Katika mahusiano huwa kuna changamoto tofauti tofauti. Kwa kawaida ni muhali kupata mahusiano ambayo hayana patashuka moja au nyingine. Inajulikana ya kuwa mahusiano huwa kuna migogoro, kutoelewana, kunyamaziana na mbaya zaidi…vita.
Anyway mambo kama haya huwezi kuyazuia kwa sababu wenyewe ndio wanayaita mapenzi. Utaskia mtu akilalamika kuwa amemiss kugombana ama kuteteshana na mpenzi wake, jambo ambalo huwa ni la kawaida.
Ok. tukija katika mada yetu ni kuwa nataka nikuulize maswali yafuatayo. Je hivi karibuni umeona kama mpenzi wako amekuwa mtu tofauti na ilivyo kawaida? Je mpenzi wako imekuwa muda mrefu tangu mfanye mambo yenu ya kawaida ambayo mlikuwa mkifanya? Je unamshuku kama amepata mwingine?
Kama majibu yako ni NDIO basi hili chapisho nimeliandika spesheli kwako na nataka umakinike kwa kusoma dalili zetu tulizoziandika na kama yote yanawiana na dhana yako basi ni wakati wa kumfungukia mpenzi wako na umwambie kweupe kuwa umechoshwa na tabia yake ya ‘kutoka nje’, na umuulize kama amechoshwa nawe ili ukate minyororo ya kuwa naye ili uwe huru.
Zama nami!
Dalili #7: Muda mwingi anajaribu kujirembua kuoneka vizuri
Kuvalia vizuri kila wakati si jambo baya la kufanya katika mahusiano, mwanzo wapenzi hupenda sana kuhakikisha ya kuwa wanampendeza mwenza wao.
Lakini, ukiona ya kuwa anamakinika zaidi na upande wa kujifanya aonekane mrembo, basi itakuwa anajaribu kumridhisha mtu mwingine kando na wewe. Kama umemgundua kuwa anajaribu kuvalia vizuri wakati anatembelea hizi sehemu basi weka ? katika mawazo yako: Kazini, supermarket, mkahawa, na hata gym! [Soma: Sifa za mwanamke mzuri]
Makinika: Zile sehemu zake za kawaida anazozienda kama amezijeuza kuwa fashion show itakuwa ni ishara ya kuwa anakucheat.
Dalili #6: Anakuwa msiri na simu yake, pakatalishi yake nk
Kila mtu ana haki ya kuwa na faragha yake. Mwanzo, watu wengi hawapendi faragha yao ishambuliwe na hata wapendwa wao. But ishu itakuja wakati ambapo anakuwa msiri kuhusu vitu vyake zaidi kuliko awali.
Hii inaweza kumaanisha kuwa kunakuwa na migogoro isioisha wakati ambapo umechukua kuangalia simu yake hadi ule wakati anaudhika wakati umeingia kwa chumba chake akiwa anatumia kompyuta yake. Ukiona mtu akianza kuwa msiri zaidi ni kuwa atakuwa anawasiliana na mchumba mwingine ambaye ako naye.
Dalili #5: Anapunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa hadi kukataa asilani
Hata watu waseme nini, kufanya mapenzi ni sehemu muhimu inayohitajika katika mahusiano. Kama hamfanyi mapenzi, utajihisi ya kuwa unabezwa na kukatalika na mpenzi wako.
Wakati umri unaposongea, utagundua ya kuwa kiasi cha mapenzi mnachofanya huwa kinapungua. Hio ni kawaida, lakini kuna hatua nyingine neno ‘ni kawaida’ linaondolewa.
Kukataliwa katakata kufanya mapenzi ama kutoa visababu inaweza kumaanisha kwa njia rahisi kuwa hajiskii kufanya mapenzi na wewe. Wakati mtu anakucheat, huwa anapoteza ule muungano wa kihisia na wewe na atakuwa hana hamu ya kufanya mapenzi na wewe
Dalili 4: Kuna yule mtu kilinge (mysterious)
Wale watu kilinge ndio unaopaswa kuwaogopa zaidi. Wanaume na wanawake kwa kawaida watakuwa na marafiki wa jinsia ile nyingine, lakini kama utamwona mpenzi wako haachi kuongea kuhusu huyo mtu basi kuna tatizo.
Hata kama nia yake ni nzuri, anaweza kuwa na kitu ambacho ni zaidi ya kuwa marafiki. Kama hatakuruhusu ukutane na huyu mtu kilinge ambaye amekuwa akipoteza muda wake mwingi naye, basi kunaweza kuwa na kitu ambacho ni zaidi ya kuchat pekee.
Dalili #3: Anazozana na wewe zaidi ya kawaida
Kukefyakefya na kukufananisha na wengine ni jambo lisilokubalika katika usuhiano. Wakati ambapo hii itatoka kuanzia mzaha hadi kuwa serious, ni ishara ya kuwa anakucheat.
Mara nyingi, mpenzi akikosana na mwenziwe hujaribu kujitenga na majibizano. Lakini ukiona ya kuwa kila wakati anagombana na wewe kwa sababu ya mahusiano yenu basi ni ishara ya kuwa kuna mwingine ambaye anamwonyesha mapenzi ya dhati…na si wewe
0 comments:
Post a Comment