juu

Sunday, 26 January 2020

Mambo ambayo wanawake wanayahitaji kutoka kwa wanaume ila wanashindwa kusema

Kila mwanamke ana matarajio makubwa inapofika kwenye suala zima la mahusiano. Jamani wanawake tupende tusipende, kuna vitu tunatamani wanaume zetu watufanyie lakini tunashindwa kusema ukizingatia kuwa wanawake wengi tuna aibu na kushindwa kuzielezea hisia zetu za moyoni mara kwa mara.

Wanawake hutamani sana kukumbushwa na wanaume wao ni jinsi gani wanavyowapenda na kuwathamini, yaani vimeseji na vibarua vingi vingi vya kutusifia na kukiri kuwa tunapendwa. Lakini, hebu tuwe serious, ni nadra sana hilo kutokea.

Haya!!!  Hebu sisi wanawake turudi nyuma, tuanze kutafakari kidogo, ni mambo gani hasa tunatamani tusiyakose kutoka kwa hawa wanaume zetu?  Haya sasa, tuanze kuchambua mambo, kidogo kidogo tuweke vitu wazi.

Jamani wanaume sikilizeni, tambueni kuwa sisi wanawake hatuhitaji kuwaomba kila kitu! Tunachotaka sisi kwa kweli ni upendo, matunzo na kusifiwa bila shaka! Kuna orodha ndefu ya mambo ambayo tunayahitaji kweli kutoka kwenu ila kamwe hatuwezi sema, lakini yafuatayo ni mambo kadhaa yatakayokushangaza ambayo hukuwahi kuyajua kabla.

Meseji tamu ya mapenzi kila anapoamka kitandani asubuhi.

Mpe faraja na mpe moyo pale mambo yanapokuwa magumu shuleni, kazini au katika maisha yake ya kila siku.

Cheka pamoja naye pale anapokuchekesha.

Mpe sifa za ukweli pale anapobadilisha staili ya nywele au kusuka na pia anapovaa nguo mpya.

Mshirikishe siri zako ambazo usingeweza kumshirikisha au kumwambia mtu yeyote.

Jitoe sadaka, jishushe pale inapokubidi.

Msikilize kwa makini pale anapokuambia kuhusu mipango yake ya baadae.

Mshtukize kwa zawadi mara kwa mara.

Mpe muda wako kama kupiga stori mbili tatu na kucheka pamoja.

Msifie mara kwa mara na umkumbushe kuwa unampenda.

“Sasa kwanini wanawake wengi hushindwa kuomba vitu hivi?" Ukweli ni kwamba, hatutaki kuonekana wahitaji sana au wasumbufu. Tunaogopa kwamba tukisema kuwa tunahitaji haya, tunaweza kuachwa, yaani, mwanamume atakereka na kuamua kusepa! Wanawake sisi tunapendwa kujisikia wazuri na kupendwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger