juu

Sunday, 2 June 2019

Sifa 10 za mwanaume ambaye kila binti anayetaka aolewe angependa aolewe naye!!

Related image

Sifa 10 za mwanaume ambaye kila binti anayetaka aolewe angependa aolewe naye!!

SIFA 10 ZA MWANAUME AMBAYE KILA BINTI ANAETAKA KUOLEWA ANGEPENDA AOLEWE NAE.
1. Awe na pesa nyingi
2.Siyo lazima awe mzuri wa sura
3. Ajenge ukweni
4.Awe mpole
5.Asimuonee wivu mke wake
6.Awe mwenye upendo wa dhati
7.Asishike simu ya mke wake.
8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani
9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.
10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake
UKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Share:

Saturday, 1 June 2019

SMS nzuri sana ya Kimahaba

Related image

Nimekuapata! Kama unanichukia, nipige mshale, lakini
tafadhali si moyoni sababu hapo ndipo wewe ulipo.
Share:

Siwema wa Nay wa Mitego Akanusha Kumtelekeza Mwanaye

Image result for Siwema wa Nay wa Mitego

MZAZI mwezie na mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay’, Siwema Edson amekanusha madai ya kutomtembelea mwanaye Cartes.


Akizungumza na gazeti hili, Siwema alisema huwa ana ratiba maalum ya kwenda kumuona mwanaye huyo ambaye anaishi na bibi yake, ambaye ni mama yake na Nay, ila anapokwenda huwa hamjulishi mzazi mwenzake huyo.


“Mtoto wangu naongea naye kila mara na nimeshaenda kumuona zaidi ya mara tatu, sema tu baba yake hajui hivyo angekuwa anamuuliza mama yake angempa jibu, lakini mwanangu nishamuona na ninaongea nae kila mara,” alisema Siwema.

Stori: Imelda Mtema
Share:

KUMUOTA EX WANGU MARA KWA MARA INATOKANA NINI?

Related image

Habari za Majukumu!?

Nilikuwa na Mpenzi wangu wa Tangu Shule ya Msingi tupo wote, Sekondari Pia, Tukahitimu Tukarudi uraiani Tukiwa wote, Baadae yeye Alibahatika kupata kazi kabla yangu Akaondoka Mkoani, Baada ya miaka miwili Nami nilipata kazi Baada ya mafunzo kumalizika Nikapangiwa Mkoa Fulani, Cha Ajabu nilipofika Mkoa huo Nikakutana na baadhi ya vijana tulikuwa wote huko Nyumbani wakaniambia Kuwa Huyo binti Yupo Mkoani Hapa nilipopangwa kikazi Kwa vile Baada yeye kupata kazi Tulipoteza mawasiliano , Sasa nikaona Haina Haja Kumtafuta, Ila Siku Moja ktk Majuku ya kazi tulikutana Live kila mmoja anamshangaa mwenzie Kutokana na majukumu yetu Hayaruhusu kusogeleana Kwa Muda ule baada ya majukumu kuisha, Ililazimu tuonane tupeane Mawasiliano upya Mahusiano Yalianza Upya tena ila Mwenzangu niligundua kuwa Yupo tofauti sana ni mtu wa Sitarehe sana na ni maisha ambayo Sikuyapenda kabisa na tayari aliishapata Mchumba Huku Huku na huyo mchumba wake nae inaonekana ni mtu wa Sitarehe sana kamwambukiza huyo Binti Kukesha kwenye kumbi za Starehe kwake kawaida tu! Sasa, alitaka Amuache yule jamaa yake ili Tuanze maisha wawili kutoka na ile Tabia ya Starehe sana kibaya zaidi Tayari Keisha kuwa mnywaji wa Pombe Na Mimi situmii kilevi chochote Nikaona, Nikaona Japo Nampenda Kweli lakini nikiingia kwenye ile ndoa nitajutia hadi kufa nikamwambia Afunge ndoa Na yule jamaa yake Mimi nitatafuta mwingine, Kweli baadae Walioana lakini Alikuwa ni msumbufu sana kwangu hata baada ya kuolewa na mpaka Leo imepita miaka 3 toka Aolewe tatizo ni kuwa Namuota sana kwa wiki lazma iwe Mara 2 au 3 Tena naota ndoto za furaha sana mpaka Huwa nacheka ndotoni kutoka na Ndoto zile za maisha ya furaha nae, Asbh Wife wangu Huniambia Usiku ulikuwa unaota Unacheka nashindwa cha kumjibu zaidi kuishia kucheka tena Sasa Swali langu ni hili 

HII INATOKANA NA NINI? NA NI MUDA SANA HATUKO PAMOJA NA ISIJE KUWA USIKU HUWA NAONGEA MANENO YA MAHABA NDOTONI WIFE ANAYASIKIA ITAKUWA INAMUUMIZA SANA.

Share:

NIMEAMUA KUWAFUNGIA WOTE

Related image

Habari wakuu

Baada ya wazaz wetu kufariki na nyumba kukosa wa kuingalia ikabidi bro wangu ahamie pale yeye na mke wake japo namimi nnaishi umbali mdogo kutoka hapo hom jap sijaoa.

Sasa mwezi uliopita alikuja binti mmoja kukaa pale hom ili asubiri mambo yake yakamilike asepe kwa kuwa tuna undugu nao japo wa mbali mbal,na kiukwel alitokea kunizoea na kunipenda sana(Hisia za mapenzi) kama mjuavyo upendo haujifichi japo mimi mpaka dakika hii sijawai mfanya chochote.

Sasa mda mchache baada ya binti kuzoena namimi alianza kunijulisha jinsi ambavo bro na mke wake wananisema kwa mabaya sana yani kila sifa mbaya ni yangu na story zingine za kutunga tunga wakati siku zote najitaidi niwe bora kwao

Binafsi nligundua wamehisi huyu dada kanipenda sana sasa wanajaribu kumwambia sifa zangu mbaya ili akate mazoea namimi kabisa,ila mara zote namwambia huyu dada kuwa sio kweli ajaribu kuchunguza hata yeye akihisi wako sawa basi poa.

Sasa Juzi kanambia tena amesikia akina bro wanazungumza issue moja kwamba Mimi nliwai kuwa na mahusiano na dada flan hapa mtaani kwetu(Namjua) ambae alifariki kama miezi sita imepita na inasemekana alifariki kwa HIV maana afya yake ilizorota sana.

Sasa mimi kiukweli tangu aanze kuniambia hayo yote nimekua siyatilii maanani na hata nkiwa na akina bro nacheka nao vizuri tu bila kuonesha kwamba nnajua kwamba wananichafua sana lakini la kufikia hatua hadi kunizushia kwamba nimeshadate na mtu aloathirika nahisi limeniuma sana na nlichoamua ni kuwa sitawaambia lolote lakini pia sitawasemesha wala kujibu salamu yao wote kuanzia
Bro,mke wake na huyu dada maana nayeye inaonekana kama tayari kashakua na hofu kubwa sana namimi,So ili nisiendelee kuumia zaidi ni bora nichukue huo uamuzi na mimi nikishakuchukia huwa sirudi nyuma hata niwe na shida ipi heri nife ndani.


Naombeni ushauri wakuu je niendelee na huu msimamo au?

Share:

USIOE USIOE Narudia tena mpendwa USIOE!!

Related image



- Ukiona msichana ana ujasiri wa kuvaa nguo fupi na kuingia barabarani bila aibu akitembea USIOE.

- Úkiona msichana ana ujasiri wa kuvaa nguo ya kubana sana halafu anatembea bila aibu mtaani USIOE

- Ukiona msichana anakunywa pombe na kulewa akiwa bar USIOE

- Úkiona msichana anaujasiri wa kusimama na wanaume hovyo barabarni bila kuona aibu USIOE

- Ukiona msichana anaujasiri wa kukujibu mbovu hadharani USIOE

- Ukiona msichana anatoa hela anasuguliwa miguu USIOE

- Ukiona msichana unamtumia vocha halafu anakubipu USIOE >

-Ukiona msichana ni mjuaji juaji USIOE

-ukiona msichana ni muongeaji sanduku la maoni la mwendokasi likasome USIOE

-ukiona msichana ametendwa zaidi ya Mara mbili kwenye mahusiano USIOE

-ukiona msichana anapenda kupigia picha kwenye dressing table za lodge, kwa marafiki, saloon huku yeye dressing table yake ni dirishani USIOE

-ukiona msichana amehudhuria harusi zaidi ya tano na bado yupo kwao USIOE

-ukiona msichana kavaa mipete kumbe Hana mume wala mchumba USIOE huyo tayari keshaolewa na shetani

-Ukiona msichana anapenda Sana kupiga picha na kuonesha makalio kwa kuyabinua Kama mtetea anaandaa mazingira ya kupandwa na jogoo USIOE

-Ukiona msichana........ ENDELEA NA WEWE 

Share:

MAPENZI SIO WEMBAMBA WALA UNENE

Mwigizaji maarufu wa Bongo Movies, Riyama Ally amefunguka kuwa hapendi watu wanavyomuita mtu mzima, akisema yeye ni mdogo hasa kwa mume wake.
Riyama amesema kuwa umri wake, muonekano wake na unene wake hauwezi kumzuia kufanya manjonjo kwa mumewe.
“Mimi kwetu mwili ni asili yetu, kwahiyo hata kama nikisema niache dawa na nikiacha tu hizo dawa nitarudi kwenye ubonge na hali niliyo nayo haiwezi kunizuia kuenjoy na mume wangu”, amesema Riyama.
“Mapenzi sio wembamba wala unene, kuwa mtu mnene sio kushindwa na ndoa, sisi watu wanene ni kama oven, muda wote tunachemka”, ameongeza. 

Share:

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger