Yawezekana umekuwa na mpenzi kwa muda mrefu sana, lakini dalili ya ndoa huioni kabisa, kana kwamba mahusiano yenu yameanza jana. Ukiwa binti mjanja leo nakupa mbinu za kumuingiza mwanaume yeyote mtegoni kwako, na mwisho wa siku mnafunga ndoa takatifu kabisa.
1. Kuwa Girlfriend Kamili
Mfanye ajihisi kuwa anakubalika, yuko salama na special hakikisha unafanya kila kitu ambacho Mwanamke Kamili anaweza kufanya. Na bila shaka atakuona wewe umejitwika jukumu la kuhakikisha kuwa wewe uko hapo kwa ajili yake.
2. Mtunze
Hakikisha kuwa unamtunza na unamfanya akutegemee kwa mambo madogo madogo, hata kama ni jambo rahisi lile la kushughulikia nguo zake ama kumpa sapoti wakati anapohitaji. Wewe kuwa ubavuni mwake kutafanya mabadiliko ya haraka sana, na hatoweza kustahimili kuishi bila wewe.
3. Kuwa Shabiki wake Mkuu
Geuka shabiki mkuu wa mwanaume wako kwa chochote kile ambacho anachofanya, hata kama ni jambo la utani ama la kuchekesha wewe mpe sapoti kwa kumshabikia atimize azma yake. Atakuona kuwa wewe uko karibu nae.
4. Mtreat
Wakati mwingine Wanaume huchoka kwa kuwa wao ndio kila wakati huwatoa wanawake out na deti. Msaprize siku moja kwa kumtoa out, na hakikisha unafanya mambo ambayo anapenda kufanya.
5. Kuwa Mkweli kwa kile Unachotaka
Ongea naye na weka wazi kuwa unampenda, na ueleze vile ambavyo unaona Mahusiano yenu yatakuwa miaka inayokuja. Hata kama hana uhakika na Ndoa, atleast utakuwa umeliweka wazo hili katika kichwa chake.
6. Kuwa na Kitu cha Kufanya
Hakuna kitu kizuri zaidi kama Mwanamke ukawa na Uwezo wa Kujitegemea Mwenyewe. Mfanye akuone kuwa wewe una mambo yako ambayo unafanya. Hii itamfanya aone ipo siku unaweza enda zako, na hivyo atahakikisha ya kuwa jambo kama hilo halitokei.
7. Muonyeshe kuwa Wewe ni Wife Material
Kama unamtaka aweke Pete kwenye kidole chako, basi Muonyeshe kuwa wewe utakuwa Mke Mwema. Kuwa mtiifu, mwaminifu, mpole, mvumilivu, na mpendezi. Muda si mrefu ataona kuwa hakuna Mwanamke yeyote ambaye anaweza kuzishinda tabia ambazo uko nazo.
Kama unamtaka aweke Pete kwenye kidole chako, basi Muonyeshe kuwa wewe utakuwa Mke Mwema. Kuwa mtiifu, mwaminifu, mpole, mvumilivu, na mpendezi. Muda si mrefu ataona kuwa hakuna Mwanamke yeyote ambaye anaweza kuzishinda tabia ambazo uko nazo.
0 comments:
Post a Comment