Saturday, 1 June 2019
Sifa za Mahusiano ya Kudumu Katika Mapenzi

Kikubwa kinachotafutwa na wapendanao huwa ni furaha ya moyo. Wapendanao wanapaswa kuishi kwa furaha, amani na upendo. Uhusiano wao uwe sehemu ya kudumisha urafiki, udugu na kwa pamoja muweze kuishi vizuri.
Wapendanao wanatengeneza umoja wao ambao ni wa kutiana moyo pale mambo yanapokuwa si mazuri. Wakati wa matatizo na wakati wa furaha wanakuwa pamoja, wanategemeana katika kuifanya safari yao ya hapa duniani iweze kutimia sawasawa na mpango wa Mungu.
Kwa kuzingatia hilo, kila mmoja anapaswa kuwa furaha ya mwenzake. Anapaswa kumtendea mambo mazuri ili aweze kuwa na furaha na amani muda wote. Mwanaume anapaswa kushughulikia amani na furaha ya mwanamke wake, vivyo hivyo mwanamke ashughulikie furaha na amani ya mwanaume wake. Kuna vitu ambavyo mara nyingi huwa tunaviona ni vidogo lakini kimsingi huwa vina maana kubwa sana katika suala zima la uhusiano wa kimapenzi kwa mchumba au hata hatua ya ndoa.
Vitu hivyo ni pamoja na:
Mitoko ya hapa na pale.
Mara nyingi wapendanao huwa wanajisahau sana katika suala zima la mitoko ya hapa na pale. Mara nyingi kila mtu anajua kutoka kivyake na marafiki zake.
Mwanaume anatoka kwenda hoteli au sehemu mbalimbali za burudani na rafiki zake na mwanamke naye anatoka na mashoga zake. Ndugu zangu, hata kama kweli kila mtu ana mitoko yake lakini ni vyema kujiwekea utaratibu siku moja moja wapendanao mkatoka pamoja, ina maana kubwa sana katika suala la kujenga mahusiano yenu ya kimapenzi.
Kupeana zawadi.
Lingine ni la vizawadi. Hata kama unajua kwamba mwenzako ana uwezo wa kununua kile ambacho wewe utamnunulia lakini fanya hivyo kama ishara ya upendo, inaleta maana kubwa sana katika uhusiano.
Toa kipaumbele kwa mwenzako.
Unapokuwa unawaza juu ya jambo fulani, mpe kipaumbele mwenzi wako kwa kuomba hata ushauri badala ya kuomba ushauri kwa marafiki zako, wafanyabiashara au wafanyakazi wenzako. Mwenzi wako anapoona humpi kipaumbele hususani katika masuala ya msingi, anaweza kuona ni kama unamdharau na hivyo kupunguza hamu ya kuwa na wewe.
Msaidie katika kufanya mambo mbalimbali.
Kuna wakati mwenzi wako anaweza kuwa anaweza kufanya jambo fulani lakini anapokuwa na wewe, anatamani wewe umsaidie, hilo nalo lina maana kubwa lifanye kadiri uwezavyo.
Mjali kwa hali na mali.
Hili ni la muhimu sana, unaweza kuona kama halina maana sana lakini unapokuwa unamkumbusha mwenzi wako kuhusu suala la kula au kumuamsha asubuhi awahi kazini na mambo mengine kama hayo, yanaleta chachu na hamasa kubwa katika uhusiano.
Ukiyazingatia haya yawezekana ukaona kana kwamba hii dunia mmeumbiwa watu wawili tu yaani wewe nay eye kwa sababu hatua na mtu mwingine zaidi ya huyo mwenza wako katika suala la mafanikio.
SABABU za Wanawake Kulia Baada ya Kufanya Mapenzi!

Kulia baada ya kushiriki ngono au kufanya mapenzi ni kawaida na hushuhudiwa sana kwa wanawake, ijapokuwa imesemekana kuwa wanaume hulia pia.
Kulingana na wataalam, kuna sababu kadhaa ambazo humfanya mwanamke kulia au kujawa na huzuni baada ya kushiriki ngono, na mojawapo ya sababu hizo ni homoni ambazo mwili wa binadamu hutoa wakati huo.
Umewahi kushiriki mapenzi na kugundua kuwa mpenzi wako amelia tu, baada ya kipindi kirefu cha kufurahisha?
Kulingana na wanasayansi, ni kawaida.
Utafiti mwingine umeonyesha kuwa kati ya asilimia saba nukta saba na asilimia thelathini na mbili nukta tisa ya wanawake wamewahi kulia baada ya kushiriki mapenzi.
Mara kwa mara, wanaume hulia pia.
Sababu za wanawake kulia baada ya kufanya mapenzi!
Mtaalam mmoja ameieleza hali hiyo kama 'hali ambayo mwanamke hushindwa kujidhibiti na kulia bila sababu, hasa baada ya kupandwa na raha ya kujamiana, au kufika katika upeo wa raha ya kujamiana (orgasm.)
Umewahi kudhani kuwa 'ustadi' wako ndio uliosababisha kulia kwa mwanamke baada ya kushiriki ngono? Pole sana!
Hata hivyo, mtaalam mwingine amesema kuwa ukweli wa mambo na mawazo yanayokuja punde baada ya kushiriki ngono kama woga, huweza kumfanya mwanamke kulia, ijapokuwa amesisitiza kuwa kulia kwa mwanamke baada ya kushiriki mapenzi ni kawaida!
Jinsi ya kuamsha mahaba na mapenzi katika mahusiano
Hizi hapa njia za kuamsha na kudumisha uhusiano mzuri kati yako na mpenzi wako hasa baada ya kuwa mmeshazoeana sana na kuhisi kuchokana.Dumisha faragha katika mahusiano yenu
Hakikisha kunakua na faragha katika mahusiano yako na mpenzi wako. Vile vile itahakikisha kuwa wewe na mpenzi wako mnakuwa na wakati wa kutosha kustarehe bila wasiwasi. Usiruhusu siri zako na mwanamke zitoke nje kati yenu.
Tenga muda wa kustarehe pamoja
Ili kudumisha mahusiano na mwanamke lazima kuwepo na mda wa kuwa pamoja na kufanya mambo yenu mnayoyataka kwa kuridhika bila kupungukiwa na muda. Kwa mfano ni muhimu kupumzika mapema kitandani ili kuhakikisha mnakuwa na wasaa wa kutosha wa kufanya mapenzi.
Ongeeni pamoja kwa uhuru kuhusu suala la tendo la ndoa
Ni muhimu kujadili na kukubaliana na mwanamke kuhusu swala la kufanya mapenzi. Ni vyema muongee kuhusu suala la mapenzi na jinsi ya kuwasha moto wa mapenzi baada ya kuchokana. Mwanamke anatakiwa apewe uhuru wa kusema kile anachokihitaji.
Pangeni miadi ya usiku
Mwanamke huridhika zaidi katika mapenzi kwa kuandaliwa ipasavyo hii ikiwa ni pamoja na kuwa na utayari wa kufanya mapenzi. Hivyo ni vyema kupanga miadi ya usiku ili mwanamke awe tayari na ili kumridhisha mwanamke.
Badilisha mazingira
Njia nyingine ya kuamsha mapenzi ni kubadili mazingira ya kufanyia mapenzi. Kwa mfano mnaweza kuacha kitanda chenu cha nyumbani na kulala katika chumba cha hoteli iwapo uamuzi huo utaboresha mapenzi kati yenu.
PENNY, HABARI YA NDOA NITASHANGILIA WENZANGU TU, MIMI HAPANA!

MTANGAZAJI wa Kipindi cha Harusi Yetu kupitia Runinga ya Magic Swahili, Penieli Mwingilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa anafurahi anapoona wenzake wakifunga na kutangaza ndoa zao lakini jambo hilo hataki litokee kwake. Akizungumza na SHUSHA PUMZI, Penny alisema kuwa, moyo wake bado hauko tayari kuingia kwenye ndoa kwa sasa mpaka atakaporidhia hapo baadaye.
“Nafanya kipindi cha harusi, lakini huwezi amini napenda sana kuona watu wakioana na kuvaa mashela vile lakini mimi sipendi kabisa kuingia kwenye ndoa. Nafsi yangu inaona wazi bado haihitaji ndoa,” alisema Penny.
The post PENNY, HABARI YA NDOA NITASHANGILIA WENZANGU TU, MIMI HAPANA! appeared first on Global Publishers.
SIWEMA AFUNGUKA KUMUONA MTOTO WAKE
MZAZI mwezie na mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay’, Siwema Edson amekanusha madai ya kutomtembelea mwanaye Cartes.
Akizungumza na gazeti hili, Siwema alisema huwa ana ratiba maalum ya kwenda kumuona mwanaye huyo ambaye anaishi na bibi yake, ambaye ni mama yake na Nay, ila anapokwenda huwa hamjulishi mzazi mwenzake huyo.

“Mtoto wangu naongea naye kila mara na nimeshaenda kumuona zaidi ya mara tatu, sema tu baba yake hajui hivyo angekuwa anamuuliza mama yake angempa jibu, lakini mwanangu nishamuona na ninaongea nae kila mara,” alisema Siwema.
Stori: Imelda Mtema
RC MAKONDA IFTAR: Nyoni, Kagere, Bocco Walivyopakua Chakula!
The post SIWEMA AFUNGUKA KUMUONA MTOTO WAKE appeared first on Global Publishers.
FAHAMU AINA ZA UGUMBA (INFERTILITY); KUJIKINGA

UGUMBA ni hali inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke wanapokutana kimwili bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi kwa muda wa miezi 12, kutoweza kupata ujauzito.
AINA ZA UGUMBA
Kuna aimba mbalimbali wa ugumba kama vile; ugumba wa asili (Primary infertility) – Hii ni pale ambapo inapotokea mwanaume na mwanamke hawajawahi kutungisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kukutana kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.
Ugumba unaotokea baadaye maishani (Secondary infertility) – Hii ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena. Asilimia 30-40 ya tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi hazijulikani.
Kwa wale wenye afya njema, uwezekano wa kupata au kutungisha mimba iwapo watajamiiana mara kwa mara kwa mwezi ni asilimia 25- 30. Wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak fertility) wakiwa kwenye miaka ya ishirini. Mwanamke aliye na umri wa zaidi ya miaka 35 (au baada ya miaka 40) ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia 10.
Mimba hutungwa baada ya mwanamke kutoa yai kutoka katika moja ya ‘viwanda’ vyake vya mayai ya kike yaani ovaries, kitendo hiki hujulikana kama ovulation. Yai husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama uterus (womb) kupitia kwenye mirija ya uzazi inayojulikana kama mirija ya fallopian. Mbegu moja ya kiume (sperm) ni lazima itungishe au iungane (fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova) wakati yai likielekea kwenye uterus.
Baada ya mbegu ya kiume na yai la kike kuungana, muunganiko uliotengenezwa yaani kiinitete (embryo) hushuka mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kujiwekeza hapo ili kiendelee kuwa kiumbe. Tatizo la ugumba linaweza likawa ni la mwanaume au mwanamke pekee ingawa wakati mwingine wote wawili wanaweza kuwa na tatizo hili. Tatizo la ugumba linaweza kutokea wakati wa: Yai au kiumbe kilicho ndani ya mfuko wa uzazi (uterus) kushindwa kukua hadi kufikia kuwa mtoto, mayai yaliyo
ndani ya mfuko wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus lining), matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa uzazi na matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai.
Tatizo la ugumba kwa wanawake husababishwa na; matatizo katika mfuko wa uzazi na shingo ya kizazi (cervix) kama uvimbe (fibroids or myomas) na birth defects, matatizo katika mfumo wa kuganda damu (clotting disorders). Sababu nyingine ni mazoezi kupita kiasi, afya iliyodhoofika (poor nutrition), matatizo ya kula (eating disoder), baadhi ya madawa au sumu, msongo wa mawazo (emotional stress), tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal imbalance) na uzito uliopitiliza (obesity).
Itaendelea wiki ijayo…
The post FAHAMU AINA ZA UGUMBA (INFERTILITY); KUJIKINGA appeared first on Global Publishers.
