juu

Saturday 1 June 2019

KUMUOTA EX WANGU MARA KWA MARA INATOKANA NINI?

Related image

Habari za Majukumu!?

Nilikuwa na Mpenzi wangu wa Tangu Shule ya Msingi tupo wote, Sekondari Pia, Tukahitimu Tukarudi uraiani Tukiwa wote, Baadae yeye Alibahatika kupata kazi kabla yangu Akaondoka Mkoani, Baada ya miaka miwili Nami nilipata kazi Baada ya mafunzo kumalizika Nikapangiwa Mkoa Fulani, Cha Ajabu nilipofika Mkoa huo Nikakutana na baadhi ya vijana tulikuwa wote huko Nyumbani wakaniambia Kuwa Huyo binti Yupo Mkoani Hapa nilipopangwa kikazi Kwa vile Baada yeye kupata kazi Tulipoteza mawasiliano , Sasa nikaona Haina Haja Kumtafuta, Ila Siku Moja ktk Majuku ya kazi tulikutana Live kila mmoja anamshangaa mwenzie Kutokana na majukumu yetu Hayaruhusu kusogeleana Kwa Muda ule baada ya majukumu kuisha, Ililazimu tuonane tupeane Mawasiliano upya Mahusiano Yalianza Upya tena ila Mwenzangu niligundua kuwa Yupo tofauti sana ni mtu wa Sitarehe sana na ni maisha ambayo Sikuyapenda kabisa na tayari aliishapata Mchumba Huku Huku na huyo mchumba wake nae inaonekana ni mtu wa Sitarehe sana kamwambukiza huyo Binti Kukesha kwenye kumbi za Starehe kwake kawaida tu! Sasa, alitaka Amuache yule jamaa yake ili Tuanze maisha wawili kutoka na ile Tabia ya Starehe sana kibaya zaidi Tayari Keisha kuwa mnywaji wa Pombe Na Mimi situmii kilevi chochote Nikaona, Nikaona Japo Nampenda Kweli lakini nikiingia kwenye ile ndoa nitajutia hadi kufa nikamwambia Afunge ndoa Na yule jamaa yake Mimi nitatafuta mwingine, Kweli baadae Walioana lakini Alikuwa ni msumbufu sana kwangu hata baada ya kuolewa na mpaka Leo imepita miaka 3 toka Aolewe tatizo ni kuwa Namuota sana kwa wiki lazma iwe Mara 2 au 3 Tena naota ndoto za furaha sana mpaka Huwa nacheka ndotoni kutoka na Ndoto zile za maisha ya furaha nae, Asbh Wife wangu Huniambia Usiku ulikuwa unaota Unacheka nashindwa cha kumjibu zaidi kuishia kucheka tena Sasa Swali langu ni hili 

HII INATOKANA NA NINI? NA NI MUDA SANA HATUKO PAMOJA NA ISIJE KUWA USIKU HUWA NAONGEA MANENO YA MAHABA NDOTONI WIFE ANAYASIKIA ITAKUWA INAMUUMIZA SANA.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger