juu

Saturday 14 September 2019

SIFA 5 ZA MWANAMKE MWENYE MVUTO WA JUU



Kuwa na mvuto haihusiani na kutumia manicure, moisturizer, au kununua nguo za gharama na viatu vya gharama na pochi. Nimesema baadhi tu ya vitu ambavyo wanawake wanapenda kuvitumia.

Wakati kitu cha muhimu ni kile ambacho kinamfanya mtu awe na ujasiri anapokuwa anatembea mtaani, na awe anajisikia vizuri.

Lakini hapa kuna njia zingine za mvuto ambazo unaweza kuzitumia kwa ajili yako pamoja na mwenza wako;

1.Jenga Ujasiri

Ujasiri ni kitu kikubwa-Ni aina ya mng’aro wa ndani. Hii haina maana kwamba usihofie kitu. Ujasiri ni uwezo wa kutambua hofu yako. Kujenga ujasiri ambao utakuzunguka wewe na watu wanaokuamini. Weka kipaumbele katika kulea mambo mazuri kwa ajili yako , na kutumia muda kwa ajili ya kufanya kazi unazozipenda, hizo ndio zinakufanya ung’ae.

Unapokuwa Mgumu wa kueleweka , unatengeneza kitu kinachoonyesha kama unasema ; ‘’usinipende mimi’’

Tengeneza orodha ya nguvu zako. Huenda ni hisia zako za furaha, au namna ambavyo unaweza kucheza , au usikivu wako , vitu ambavyo unaona vinakupa furaha .kila mtu ndio ulimwengu wako utakuwa unajikubali kwa sababu yao, Na ndio njia pekee ya kuonyesha mvuto kwao..

2.Kuwa huru

Watu wengi huelezea jinsi ambavyo waliweza kukutana na wenza wao ; Macho yetu yalikutana wakati tulipokuwa kwenye kundi la watu wanaotoa historia za maisha yao, au alikuwa sehemu ya mgahawa, au tulipokuwa tunapishana kwenye ngazi, au tulikutana kwenye basi, au ndege. kwa hio mwenza wako alikuwa kwenye mambo yake. Walikuwa mbali na wewe.

Hizi ni baadhi ya sehemu ambazo unaweza kukutanisha macho na mtu , na ukavutiwa nae.

3.Take risk

Wanandoa wenye uzoefu wa kutosha wamekuwa wakipata utoshelevu mkubwa kwenye mahusiano yao. Na hii ina maana kwamba wako tayari kujitoa kwa ajili ya wenza wao. Sina maana kujimaliza maisha. Yani wako tayari kubeba matatizo ya wenza wao na kuyafanya ya kwao.

Nafikiri umewahi kusikia mwanaume anaamua kuiba kwa ajili ya kutaka mke wake awe na furaha. Hio ni risk .Wanaume wakipenda huwa hawaogopi risk.

Ujasiri ni uwezo wa kufahamu woga wako unatoka wapi, unatokana na nini.

Sex inaweza kuwa ni silaha pia.ni kitu ambacho kinaweza kuimarisha mahusiano na kuwepo hamu ya wema kushikana pamoja.

4Jifunze jinsi ya kuwa na raha katika mwili wako

Kujisikia vizuri mwilini mwako sio kuvaa nguo za gharama na kunukia kupita kiasi, au kuwa kama matangazo ya mji . Ni aina ya kuwa na furaha ya ndani , kuwa huru, kujisikia salama, kuwa na amani wakati ukiwa unatembea mtaani na jinsi unavyosogeza hips zako.

Kuanza kutaka kuwa mtu wa kuvutia , fanya mazoezi ya mwili, kula vizuri, tafakari , hapo utakuwa umebalance mvuto wako.

5.Acha kujikosoa

Unapojikosoa mwenyewe, umuhimu wako utakuwa unaonekana kwa wengine. Don’t like me. Hii ni kitu kibaya ambacho kinawafanya wanaume wageuzie shingo zao mbali.

Pia wakati mtu anakupongeza,pokea pongezi hio. Huwa ngumu kwa mtu ambaye hajiamini na haoni maana ya pongezi hio. Anaona kama anabezwa. Kwa hio wakati mtu anakuambia , you look beautful, Usiseme hivi, Inaonekana hujavaa miwani yako leo wewe..

Kubali pongezi hio– inawafanya watu wengine wanaokuambia hivyo kujisikia vizuri unapokubali na kupokea kitu walichokisema.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger