juu

Saturday, 1 June 2019

FAHAMU AINA ZA UGUMBA (INFERTILITY); KUJIKINGA

UGUMBA ni hali inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke wanapokutana kimwili bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi kwa muda wa miezi 12, kutoweza kupata ujauzito.

AINA ZA UGUMBA

Kuna aimba mbalimbali wa ugumba kama vile; ugumba wa asili (Primary infertility) – Hii ni pale ambapo inapotokea mwanaume na mwanamke hawajawahi kutungisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kukutana kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.

Ugumba unaotokea baadaye maishani (Secondary infertility) – Hii ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena. Asilimia 30-40 ya tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi hazijulikani.

Kwa wale wenye afya njema, uwezekano wa kupata au kutungisha mimba iwapo watajamiiana mara kwa mara kwa mwezi ni asilimia 25- 30. Wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak fertility) wakiwa kwenye miaka ya ishirini. Mwanamke aliye na umri wa zaidi ya miaka 35 (au baada ya miaka 40) ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia 10.

Mimba hutungwa baada ya mwanamke kutoa yai kutoka katika moja ya ‘viwanda’ vyake vya mayai ya kike yaani ovaries, kitendo hiki hujulikana kama ovulation. Yai husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama uterus (womb) kupitia kwenye mirija ya uzazi inayojulikana kama mirija ya fallopian. Mbegu moja ya kiume (sperm) ni lazima itungishe au iungane (fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova) wakati yai likielekea kwenye uterus.

Baada ya mbegu ya kiume na yai la kike kuungana, muunganiko uliotengenezwa yaani kiinitete (embryo) hushuka mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kujiwekeza hapo ili kiendelee kuwa kiumbe. Tatizo la ugumba linaweza likawa ni la mwanaume au mwanamke pekee ingawa wakati mwingine wote wawili wanaweza kuwa na tatizo hili. Tatizo la ugumba linaweza kutokea wakati wa: Yai au kiumbe kilicho ndani ya mfuko wa uzazi (uterus) kushindwa kukua hadi kufikia kuwa mtoto, mayai yaliyo

ndani ya mfuko wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus lining), matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa uzazi na matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai.

Tatizo la ugumba kwa wanawake husababishwa na; matatizo katika mfuko wa uzazi na shingo ya kizazi (cervix) kama uvimbe (fibroids or myomas) na birth defects, matatizo katika mfumo wa kuganda damu (clotting disorders). Sababu nyingine ni mazoezi kupita kiasi, afya iliyodhoofika (poor nutrition), matatizo ya kula (eating disoder), baadhi ya madawa au sumu, msongo wa mawazo (emotional stress), tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal imbalance) na uzito uliopitiliza (obesity).

Itaendelea wiki ijayo…

The post FAHAMU AINA ZA UGUMBA (INFERTILITY); KUJIKINGA appeared first on Global Publishers.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger