juu

Saturday 1 June 2019

NIMEAMUA KUWAFUNGIA WOTE

Related image

Habari wakuu

Baada ya wazaz wetu kufariki na nyumba kukosa wa kuingalia ikabidi bro wangu ahamie pale yeye na mke wake japo namimi nnaishi umbali mdogo kutoka hapo hom jap sijaoa.

Sasa mwezi uliopita alikuja binti mmoja kukaa pale hom ili asubiri mambo yake yakamilike asepe kwa kuwa tuna undugu nao japo wa mbali mbal,na kiukwel alitokea kunizoea na kunipenda sana(Hisia za mapenzi) kama mjuavyo upendo haujifichi japo mimi mpaka dakika hii sijawai mfanya chochote.

Sasa mda mchache baada ya binti kuzoena namimi alianza kunijulisha jinsi ambavo bro na mke wake wananisema kwa mabaya sana yani kila sifa mbaya ni yangu na story zingine za kutunga tunga wakati siku zote najitaidi niwe bora kwao

Binafsi nligundua wamehisi huyu dada kanipenda sana sasa wanajaribu kumwambia sifa zangu mbaya ili akate mazoea namimi kabisa,ila mara zote namwambia huyu dada kuwa sio kweli ajaribu kuchunguza hata yeye akihisi wako sawa basi poa.

Sasa Juzi kanambia tena amesikia akina bro wanazungumza issue moja kwamba Mimi nliwai kuwa na mahusiano na dada flan hapa mtaani kwetu(Namjua) ambae alifariki kama miezi sita imepita na inasemekana alifariki kwa HIV maana afya yake ilizorota sana.

Sasa mimi kiukweli tangu aanze kuniambia hayo yote nimekua siyatilii maanani na hata nkiwa na akina bro nacheka nao vizuri tu bila kuonesha kwamba nnajua kwamba wananichafua sana lakini la kufikia hatua hadi kunizushia kwamba nimeshadate na mtu aloathirika nahisi limeniuma sana na nlichoamua ni kuwa sitawaambia lolote lakini pia sitawasemesha wala kujibu salamu yao wote kuanzia
Bro,mke wake na huyu dada maana nayeye inaonekana kama tayari kashakua na hofu kubwa sana namimi,So ili nisiendelee kuumia zaidi ni bora nichukue huo uamuzi na mimi nikishakuchukia huwa sirudi nyuma hata niwe na shida ipi heri nife ndani.


Naombeni ushauri wakuu je niendelee na huu msimamo au?

Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger