juu

Saturday 14 September 2019

Nipo Kwenye Ndoa Lakini Najisikia Mpweke



Bado nahisi kutopendwa, kutothaminiwa, kutounganishwa, kutojaliwa.

Kushughukia mvutano huu kati ya kilichotokea na kitu unachotaka.

Moja ya tatizo kubwa kwenye ndoa nyingi, kuna kitu nilichokiona kutokana na uzoefu wangu ni mvutano uliopo kati ya kilichotokea na hamu iliopo , uhitaji uliopo, na kutaka kwa mtu.

Ndoa za umri wote zimekuwa na story moja, hongera wewe ambaye haupo kwenye story hii. Shauku kubwa ya ndani , Ya kuwa kitu ambacho anataka kukipata na kukizoea. Lakini mtu anajikuta kuishi na maumivu ya kutokipata kitu hicho.

Kama nilivyoona katika sehemu hizi tatu

1.Ni katika Shauku ya mtu

2.Wazo la shauku ya mtu kuweza kukamilika

3.Kushindwa kujielezea maumivu aliyonayo kwa mwenza wake ambaye anaendelea bila ya kuboresha hicho.

Shauku.

Ni kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa macho , kimetengenezwa na hamu ya shauku.Ni kitu kilichopo , kwa maneno mengine Ni shauku gani uliyonayo? Wakati mwingine tunaamini kwamba tunataka wenza wetu kufanya kitu fulani ili kupata tunachokitaka, lakini hatuelewi, kwa njia ya ndani ni kipi tunachokitaka. Nataka kujisikia kupendwa, kuwa salama, kuonekana wa muhimu, au kuthaminiwa kwa jinsi ipi? Nataka kupata muda wa kutosha? Nina maumivu ambayo nataka yapone? Nitafanikiwaje? mara nyingi tunaingia kwenye mahusiano na matarajio ambayo hatuyapati. tunaweza kukuta tofauti. hilo ni tatizo kubwa.

1-2-3 Nipo Kwenye Ndoa Lakini Najisikia Mpweke

Kwa mfano. Mimi napenda mume wangu kila anapoongea nami anishike mahali, mikono au kunikumbatia kila mara anapokutana na mimi . Lakini kama atakuwa hafanyi hivyo , nitajiona kupungukiwa kitu. nitajisikia huzuni, sipendwi, hanijali. hio ndio shauku yangu. kila mtu ana shauku tofauti tofauti. Na Upande wangu pia natakiwa kujua mwenzangu ana shauku ipi? Anapenda nini? ili tuweze kwenda sambamba.

Lakini nimekuja kugundua kitu kimoja kizuri , nafikiri tunaweza kukubaliana , kuwa unachotaka kufanyiwa , mfanyie mtu mwingine hivyo. Kila unapomfanyia mume wako au mke wako kitu unachokipenda, Naye atakufanyia hivyo. Ni rahisi tu. huku ndiko kujielezea kwa mwenza wako.

Kwa hio mtu yeyote ambaye anataka shauku yake ikutane na maisha yake , halafu akaendelea kusubiri kutoka upande mmoja , hataweza kufanikiwa .Badala yake utaanza kujisikia kuwa mbali na mwenza wako kwa sababu utaanza kuona hakupendi. hakujali. hakuthamini. Utajiona kuwa hukutakiwa kuwepo katika mahusiano hayo, mtu huyo hakufai, kumbe tatizo liko kwako pia. Ufahamu wako ndio unaokufikisha katika hali hio. unajikatisha tamaa mwenyewe. Na utaishia hapo kama utachelewa kuamka kutoka usingizini.

Kutazama kwa Jicho lingine.

Kurudi katika jicho lingine , Swali ni kwamba , ni nini kusudu kubwa la urafiki wa kimapenzi? kwa nini nafikiria nataka hiki— kwa nini nina uhakika ni hili? Hii inahitaji uchunguzi wa ndani katika kusudi la matarajio .

Utakapojibu maswali haya, Swali linalofuata ni Ni nani mtu huyu ambaye nina urafiki naye? Ana sababu iliyo sawa na yangu, na kama ndio hivyo, zinajieleza kwa urahisi katika utofauti wake? Inahitaji uelewa wa mwenza wako hapa. msukumo uliopo, hamu na matendo yaliopo. Huenda yasifanane na unayotaka.

Mwisho lipo swali la kwa nini na ni kwa jinsi gani mambo haya yatawasiliana. Kukutana na mahitaji, hamu, na kusudi , inaweza kuwa inatakiwa kuwepo na zoezi la kujenga hivyo vitu ndani kukamilisha mapenzi yenu, au kama hamtaweza kufanya hivyo mtaishi hivyo mkiwa na upweke japo mpo wawili, kujihisi kutengwa wakati mpo pamoja. na utaishi na huzuni. kujiona kutapeliwa kimapenzi, matatizo mengi.

Panahitajika mbinu zenye ujuzi wa kurekebisha, umuhimu wa uaminifu na tabia ya kuwa wazi kwa mwenza wako. Mfanyie mtu kitu ambacho unapenda kufanyiwa na yote yatakurudia.

Umeipenda makala hii? Shirikisha wengi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger