumpata wa kuishi naye forever hutapata.

Wanaume
Kumpatia pesa mpenzi wako kila akihitaji hakumfanyi yeye akuone ni kiasi gani unampenda ila huenda ukageuzwa kitega uchumi chake. Lugha ya mjini tunaita atm yake.

Unampomuapproach mwanamke epuka kumuonyesha maisha ambayo siyo level zako maana kama utampa pesa sana kabla ya kumuoa jiandae kufanya hivyo baada ya ndoa
Ukishindwa black brother huna ndoa tena, Wahenga wanasema "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo"

Nyote
Epuka kuweka mbele katika mahusiano vitu ambayo vinaisha na kupotea kabisa kama pesa, mali na mengine mengi maana yakiisha hayo yatatengeneza hatima ya mapenzi yenu..

Busara yangu/ ushauri
Katika mapenzi siku zote tanguliza moyo wako na hisia za kweli kwa uliye naye , mpe moyo wako na yeye akupe wake ila mambo mengine mungu atawapatia mbele kwa mbele.

Kama nilichosema haifai na kimekuudhi utanisamehe lakini nimeongea ukweli na mambo ambayo yemetawala sana kwenye mahusiano ya sasa hivi.
Share:

Maneno ambayo unapaswa kumwambia mpenzi wako ili kuongeza ladha katika mahusiano

Mapenzi yanayotawaliwa na maneno matamu hunawiri na kuchanua kama mmea uliopandwa kando ya mto. Hakika maneno mazuri husadifu mambo mengi mazuri baina yenu ikiwemo upendo, kujali, kuthamini, heshima, utii, upole, nidhamu, uaminifu, unyenyekevu, usikivu, ukarimu na faraja hivyo ni vema kuhakikisha kama kweli unampenda kinywa chako daima kimtolee lugha nzuri ya maneno matamu.

Weka desturi ya kusema mambo haya kwa mwenza wako hakika inazidisha furaha na amani kati yenu..

Nakupenda
Nakupenda ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mwenza wako. Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mwenza wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko pamoja.....```

Umependeza
Kama umekuwa kwenye ndoa kwa muda mrefu, ni rahisi kujisahau katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha mwenza wako kuwa anakuvutia. Kumjulisha kuwa ulivo vaa umependeza sana’ kutamfanya ajisikie vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye.

Samahani
Kila mtu hukosea wakati fulani. Wakati mwingine hujikuta tukiongea maneno kwa hasira na baadaye kugundua kuwa hatukuwa sahihi. Ubishi hauna nafasi kwenye ndoa ya wenye furaha, hivyo omba msamaha unapofanya kosa. Omba msamaha kwa kukasirika. Omba msamaha kwa kuumiza hisia za mwenza wako..```

Nilikuwa nakuwaza
Ni muhimu kumjulisha mwenza wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu moja. Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho kinakufanya umkumbuke, mjulishe...```

Siku yako ilikuaje?
Muulize masuala ambayo mwenza wako anakutana nayo katika shughuli zake kazi kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mwenza wako kushare sehemu zingine za maisha yake kutasaidia kuumuweka sawa.```

Napenda mawazo yako.
Mwambie mwenza wako kuwa unapenda mawazo yake. Mjulishe kuwa unaona ana akili, mcheshi, anajua kupenda na ana kipaji.```

Nakuunga mkono
Mpe moyo mwenza wako kwa kumjulisha kuwa unaunga mkono maamuzi yake. Unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kujaribu kumsaidia afanikishe malengo aliyojiwekea. Maisha yamejaa vikwazo vingi, na ile hisia kuwa una mtu mwingine upande wako zinaweza kukusaidia kuvivuka. Msiwe wanandoa tu, kuweni timu. Kumkumbusha mwenza wako kuwa upo nyuma yake kutaimarisha umoja wenu.

Hakuna kama wewe.
Mwenza wako anatakiwa kuwa rafiki yako. Kama hautaki kutembea naye, basi hamkupaswa kuwa pamoja. Mfanye mwenza wako ajue kuwa yeye ni bora na hakuna kama yeye.
Share:

Sunday, 26 January 2020

Jambo hili ni muhimu sana kwa wanandoa

Kama penzi ni kujitoa sadaka "sacrificing" basi wote mnapaswa  mjitoe sadaka kikamilifu. Kama penzi ni kuwa tayari kumfia mwenzako basi wote muwe tayari kuyatoa maisha yenu kwa ajili ya mwingine.

Kama penzi ni kuhudumiana basi muwe tayari kuhudumiana. Sio mmoja anajitesa kila siku kwa ajili ya mwingine ambaye hata haoni maana ya mwenzake kuteseka.

Ni muhimu kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha kila mmoja wenu anajitoa kikamailfu kwa mwenzake. Iwe ni kazi au malezi asiwepo  mtu yeyote mwenye kumuchia majukumu mtu mwingine, kwa kisingizio mwenzangu atafanya. Ni muhimu kila mmoja wenu aelewe vyema kwamba majumu yote ni ya kwenu kwa pamoja.

Nyumba ambayo itajijengea misingi mizuri ya kushirikiana kwa pamoja ni kwamba mahusiano hayo yatakuwa ni mazuri daima na yenye kudumu milele. Usisahau, mapenzi yenye machungu na machozi mfululizo yana sumu na madhara makubwa kuliko kuwa SINGLE. Choose life. Choose happiness {Furaha}. Hivyo ni wajibu wenu kuanzia sasa kuishi maisha ambayo yatawasaidia sana kwa namna moja ama nyingine kufika mbali kwa kuhakikisha mnafanikiwa katika mambo myafanyayo.
Share:

Mambo yatakayowasaidia kuweza kuboresha mahusiano ya kimapenzi

Bustani nzuri ili iweze kuzalisha kitu ambacho ni kizuri inategemeana sana na jinsi mmiliki wa bustani hiyo jinsi anavyoihudumua. Kama hutawekeza juhudi za kutosha katika kuhakikisha bustani inakuwa vizuri muda wote ni kwamba mimea ya bustani hiyo ni lazima itakufa tu hata iwaje.

Kama ilivyo kwenye bustani hata mahusiano yenu yanaweza kuwa mazuri yenye kuwapa tulizo au mabaya kuendana na kujitoa kwenu kuyatunza na kupambana na changamoto zozote zile kwenye vipindi vya shida na raha.

Ndani ya mahusiano kuna chanagamoto nyingi sana ambapo kimsingi kama wahusika hawatakuwa makini na yale wanayoyasikia na kuyaona ni kwamba mahusiano yao hayatafika mbali sana.

Watu wataleta choko choko za kuwagombanisha kama mhusika fulani hata kuwa makini kwamba mtu anaweza kujikuta anamuacha yule ampendaye pasiyo kufanya uchunguzi wa kutosha juu wa yale aliyoyasikia.

Asikwambie mtu wangu wa nguvu, Inachosha sana pindi we unahangaika kuyapalilia, kumwagilia  mahusiano yako ya kimapenzi ili yastawi, halafu watu wengine wanakuja kwa kasi kubwa kwa ajili ya kung'oa mazao badala ya magugu. Inauma sana.

Hivyo ni wajibu wako kuanzia sasa kujua namna sahihi ya kuitunza bustani yenu ya mahusiano ya kimapenzi ili mahusino yenu yaweze kudumu daiama, Ni wajibu wenu kuhakikisha mnalinda mahusiano yenu kila itwapo leo,

Na; Benson Chonya.
Share:

Meseji nzuri za kumtumia mpenzi wako ili azidi kukupenda zaidi



  1. Wewe ni kila kitu kwangu.
  2. Nitateseka bila wewe.
  3. Ninataka nikwambie tu kuwa ninakuwaza muda wote.
  4. Ninatamani kuwa mikononi mwako muda wote.
  5. Ninakupenda zaidi ya unavyofikiria.
  6. Unafanya mapigo ya moyo wangu yaende mbio nikikuona.
  7. Najisikia vizuri mno nikikuwaza mpenzi.
  8. Ninajihisi salama nikiwa nawe.
  9. Nikiwa mikononi mwako ninajihisi nimefika!
  10. Ulishaubeba moyo wangu na sitaki uurudishe.
  11. Siwezi kuishi bila wewe mpenzi.
  12. Sitosahau usiku ule ambao tuli.
  13. Tabasamu lako linanipoteza kabisa.
  14. Unanistaajabisha kila siku.
  15. Nitafanya lolote ili niwe nawe.
  16. Ninakutamani kila saa.
  17. Ninaona fahari kuwa na wewe. 
  18. Wewe ni wangu daima na milele.
  19. Unanifaa sana mpenzi.
  20. Sijui ningekuwa wapi bila wewe.
  21. Kila siku tunapokuwa pamoja naona ninaishi ndoto yangu ya siku nyingi.
  22. Moyo wangu unasisimka ninapokuwa nawe.
  23. Hakuna mtu aliyewahi kuwa karibu nami na akanifanya nijisikie raha kama unavyonifanya nijisikie.
  24. Ninahesabu muda mpaka pale nitakapo pata busu lako tamu.
  25. Ni kama vile uliumbwa kwa ajili yangu.
  26. Wewe ni mtu pekee ambaye siko tayari kukuacha. 
  27. Kila saa wewe ndiye chaguo langu.
  28. Unanifanya nijiamini sana mpenzi.
  29. Wewe ndiye baraka kubwa niliyowahi kuipata.
  30. Wewe ni mzuri sana aisee.
  31. Nikikuwaza tu, hata niwe na siku mbaya, itageuka kuwa nzuri tu
  32. Moyo wangu unakuhitaji sana sasa.
  33. Ninatamani ungekuwepo hapa na mimi.
  34. Ninavyokupenda jamani, acha tu!
  35. Ninajihisi mwenye bahati sana kukupata wewe kama rafiki wa karibu na mpenzi pia.
  36. Hata milele hainitoshi kuwa na wewe.
  37. Natamani ungekuwepo hapa ukanishika mkono na ukanivuta kwako.
  38. Nimekuwaza siku nzima. Ahsante kwa usiku mzuri kama ule.
  39. Sikuwahi kujua kuwa unaweza kummiss mtu hata kabla hajaondoka, mpaka nilipokujua wewe ndio nikaamini.
  40. Maisha yetu pamoja ni tafsiri ya upendo.
  41. Natumai uko na siku njema, mwenzio nashindwa kuacha kukuwaza muda wote.
  42. Daima hujawahi shindwa kunifanya nitabasamu wakati wote.
  43. Najikuta nikishindwa kujizuia kutabasamu kila ninapofikiria kukuona ukirudi toka kazini.
  44. Wewe ni wangu, kipenzi cha nafsi yangu.
  45. Ninakuthamini sana mpenzi.
  46. Unanifanya nijisikie mwenye bahati sana kuliko wote.
  47. Natamani nikupe mabusu mazito kila ninapokuona.
  48. Nataka niamke pembeni yako siku zote za maisha yangu.
  49. Wewe ni mcheshi sana, unanifanya niwe mwenye furaha wakati wote.
  50. Ninashukuru sana nimekujua.
Share:

Mambo ambayo wanawake wanayahitaji kutoka kwa wanaume ila wanashindwa kusema

Kila mwanamke ana matarajio makubwa inapofika kwenye suala zima la mahusiano. Jamani wanawake tupende tusipende, kuna vitu tunatamani wanaume zetu watufanyie lakini tunashindwa kusema ukizingatia kuwa wanawake wengi tuna aibu na kushindwa kuzielezea hisia zetu za moyoni mara kwa mara.

Wanawake hutamani sana kukumbushwa na wanaume wao ni jinsi gani wanavyowapenda na kuwathamini, yaani vimeseji na vibarua vingi vingi vya kutusifia na kukiri kuwa tunapendwa. Lakini, hebu tuwe serious, ni nadra sana hilo kutokea.

Haya!!!  Hebu sisi wanawake turudi nyuma, tuanze kutafakari kidogo, ni mambo gani hasa tunatamani tusiyakose kutoka kwa hawa wanaume zetu?  Haya sasa, tuanze kuchambua mambo, kidogo kidogo tuweke vitu wazi.

Jamani wanaume sikilizeni, tambueni kuwa sisi wanawake hatuhitaji kuwaomba kila kitu! Tunachotaka sisi kwa kweli ni upendo, matunzo na kusifiwa bila shaka! Kuna orodha ndefu ya mambo ambayo tunayahitaji kweli kutoka kwenu ila kamwe hatuwezi sema, lakini yafuatayo ni mambo kadhaa yatakayokushangaza ambayo hukuwahi kuyajua kabla.

Meseji tamu ya mapenzi kila anapoamka kitandani asubuhi.

Mpe faraja na mpe moyo pale mambo yanapokuwa magumu shuleni, kazini au katika maisha yake ya kila siku.

Cheka pamoja naye pale anapokuchekesha.

Mpe sifa za ukweli pale anapobadilisha staili ya nywele au kusuka na pia anapovaa nguo mpya.

Mshirikishe siri zako ambazo usingeweza kumshirikisha au kumwambia mtu yeyote.

Jitoe sadaka, jishushe pale inapokubidi.

Msikilize kwa makini pale anapokuambia kuhusu mipango yake ya baadae.

Mshtukize kwa zawadi mara kwa mara.

Mpe muda wako kama kupiga stori mbili tatu na kucheka pamoja.

Msifie mara kwa mara na umkumbushe kuwa unampenda.

“Sasa kwanini wanawake wengi hushindwa kuomba vitu hivi?" Ukweli ni kwamba, hatutaki kuonekana wahitaji sana au wasumbufu. Tunaogopa kwamba tukisema kuwa tunahitaji haya, tunaweza kuachwa, yaani, mwanamume atakereka na kuamua kusepa! Wanawake sisi tunapendwa kujisikia wazuri na kupendwa.
Share:

Jifunze namna ya kumuacha mpenzi wako kistrabu


Inapofika mahali umemchoka mpenzi wako ni bora umwambie kwa maneno matupu tena ya bila kupindisha kwamba nimekuchoka sikutaki tena sitaki mahusiano na wewe tena nenda zako, ukieleza kifupi hivyo utaeleweka vizuri tu na kama huyo unaemwambia ana akili timamu wala hawezi kuendelea tena na mahusiano na wewe au kukulilia kama vile wewe ni mungu kwake ikiwa umemtamkia maneno mazito kama hayo.

Lakini tabia ya kuachana kwa maneno mazito yenye matusi mazito mazito yanayohusisha mpaka na wazazi na ndugu wengine ambao hawayajui hata mahusiano yenu tabia hii huwa sio nzuri kabisa, kwanza inaonyesha hujakua hata kidogo na akili yako finyu na ndogo kama tonge la ugali wa mtama.

Mwanamke au mwanaume aliekuwa ki akili cha kwanza ni lazima kinywa chake kiumbwe na maneno ya busara, hekima na adabu, no matter how/haijalishi mmeudhiana vipi katika mahusiano na mmefikia stage ya kuachana ni lazima muachane kwa busara, tabia ya kukamuliana matusi kama chunisi dume au ndimu kwenye samaki kukata shombo inaprove kwamba wewe ni zero brain kiasi gani katika maisha yako.
Share:

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger