juu

Saturday, 31 August 2019

Mfanye Mpenzi Wako Unayempenda Achanganyikiwe Juu Yako Na Kukupenda Zaidi.


"Kwenye mahusiano ya kimapenzi ni vizuri uzito wa mahusiano uwe pande zote mbili, mapenzi huwa matamu zaidi iwapo umpendae naye anakupenda kwa kiwango umpendacho wewe, na si vinginevyo maana tofauti na hapo mapenzi huwa kama kero au mzigo na hisia hukupelekea kujiumiza moyo na kujiharibu kisaikolojia".

Wewe ni mtu mzuri na unampenda sana msichana wako, kiasi kwamba unamkubali sana mpaka unampa dunia yako kumuonyesha unavyomjari, ndani ya muda mrefu mliopo kwenye uhusiano umeshajitoa kwa mengi, kimuda na hata kifedha, unamchukua kutoka kazini kila siku ndani ya juma ili tu asije kuchosha miguu yake mizuri na laini.

Unamsaidia kwa kila jambo analohitaji na umeacha kutumia muda wako na marafiki zako ili kusudi uwe na muda mwingi zaidi wa kutumia naye, umemnunulia gauni la gharama na vingine vingi ili apendeze bila kuchoka huwa unabadilisha ratiba zako ili ziweze kuendana na za kwake ili muwe pamoja na kumuonyesha jinsi gani alivyo na nafasi kubwa ndani ya moyo wako, na unafanya yote haya bila ya kumtaka kitu chochote kutoka kwake.

Na hata hivyo ni mara moja tu siku ule ulipokua unaumwa ambapo ulimuomba akupikie ugali na akakuchukulie mishikaki unayoipenda pale uswazi teki awei, ambapo alikataa kwa upole na kukwambia hajui kupika vizuri ugari na wewe ulikubali kwa roho safi maana hupendi kuwa kero kwake.

Sasa turudi kwenye uhalisia.

Rafiki sijui nikuambieje ili unielewe, kaka hapa unatiketi moja tu inayokwenda bila kurudi ambayo kupeleka kwenye nchi ya mvunjiko wa moyo ambapo wapo wapenzi wake wa zamani aliowaacha.
Ni muda wa kumuuliza, "Hivi ni kipi umenifanyia mimi hivi karibuni?".

Kila ukiwa unamfanyia kitu kizuri nahisi labda unaona kama unajiongezea pointi nyingine za ziada, lakini kiukweli ni kwamba kama yeye hatojihusisha na kuchangia kwa kukufanyia wewe hayo mambo mazuri unayomfanyia yeye kwenye uhusiano wenu, jua kabisa nguvu zako zitakua hazina faida yeyote ile, ni kama maji mtaroni yanayopita tu, na hapa ndipo kiumeni.com tunapokwambia kwanini!.

Kikawaida tunaweza kuwapa ushauri wanaume wengi wanaokutana na haya wavunje uhusiano tu pale mwanamke anapomtumia mwanaume bila kurudisha upendo wowote ule anaofanyiwa, hapa simaanishi yale mambo yetu mengine ya kitandani.

Lakini kama kweli umejiweka kwenye huu uhusiano kwa roho yote na unataka uhusiano uendelee kuwa wa muda mrefu lazima ufanye na yeye awekeze hisia zake na hata pesa zake kwenye huu uhusiano hata kama ni asilimia 50%.

Hapa haijarishi wewe ni tajiri kiasi gani, ni mzuri kiasi gani au ni mwanaume mwenye mahaba yote duniani kiasi gani, kama mwanamke hana kitu chochote alichowekeza kihisia, iwe ki muda au ki fedha lazima atakuacha iwapo mtu mwingine ambaye yuko zaidi ya wewe akitokea. Kama sheria za kiumeni.com zinavyosema(kama msomaji utakua unazijua), "Mtu mpya na ambaye ni zaidi yako huwa yuko nyuma anakuja, anasubiri ukosee kidogo tu", na kama hata jiwekeza kwako likija dili ambalo ni zaidi ya wewe unalompa lazima ataondoshwa tu

Bado hujaniamini tu?

Kama ukiwekeza kiasi fulani cha muda na fedha kwenye mpango flani, iwe kununua nyumba au kuanzisha biashara, utakua unajua uchungu na uzito wa kitega uchumi chako tofauti na ukiwa umepewa bure.

Sheria hizi hizi ndizo zinazofanya kazi kwenye mapenzi, ni ubinadamu kuona uzito na uchungu kwenye kitu ambacho umekiwekeza, sasa nini swali kwako, "Ni nani anayechangia sa kwenye uhusiano wenu?, ni wewe au ni malaika wako mrembo?
Fikiria kwa umakini maana uhalisia wa jibu lako tayari limeshafanya kazi kubwa kuutengeneza uhusiano wako jinsi ulivyo sasa.

Mwachie baadhi ya malipo afanye yeye...

Inabidi uwe kama vocha isiyorudishwa, fikiria kila saa msichana wako akienda kununua mahitaji yake, analipia kwa vocha na anapata muda wa maongezi, atafanya hivi kwa kipindi kirefu mpaka ndani ya muda atakuwa na muda wa maongezi ambao anaweza kuutumia kuongea kwa miaka mingi, sasa vipi kampuni nyingine ya vocha ikiingia na kumpa ofa nzuri zaidi?, kwa unavyofikiria anaweza kubadilisha kampuni?
Kama hata kuwa na muda wa maongezi mwingi na wewe, basi kuna nafasi kubwa atabadilisha kampuni bila kujiuliza na kwa upande mwingine kama atakua na muda wa maongezi mwingi wa miaka kumtosheleza maongezi yake kutokana na jinsi alivyowekeza, hawezi kubadilisha kampuni. Umeipata pointi yamgu, Rafiki?

Kazi yako...

Ni kazi yako kumfanya msichana wako awekeze muda na hela kwenye kampuni yako ya vocha ili ikija kampuni nyingine isiweze kumchukua akili kwa ofa nzuri itakazokuja nazo.
Kwa kuwa sasa hivi nimeshakuelewesha umuhimu wa kumfanya msichana wako awekeze kwenye uhusiano, sasa utafanyaje ili aanze kuwekeza?

Omba misaada: Kitu muhimu cha kuangalia sasa hivi ni misaada, kama akikupa msaada atajishauli amefanya hivyo kwa sababu unamvuto kwake na unastahili kufanyiwa hicho alichokifanya, acha sasa hivi akuhudumie vizuri, mwache sasa hivi akupikie, saa zingine mwombe aje akupitie kazini na mwache alipie baadhi ya vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wake.
Ukiishiwa vocha usione aibu kumtumia tafadhari niongezee salio mara moja moja.
Hii ni moja ya sababu hutakiwi kuweka mayai yote kwemye kapu moja, na ndio maana huwezi kumwacha mwanamke ambaye hakujali kwa sababu wanaume wengi wanakuwa wamewekeza muda mwingi na fedha kwa huyo mwanamke.

Muda ni pesa: unaweza kumwongezea hamasa zake kwako kwa kumfanya atumie muda mwingi na wewe kwa kufanya vitu unavyovipenda na sio anavyovipenda, hii itamuonyesha uzito wako kwake.
Sio mbaya kumbeba mwanamke kama dhahabu, ila hakikisha ndani ya uhusiano kila mmoja anawekeza na sio uhusiano uwe unaegemea upande mmoja tu, kama kweli anahisia na wewe basi hisia zakezitamwendesha na yeye akujali wewe kama ambavyo zinakuendesha wewe.




Share:

Kim Nana Afunguka “Mimi Sijaachika na Wala Siwezi Achika Kirahisi Hivyo”

WALE mnaopenda kufuatilia maisha ya watu mpo? Haya sasa muuza nyago maarufu Bongo Lilian Kessy ‘Kim Nana’ amesema kuwa yeye kuachika siyo rahisi kama watu wanavyodhani au wanavyoomba iwe kila siku anajiamini ni msichana mzuri.

Kim Nana aliiambia Mikito Nusunusu kuwa mikwaruzano katika uhusiano lazima itokee hivyo hata yeye ametofautiana kidogo tu na mpenzi wake Tonny Albert ’T Bway’ lakini siyo kama wameachana kama ambavyo watu wanazusha na kibaya zaidi ni kwamba asilimia kubwa ya watu wanapenda kusema mambo ambayo hawana uhakika nayo.

 “Jamani eti nimeachika na kipigo juu, mimi siwezi kuachika kirahisi hivyo kama wanavyofikiria najiamini sana, sasa watu wanapenda kuongeaongea tu mambo wasiyokuwa na uhakika nayo.“Kutofautiana katika uhusiano ni jambo la kawaida sana tu, kwa sababu hata hao wanaoongea kuhusu mimi huwa wanagombana na watu wao wakaribu,” alisema.Nana haachiki kirahisi.










Share:

Anakupenda kweli kwa mapenzi ya kweli au ni swaga za kadi yako ya benki na pesa zako tu?


"Anajua kukutumia, anajua kukushika vilivyo kihisia za mapenzi na anajua kukukamatilia vilivyo!, ila gharama alizonazo zinazidi bajeti ya serikali!."
 Tuseme kwenye muda maisha yako yana kila kitu kinaenda sawa, unasehemu nzuri ya kuishi, unava vizuri, maisha yako yanaenda sawa na una uwezo wa kujipatia chochote kile unachohitaji.
Sasa hivi umejipatia mchumba ila kila saa swali hili linakuingia akilini "Je ananipenda mie kama mie au anapenda pesa zangu?".
Hizi hapa ni dalili ambazo kiumeni.com imekukusanyia ili kujua iwapo msichana uliyenae anakupenda kweli au anachokifuata ni ujazo wa pochi yako na hela zako, misho wa siku akuache solemba na kukuumiza roho yako.
  • Anataka zawadi za thamani...
Ukiwa unampa zawadi za kihisia ambazo hazina gharama zozote, ila zina kumbukumbu flani ambayo ni spesho kwenu, kumbukumbu nzuri ya wakati flani katika mapenzi yenu atakuangalia kwa jicho baya huku akielekeza pua yake kwenye zawadi anayoitaka.
Wanawake waliopo kwa ajiri ya pesa huwa hawana hisia na zawadi zenye umaalumu wa kipekee kwenye mahusiano ila wanapendelea zawadi zilizopikiwa gharama na fedha.
  • Marafiki zake wanaishi maisha ya gharama ya juu...
Kuna usemi usemao, "Utamjua mtu kutokana na iana ya marafiki waliomzunguka", kama msichana wako anatumia muda mwingi na marafiki wenye matumizi ya hali ya juu, ujue yupo nawe ili apate hio hela ya kukidhi garama ya hayo matumizi anayoyataka.
  • Ana hamasa kubwa ya kujua hali ya maisha yako kiuchumi...
Msichana wako anakua anakuuliza sana maswali ya hapa na pale yenye marengo ya kujua hali yako kiuchumi tokea siku ya kwanza upo nae, unaweza kuchanganya maswali yake na kudhani anataka tu kujua mambo kuhusu wewe kimaisha, hapa anataka kujua kama una uwezo wa kutosha wa kutimiza mahitaji yake katika kipindi chote cha mahusiano yenu.
  • Halipii bili hata siku moja...
Bili ikija mezani utamuona anakua bize na simu au kitu chochote kingine, anakua hata haioni kama ipo pale, hawezi kujitolea hata siku moja kulipia hata soda, ukiona hivyo ujue kakupenda kwa uwezo wako ulionao na sio kitu kingine.
  • Hajiamini mbele ya wanawake wengine wenye hadhi aliyojiwekea...
Siku zote anavaa vizuri kwa nguo za gharama, vito vya thamani na aliyependeza, na anafanya vyote hivyo kwa kutumia pochi yako, na kwa sababu kawekeza sana kwenye muonekano wake hapendi wanawake wengine wanaomfanana au wenye hadhi ya juu kumshinda yeye, saa zote anakua hajiamini wakiwepo karibu.
  • Anatumia maumbile yake na muonekano wake kupata mahitaji yake...
Atafanya chochote na kutafuta udhaifu wako kwake na ana uwezo mkubwa na ukufunzi mzuri juu ya mapenzi na anajua kuutumia vilivyo kukutoa hela na anaweza fanya hivyo katikati ya kufanya mapenzi au baada kukwambia baadhi ya mahitaji yake na shida zake. 
  • Anaangalia sana hadhi...
Anatunza hadhi yake saa zote na anahakikisha inabaki pale pale kwa nguo na vito vya thamani anavyovaa, huwa hapendi kuwa karibu na watu anaohisi wana hadhi ya chini na hutumia kiburi chake na maneno ya kejeri kuhakikisha wanakaa mbali nae.
Anaonyesha kupendezwa zaidi mwanaume anapoongelea maswala ya kifedha kuliko kitu chochote kingine.
  • Anawapanda wapenzi wake...
Badala ya kupanda cheo, anawapanda wapenzi wake, ukiangalia historia yake ya mahusiano kati ya mpenzi wake aliyopita na wa sasa, wa sasa anakua na pesa nyingi kuliko yule wa zamani, anafanya hivi ili kukidhi mahitaji yake ambayo yanakua yanapanda zaidi.
  • Yupo nje ya ligi yako...
Ukimwona unajua kabisa kutokana na jinsi alivyo kwa muonekano wake ya kuwa yupo nje ya ligi yako, ukimwangalia anakila kitu kizuri, na unaweza kujiuliza anatafuta nini na mwanaume wa aina yako. 
Ukiwa na pesa nzuri ujue yupo kuongezea zaidi hadi aliyoifikia kutoka kwako.
  • Anahadhi ya kuwa na cheo...
Ukimwona unaweza sema anafanya kazi sehemu flani ila sio kiivyo!, yeye yupo bize na starehe na kula bata kwa wingi, zaidi ya hapo hana kitu anachofanya ila gharama zake ni za juu kushinda uwezo wa kipato chake na anaujuzi mkubwa wa kutumia hisia zako kulipia kila kitu anachohitaji.




Share:

Mlela Alindwa na Baunsa, Ataja Sababu








Share:

Sifa wanawake wanazopenda, wanazoangalia na kuzitafuta kwa mwanauwe...


"Kila mwanamke hupendezwa nazo, hufikiria na kusari ili mwanaume atakae kuwa nae au ambae anaye awe nazo!."
 Kila mwanamke ana orodha ya vitu anavyovipendelea kwa mwenza wake, inawezekana ikawa urefu, rangi ya ngozi au chochote kingine, mara nyingine haiwezekani kujibadilisha ili kuendana na sifa wapenzi wetu wanazopendelea.
Kuna sifa nyingine wanawake wanaziangalia kwa mwanaume ambazo hazihusiani kabisa na muonekano, hizi sifa ni za muhimu sana maana zinamtambulisha mwanaume jinsi alivyo kwa undani.
kiumeni.com wameweza kukuandalia sifa zinazokuza hamasa kwa mwanamke, na sababu kwanini kila mwanaume anatakiwa azizingatie na kuzionyesha kwa yule anayemfanya moyo wake uende mbio...

            1: Awe mwenye shauku na kujari...

Kuwa na shauku na mpenzi wako na kuonyesha jinsi gani unavyo mjari na anavyo kuvutia na sio tu kimapenzi pekee bali na kihisia pia, kuwa na shauku kwenye vitu vinavyo mpendezesha kuanzia kikazi mpaka kwenye maisha yake kijamii, mwanamke anapenda sana mwanaume anayejua kujari na kumpa msaada pale anapouhitaji.

            2: Awe anaejiamini...

Kujiamini ni jambo moja ambalo ni muhimu sana kwa mwanamke, na huliangalia kwa macho yote mawili kuanzia wakati unapomtongoza, maana wanawake wanapenda wanaume wanaojiamini na wanaojua nini hasa wanafanya na wanataka katika maisha yao, hii sifa wanaitumia ili kumpata mwenzi anaejiamini na anayeweza kuwa baba wa familia, hii sio kuhusu tu kwa jinsi unavyo fanya vitu kwa watu wengine bali kwa muuonekano wako kiujumla kwa jamii.

           3: Awe mwaminifu...

Wanawake hawapendi mtu ambaye ni muongo, hawapendi kudanganywa na kama ni kitu ilihaidi kufanyabasi na ufanye katika muda ambao umeuhaidi kufanya, zaidi ya hapo wanapenda utulivu wako kwa wasichana wengine, hawapendi mwanaume ambae ni kiruka njia, ambae hawezi kutulia kwenye uhusiano na msichana mmoja, wanawake wakiingia kwenye uhusiano, huwa wanaingia ili wakae kwa muda mrefu na wanapenda wenzi wao wawe hivyo vivyo.

           4: Awe msiri na asiyeeleweka...

Wanawake wanapenda kusisimka, hasa kwenye mahusiano mapya, na hakuna njia nzuri ya kufanya msisimko uendelee kwenye mahusiano kama kwa kuwa msiri, fanya usiri mzuri kwa kumshitukiza mpenzi wako kwa zawadi au jambo ulilolifanya kwa siri, hii huongeza hamasa ndani ya mapenzi na katika uhusiano.

             5: Awe mkarimu...

Wanawake wanapenda ukarimu na ni moja ya vitu wanavyoviomba sana kwa mungu wapenzi wao wawenavyo, kuwa mkarimu kwa yeye na watu wote wakuzungukao, hii ni sifa wanawake wakikijua unayo na upo singo lazima wakukimbilie tofauti na wanaume wanaofikiria kuwa mwanaume anapaswa kuwa mgumu, kwa wanawake hili ni tofauti.

            6: Awe anayejua kutumia maneno...

Wanawake wanapenda kufurahi na wanapenda mwanaume anayefanya wakae na furaha na vicheko, unatakiwa kutumia maneno vizuri kumfanya mpenzi wako ajisikie vizuri kuwa nawe, na hata kama amekasirika, kununa au yupo kwenye majonzi tafuta maneno ambayo yatamfanya arudishe tabasamu lake.
Hizo ni sifa sita ambazo kila mwanamke hutamani mweza wake awe nazo, na ukizitumia vizuri hakika hakuna mwanamke atakaye baduka pambeni yako na siku zote atakutamani mpaka mwisho wa maisha yake.




Share:

Mshangaze Msichana Wako Apendezwe Nawe zaidi. Iwe ndio Unamtongoza au upo naye kwenye Mahusiano kupitia Rafiki Zake.


Ufunguo wa moyo wa mwanamke huwa ni kupitia kwa rafiki zake, kama rafiki zake wakipendezwa na wewe, huyo mwanamke aliekukonga moyo basi nawe utakuwa umeanza kuuteka taratibu, kiufupi utakuwa umeupata kila kitu kuhusu yeye, namba ya mwenye nyumba wake mpaka namba ya jirani yake, ukiwafurahisha rafiki zake basi bara bara yako ya wewe na yeye imeshaanza kuwa nyeupe.

Hakuna kitu kinachomjulisha mwanamke unayemtongoza au uliye nae kuwa umetumwa na Mungu kuwa mpenzi wake kama kukuona wewe ukiwa unapatana na marafiki zake. Marafiki wa karibu wa mwanamke ndio majaji wanaokujaji kuwa ukoje, unatabia gani na kama unafaa kweli kuwa kipenzi cha rafiki yao mpenzi, maana wao ndio wanaomshauri na wao ndio nguvu ya umaa ya kimawazo kwenye kichwa cha huyo msichana umpendae.

Ila kuna sanaa ambayo kiumeni.com leo hii inataka kukufahamisha, kukujuza na kukuelekeza, sanaa ambayo ni nyepesi kueleweka na wala usiwe na shaka.

Kuwa unajua iwapo ukiparamia mti na kwenda kwa papara lazima zikutokee puani kwa mawili. Ukienda kwa kujifanya wewe ndio unaojua kutengeneza urafiki na kuwa rafiki kupitiliza lazima wakushitukie na kuondoa shauku yako kwako kwa kukuona ni mfuatiliaji tu wa kupotezea mda au mzushi flani unayewachimba kwa sababu ya rafiki yao, na pia iwapo ukienda kwa ukimya utaonekana kauzu, unaojidai na kuwaona wao sio lolote sio chochote na iwapo wakikuendekeza utamfanya rafiki yao wanao mjua tokea kitambo kabla ya wewe kuonyesha sura yakoajitenge na wao.

Nachojaribu kukufahamisha unatakiwa uwe kama maji, usiwe ya moto na usiwe ya baridi, na kiumeni.com itakusaidia kukupa maelezo ya kina ya jinsi ya kuwaingia.

1. Waulize majina yao. Kumbuka majina yao na ukiwa unayatumia usiyatumie kuwaita kwa ufupi, fanya hivyo iwapo watu wote wengine wanafanya hivyo pia.

2. Waulize maswali kuhusu wao. Uliza maswali mengi hata kama mengine yanaboa, kama kuna jambo ambalo wanataka kulifanya kwa pamoja jifanye kabisa kama unataka kulijua kwa marefu na mapana, na hakikisha ukiwa unauliza jambo hilo kuwa kama ndo umevutiwa na jambo kuliko ambavyo umeweza kuvutiwa na kitu chochote katika maisha yako.

3. Waambie jinsi ambavyo rafiki yao kipenzi anavyokuvutia na kukuchanganya. Hakikisha lugha unayoitumia sio kwa kuwalingishia kuwa huyu rafiki yao ndo mzuri kupita wao, tafuta rugha nzuri nyepesi maana unaongea na wanawake vile vile, kwa rugha isiwe kana kwamba unawaringanisha. Jua jambo moja kwa yote utakayoyaongea hapo yatakuwa kichwa cha habari baada ya wewe kuondoka, watakuongelea na kuyapima maneno yako kwa kina.

Muongelee rafiki yao kama ni mtu uliependezwa nae na amekushika rohoni, waambie kuwa jinsi unayoendelea kumjua rafiki yao ndivyo unavyoendelea kumpenda zaidi.

4. Wasifie. Ila hakikisha unakuwa na mpaka, wasifie kuhusu nguo zao, kazi zao au radha yao kwenye vitu flani flani walivyonavyo, hakikisha sifa zako zisiongelee miili yao au nyuso zao, iwapo ukifanya hivyo ujue watakuhukumu kama mtu unaevutika na kila mwanamke anaekatisha kwenye macho yako, na juu ya yote unaanza kuonyesha hisia za kuwatongoza mbele ya rafiki yao.

5. Kama upo umetoka nao kwenye mtoko, wanunulie vinywaji na kama anaishi na marafiki zake, njoo na chupa ya waini ya dompo au saint anna siku nyingine ukija, hii inamaanisha utakuwa umejitengenezea picha nzuri na kuonekana mtu muungwana, mwenye roho nzuri, usio na choyo na unamapenzi ya kweli na rafiki yao.

Kuwafanya rafiki wa mpenzi wako uliyenae au mtarajiwa wakupende na kitu kimoja ambacho kitakupa sifa nzuri sana, maana hata kama msichana hajapendezwa sana na wewe harafu marafiki wamekupenda ujue utatetewa vizuri na uhakika wa kuwa na huyo msichana umpendae utakuwa mkubwa, na kitu kimoja kuhusu wanawake, wanawake wanategemea sana ushauri kutoka kwa marafiki zao, hivyo hata kama ukiwa umekosea jambo na upo kwenye uhusiano na huyo msichana umpendae, ukiwa upo poa na marafiki zake ujue utakuwa na watetezi wa kufanya msamaha wako uwe nje nje kupitishwa.




Share:

Friday, 30 August 2019

Umuhimu wa kula ndizi katika kujitibu tatizo la nguvu za kiume








Share:

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger