juu

Friday, 13 September 2019

MUME WANGU HUTAKA NGONO MARA 4 TU KWA MWAKA– NITAFANYAJE?



Anasema kwamba anaogopa urafiki wa kimapenzi. tiba zitamsaidia kurudisha hisia zake, au tuache hivyo na tuishi tu kama marafiki kawaida?

Katika miaka tulioishi nae , ni miaka 17 sasa, muda wote nimekuwa nikifikiria kuwa nina utofauti mkubwa na mume wangu kwa kuwa mimi nina uhitaji zaidi kuliko yeye.
Lakini miaka 10 iliopita ilikuwa ni mara chache kufanya sex kama kawaida, na kunifanya niamini kuwa ni kawaida kufanya mara nne tu kwa mwaka.

Mwishowe alianza kukabiliana na hili suala na… ni baada ya kuvunjika kitu fulani kazini kwake.. ametambua ana ugonjwa wa wasiwasi katika jamii. Na sasa ananiambia kuwa hakufahamu na wala alikuwa hana hisia asilimia 100 kuhusu maisha ya ngono na hakuweza kuzitambua hisia zake.

Alisema pia ana woga katika urafiki wa kimapenzi. mimi ni mjinga kiasi kwamba nitaweza kuamini kuwa alikuwa hawezi kupata hisia kwa muda wote huo kwa kupitia tiba, Ambazo ndio kwanza ameanza, au niachane na kuhangaika na kutaka kutimiza haja yangu ya sex maishani?

Ushauri ni kwamba
Usijaribu kumfikiria vibaya kwa kukiri kwake. hali yake ya chini ya kuhitaji sex inaweza kuwa imegundulika baada ya kuanza tiba au kwenye kushauriwa kisaikolojia. na kwa kupitia uchunguzi na matibabu yamemletea maendeleo .

Taratibu za matibabu zinaweza kumponya na kuboresha akili yake, afya ya mahusiano na kujamiiana. Msaidie kwenye matibabu haya kwa kadri awezavyo, kama inawezekana. Tafuta msaada wako mwenyewe, au ungana nae kwenye matibabu.

Ni maumivu sana kuhisi uhitaji na kupoteza matumaini, na unastahili kupata mahitaji yako.

Kwa muda huu uliopo . Fanyia kazi kurekebisha na kuweka sawa mambo ulionayo akilini mwako, tuliza akili yako , badilisha mawazo yako kuwa positive.
Itasaidia kuelewa tatizo alilonalo mumeo la wasiwasi sugu na jinsi ilivyomuathiri katika nia yake ya ngono na kuamsha hisia zake upya.

Usihofu katika tatizo hilo. litaisha na mtaendelea kuwa na mahusiano mazuri kila siku.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger