juu

Saturday 7 September 2019

Sababu ya Wasichana wengi kutoolewa ni hizi

KWANINI MABINTI WENGI HAWAOLEWI..!
zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini mabinti wengi wanashindwa KUOLEWA..
👉VIGEZO VISIVYO NA MSINGI.
🔹Kuweka vigezo vingi na kuchagua chagua sana inaweza ikawa ni sababu ya kufanya mabinti wengi wasiolewe.
🔹Binti unakuta anataka mwanaume awe amesoma, mrefu, handsome, sijui awe na kazi nzur, awe na upendo wa kweli, na mambo mengi kama hayo.
🔹Wanaume wanaokidhi vigezo hivyo ni wachache sana na kimsingi inawezekana wasiwepo kabisa. Mwisho hujikuta umri unaenda bila ya kuolewa au kuangukia kwenye mikono ya Wanaume ambao ni matapeli wa mapenzi.
🔹kuna msemo usemao, “ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu” na mwingine ufananao na huo unaosema “mchagua nazi hupata koloma”.
👉NAMNA UNAVYOJIWEKA.
🔹Jinsi unavyojiweka ndivyo watu watakavyokuchukulia. Mavazi unayovaa, marafiki ulionao na hata tabia yako kwa ujumla.
🔹Mabinti wengi wanafeli sana kwenye eneo la mavazi, mavazi ya kuacha maungio ya ndani wazi yanawashushia heshima mabinti wengi sana bila wao kujua, wengi wanaona kama wanaenda na wakati lakini wanajidhalilisha.
🔹Hakuna mwanaume anayependa kuoa mwanamke asiyejiheshimu, kama yupo basi hatakuwa muaoji. Mwanaume gani anayependa kutembea na mkewe akiwa maziwa yapo wazi yananing’inia kama yanataka kuanguka? Sketi fupi mapaja yote yapo wazi na tena ina mpasua? Suruali imembana mpaka maumbile ya ndani, michirizi ya nguo ya ndani inaonekana.
🔹Sidhani kama kuna mwanaume anayependa mwanamke ambaye mwili wake ni maonyesho ya saba saba, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye hata nyumbani kwao hana ujasiri wa kumpeleka, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye starehe yake ya usiku na Mali yake ipo wazi kwa marafiki zake na watu kama Mali ya umma.
🔹Niwasaidie dada zangu,ukivaa mavazi ya ajabu ajabu utavutia Wanaume wa kulala na wewe na kukuacha na si waoaji, utakuwa ni kiburudisho cha usiku mmoja na si mwanamke wa maisha.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger