juu

Tuesday 31 December 2019

Hizi ndizo tabia za mke mwema

Wengi wangekuja na orodha isiyokuwa na mwisho ambayo inaeleza tofauti tofauti kuhusu tabia nzuri za mwanamke. Hapa tumekuja na orodha ya sifa nzuri na muhimu zaidi ambazo zinafaa kutumiwa kama kuwa kigezo cha kupima tabia nzuri za mwanamke.

Kwa kuwa wanawake huwa na tabia tofauti tofauti, hatuwezi kusema lazima mwanamke awe na tabia zote hizi ili asomeke kama mwanamke mwenye tabia nzuri. La. hizi ni baadhi tu ya tabia ambazo mwanamke anaweza kuwa nazo, na nyingine kutokuwa nazo na bado akaorodheshwa kuwa na tabia nzuri. Zama nami.

Baadhi ya sifa nzuri kutoka kwa mwanamke

Kusamehe
Ni vigumu kuwa katika uhusiano halafu uwe hauna moyo wa kumsamehe mpenzi wako. Kawaida katika mahusiano, huwa kuna changamoto kadhaa ambazo hujitokeza hivyo lazima uwe na tabia ya kuweza kusamehe. Hii inaweza kuanzia kukosana kwa mambo ya kinyumbani, ama mambo mengine yanayofanana.

Mwanamke mzuri ni yule ambaye ana uwezo wa kumsamehe mpenzi wake bila kuweka kinyongo. Iwapo mpenzi wako umemshika katika fumanizi nk na bado unampenda, basi jambo zuri la kufanya ni kumsamehe na kuendelea na maisha.

Msikilizaji mzuri
Mara nyingi migogoro ambayo inatokea majumbani kati ya wapenzi wawili husababishwa na kutosikilizana. Huyu akiambiwa hivi huyu anajibu hivi. Iwapo mwanamke anataka mahusiano yake yake marefu na ya kufaana, basi anapaswa kuwa msikilizaji mzuri.

Mwanamke ambaye huwa anatulia na kumsikiliza mpenzi wake, mahusiano yake na mpenzi wake huwa ya furaha zaidi ukilinganisha na ya yule ambaye hatilii maanani maoni ya mwenzake.

Mwaminifu
Hii ni kuanzia kuongea ukweli bila kudanganya hadi maswala ya chumbani. Iwapo mwanamke ana mchepuko mahali fulani ama anamwendea kinyume mpenzi wake, basi aina hii ya tabia haifai kabisa.

Sifa ya mwanamke mzuri ni ile ambayo ni ya uaminifu. Mwanamke mwaminifu kwa mpenzi wake haitofika wakati fulani ambapo atakosana na mpenziwe.

Msaidifu
Katika mahusiano, kuna wakati fulani hufika ambapo lazima wapenzi wawili wasaidiane kufanya jambo ama kutimiza kitu fulani. Hivyo mwanamke mzuri ni yule ambaye anatoa msaada wa kumsaidia mpenzi wake na jambo fulani. Mathalan inaweza kuwa kumsaidia kimawazo, kifedha ama jambo tofauti. Mwanamke mwenye tabia hii humpendeza sana mpenzi wake kwa kuwa inaonyesha ya kuwa mwanamke kama huyu ana uwezo wa kumtumikia mpenzi wake wakati ambapo anaweza kupatwa na majanga.

Mwenye imani
Kuna tabia za wanawake ambazo huwachosha wanaume, nazo ni kukosa imani. Iwapo wewe una tabia za kutokuwa na imani basi tabia kama hio unafaa kuiacha mara moja. Tabia za kutokuwa na imani ni kama vile kuharakisha jambo, kulazimisha kitu ambacho hakiwezekani nk.

Hali kadhalika, mwanamke mwenye imani ni yule ambayo ana subira. Iwapo ameambiwa na mpenzi wake kuhusu jambo fulani, basi yeye hutulia hadi kungojea matokeo yake.

Kuhamasisha
Wanaume humpenda mwanamke ambaye anatoa motisha ili kumsaidia kutimiza lengo lake. Vile vile kwa kawaida kuna wanaume ambao wanahitaji kiinua mgongo ili kutimiza mambo fulani. Hivyo wewe kama mwanamke, mara moja au nyingine unafaa kuonyesha umotisha wako kwa kumuelekeza mpenzi wako mara moja au nyingine.

Mcha Mungu
Mwanamke mcha Mungu bila shaka maisha yake huwa ya kufanikiwa. Mtu yeyote yule lazima awe mcha Mungu ili awe na sifa nzuri ya maisha katika jamii.

Heshima
Heshima haimaanishi ni kwa mpenzi wako pekee bali kwa jamii nzima. Mwanamke ambaye anapenda kugombana na majirani kila kukicha halafu ikifika jioni anamheshimu mpenzi wake hafai.

Tabia za mwanamke mzuri ni yule ambaye anaheshimu na kuishi na majirani zake vizuri bila kuwa na mivurutano yeyote ile.

Anajiamini
Mwanamke mzuri ni yule anajiamini na anaamini mahusiano yake. Mwanamke mzuri ni yule ambaye hatasikia maneno ya watu halafu akampakizia mpenzi wake. Iwapo kuna swala tata ambalo linafanyika, basi mwanamke aina hii atamwekea kikao mpenzi wake na kujaribu kumuuliza maswali na kutaka kufafanua chochote ambacho kitakuwa kinamkwaza. Mwanamke aina hii hupendwa na wanaume kwa sababu anajua ya kuwa akifanya jambo fulani basi mpenzi wake atataka kuelezewa bila kuwa na hisia zozote mbaya.

Anajua mapenzi
Ikija katika swala la mapenzi, mwanamke mzuri ni yule ambaye anaujua mwili wake vizuri, hivyo si mwoga wa kuonyesha sehemu yake ya ndani ya mapenzi. Mwanamke huyu haoni aibu ya kujaribu mitindo tofauti tofauti ya kufanya mapenzi nk.

Wanawake ambao wanajua mapenzi ni moja wapo wa sifa nzuri ambayo wanaume wanapenda.
Share:

Sunday 29 December 2019

Njia zitakazowasiaidia muweze kudumu katika mahusiano yenu ya kimapenzi

Hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na kama wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe kushiriki kwenye mapenzi hayo.

Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa, wote tunapenda kupenda na pia tunapenda kupendwa pia. Na siku zote ukipenda na usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi yanapokuwa machungu kwao.

Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli kuna mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na kupendwa pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa maelewano baina yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani au ukaelewa lakini ukakosa njia za kutatua.

Zifuatazo ni baadhi tu ya njia mbalimbali za kufanya ukae na mpenzi wako kwa muda mrefu kwenye mahusiano na mkafurahia mapenzi yenu popote pale mtakapokuwa na mtakapoishi.

1. Kuwa na muonekano chanya kwa mpenzi wako.
Ukiwa ni mtu wa kuangalia mabaya/kasoro sana kwa mpenzi wako kuliko mazuri yake hautakuja kukaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu hata siku moja, utaendelea kubadilisha wanaume/Wanawake kila siku na mwisho wa siku utajiona huna bahati kwenye mapenzi na wakati Unayeyaharibu mapenzi yako ni wewe Mwenyewe…kakuna asiye na kasoro (ukiwemo wewe mwenyewe).

Kwa hiyo muonyeshe mpenzi wako mapenzi bora na umrekebishe pale anapokosea Bila kuwa na lawama mara kwa mara, kuna makosa mengine ni hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na kama wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe kushiriki kwenye mapenzi hayo.

Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa, wote tunapenda kupenda na pia tunapenda kupendwa in return. Na siku zote ukipenda na usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi yanapokuwa machungu kwao.

Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli kuna mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na kupendwa pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa maelewano baina yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani au ukaelewa lakini ukakosa njia za kutatua.

2. Mpe nafasi na uhuru mpenzi wako.
Mnapokuwa kwenye mahusiano jitahidini kwa hali na mali kupeana nafasi/uhuru kwenye mambo mengi hasa yale ya kitaaluma zaidi na kimaisha. Anapokwambia yupo kwenye kikao cha kikazi jaribu kumuelewa na umpe support ya kutosha kwenye kazi zake au biashara zake au hata masomo yake. Usipende sana kulalamika pale anapochelewa kurudi kazini au kutoka kwenye biashara zake bali mpokee kwa upole na baada ya kupumzika ndipo muulize kwa upole na kimahaba zaidi kwanini siku hizi anachelewa sana kurudi au kwenye biashara zake au shuleni tofauti na zamani.

Hii itajenga zaidi kuliko kubomoa kwa kulalamika na kupayuka mbele yake na huku yeye akiwa hata hajapumzika na itamfanya siku nyingine aione nyumba chungu kitu ambacho si kizuri kwenu wote wawili.

3. Mfanye mwenza wako ajivunie kuwa nawe kila wakati.
Hakikisha katika mapenzi yenu kila siku unamfanya mpenzi wako ajivunie kuwa nawe na hakikisha humfanyi ajute kwa kukuchagua wewe miongoni mwa wote aliowaona. Usijidanganye hata siku moja kuwa kwa kumpata tu na kwa yeye kukupenda basi hajaona mwingine wa kuweza kuwa naye.

Wapo wengi sana anaoweza kuwa nao lakini amekuchagua wewe katika hao wote, kwa hiyo usimfanye aanze kuwafikiria wale wengine wanaomfuatilia kila siku na kumsumbua. Ukianza kumwacha aanze kuwafikiria wengine aidha kwa wewe kuwa unamkosesha amani ya mapenzi kila mara au kwa mengine mabaya ndani ya mapenzi basi ipo siku utaishia pabaya.

4. Msadie kwa hali na mali kila inapowezekana.
Kwenye mahusiano huwa kuna kupanda na kushuka miongoni mwa wapenzi na hasa kiuchumi na hata kisaikolojia. Hakuna kitu kizuri kwenye mapenzi kama mtu kupata tatizo na akasaidiwa na mpenzi wake katika hali ambayo hakuitegemea, namaanisha mpenzi wako akipata tatizo lolote hakikisha wewe ndo unakuwa wa kwanza kulifahamu na kulifanyia kazi.

Sio matatizo yote yanamalizwa kwa pesa so hata ushauri na kumpa mawazo chanya inasaidia sana na kumfanya awe na furaha kuwa nawe. Kama unampenda usione tabu kumsaidia kwa kuogopa kuonekana eti unahonga, huyo ni mpenzi wako kwa hiyo jiamini na umpe kile anachostahili kusaidiwa na mpenzi wake.

Yapo mambo mengi sana ambayo kama mkiyafanya kwenye mapenzi basi uhusiano wenu utakuwa wa kudumu na wenye furaha sana ingawa hapa nimezungumzia kwa uchache sana lakini nina imani itasaidia sana kwa wote walio kwenye mahusiano .

Mapenzi hayana ndumba au limbwata hata siku moja, unapoona wapenzi wengi wana furaha kwenye mapenzi yao ni kwa sababu wanavumiliana kwa mengi na kusameheana kwa mengi. sana na unaweza kuyarekebisha kwa kukaa chini na mpenzi wako mkayamaliza kwa dakika 5 tu lakini wengine huwa issue kubwa kwao na kusababisha mwisho mbaya.
Share:

Ijue heshima ya mwanamke kwenye mahusianon ya kimapenzi

Mwanamke ni kama Jua unaweza usione umuhimu wake, yaani kila siku unaenda mjini jua lipo tu, unaliangalia lakini huangalii umuhimu wake kwako. Wakati mwingine likiwa kali unaanza kulalamika kuwa linachoma na lina kera. Lakini ukitafakari kidogo tu utajua kuwa bila jua maisha yasingekuwepo.

Chakula tunachokula ni kwasababu ya Jua, mvua ikinyesha sana mafuriko yakitokea tunatamani jua, kwenye baridi tunatamani pia jua, Hatuliwazii kwasababu lipo tu na linatimiza majukumu yake kimya kimya bila kelele.

Hiyo ni sawa na mwanamke, ukishaoa kuna mambo ambayo mwanamke huyafanya na baada ya muda unaanza kuyaona ya kawaida kawaida, chakula kinakuwa mezani kila siku hujui kinapikwaje na vyombo vinaoshwaje, anabeba mimba na watoto wanazaliwa hujui maumivu aliyoyapata lakini unatabasmu na kucheka ukijisifia watoto wangu na hata mkigombana unasema niachie wanangu wewe nenda tu, utafikili unajua maumivu aloyapata kipindi anawaleta duniani hao watoto.

Watoto wanaumwa mpaka wanapona hujui hata wameponaje, wanalia usiku hujui hata nani alikuwa anawabembeleza, ukirudi unakuta nguo safi chumba kisafi hutoi hata shukurani kwakuwa ushasahau kua kuna mtu anasafisha siwe safi muda wote.

Na anafanya vitu vyote hivyo kama Jua bila kelele lakini wewe ukitoa elfu mbili ya sukari utamnyanyasia mpaka ndugu zake kuwa unawalisha wewe! Hembu siku aondoke akuachie hao watoto unaojisifia kila siku kuwa ni wakwako na kumuambia hajaja na kitu, uanze kuwapikia na kuwaandaa kwenda shule, ufue nguo zao na zako. Unaweza kuajiri mfanyakazi lakini hawezi kufanya hata nusu ya kile anachokufanyia mkeo, kwani yeye atafanya kama kazi lakini mkeo anafanya kwa mapenzi, hahitaji umlipe chochote zaidi ya kutimiza majukumu yako na kumheshimu kama mke katika maisha yenu.

Vuta picha umeamka mkeo hayupo, watoto wanataka kuogeshwa kunywa chai na kwenda shule, hapo unatakiwa kuwahi kazini na mchana watoto wale.

Mheshimu sana mkeo kuna mambo mengi ambayo anayafanya ukiambiwa uyafanye Wewe utachanganyikiwa na mkeo huyafanya kwa upendo. Mwanamke anachohitaji kwa mume ni upendo na heshima tu.

Mhudumie, mpe upendo, muheshimu na muonyeshe kuwa kwako ana umuhimu mkubwa, mfanye mkeo atabasamu kila mara na familia nzima
Share:

How to Attract an Older Man: 3 Crucial Steps to Win Them Over

Do you wan to attract older man? Are you looking ways to attract mature man? Women love dating old men. There is something which attract women towards them. Love brings to you some of the ways to attract older men towards them. 

It is a common notion that young women love mature men and mature men love to fall for the younger women. Why does it really happen? The sole reason can be that women are emotional beings and they want their partner to be someone who can tackle any situation. Want to know more on this? All you need to do is to keep scrolling and keep reading.




Why Women Fall For Older Man?

Women fall for older men because they want to feel secured in life. They want to have that feeling of care which a mature man can easily provide them. Many of these women believe that age makes men mature. Hence, Dating a matured men is a good idea.


Be Confident:Just as younger women love matured men. Matured men love confident young women. The women who are confident in their attitude gives positive energy to them. Make him believe that you are confident in your own skin and do not really require anyone.


Change In Looks:The physical attributes helps you attract older man. The looks plays an important role in making matured men fall for you. Hence, exterior beauty also works in this case.

Don’t Be Insecure:
The thing which you need to avoid is being insecure. The more you tend to highlight your insecurity the more it will work against you. So, if you want to make matured men fall for you, try to be secure in life.

Thus, one of the essential quality that every woman should have to attract older man is that they should not be materialistic in their approach. This may definitely make mature men fall you without any doubt.
Share:

Dalili za mwanamke muhuni katika mahusiano ya kimapenzi


Zifuatazo ndizo dalili za mwanamke muhuni kwenye mahusiano ya kimapenzi;

1. Siyo rahisi kupenda
Dalili ya kwanza ya mwanamke kicheche mi kwamba huwa huwa mara nyingi hawataki mambo ya mahusiano na mambo ya kupendana, wanataka siku zote wawe huru hata mtu yeyote mwenye uwezo zaidi ya aliyenaye akitokea, iwe rahisi kwake kujihusisha naye. Utasikia akisema tuwe Marafiki tuu.

2. Anachukulia mahusiano kama njia ya kujinufaisha
Wanawake vicheche huwa hawaingii katika mahusiano kwa sababu wamependa, siku zote wanakuwa na agenda ya siri nyuma yake, unaweza kuita faida, kiujumla kwa kitu chochote atakachokupa katika mahusiano, ujue hapo anatarajia faida yake, utakuta anakuchangamkia na kukufanyia vitu ambavyo hukutarajia, ila lengo lake mwisho wa siku utakuta anaishia kukuomba kitu Fulani kutoka kwako. Yupo tayari kufanya chochote hata kama kinamgarimu ilimradi apate kile anachokitaka.

3. Anategeka kirahisi kwa vitu vidogo na kwa mtu yoyote
Kwa kawaida mwanamke kicheche, pale tu utapomfurahisha na kumpa zawadi, au hela kila akuombapo unamsaidia, ni rahisi sana kukubali chochote utakacho mwambia afanye, haijalishi kuwa unamalengo gani nae ya baadae au la, ilimradi tu unampa anachotaka.

Na hii hutokea kwa kila mwanaume anayemkuta ambaye anaweza kumpa kile anachotaka basi atamfanyia chochote huyo mwanaume anachotaka.

4. Anamarafiki wakiume kwa manufaa
Mwanamke kicheche huwa na Marafiki wengi wa kiume kila mmoja kwa ajili ya faida. Mwanamke kuwa na marafiki wa kiume siyo tatizo, ila tatizo linakuja pale ukute mwanamke ana marafiki wa kiume ambao kila rafiki yake huyo anajukumu lake katika maisha yake, kifaida zaidi na siyo tu rafiki wa story za hapa na pale.

Unakuta Marafiki hao wote kila mtu anahudumia na wote unaambiwa ni marafiki tu, unaweza kusikia huyu wa kulipia saloon, mwingine wa vocha n.k, basi ujue huyo ni kicheche.

5. Ni rahisi kuvunja mahusiano usipompa anachotaka
Mwanamke kicheche anakasirika haraka usipompa kile anachokitaka. Wanawake kama hawa wamezoea kupata kitu chochote watakacho kutoka kwa mwanamme, na ukibahatika kupendwa na mtu kama huyu ujue si bure, ameona kuna kitu utakachoweza kumsaidia, wengine utakuta wanapohitaji kitu wanazunguka na story nyingi ila mwisho wa siku kama mtu muelewa utajua tu anataka nini, tena hata kubembelezwa hashindwi, ila usimpe sasa anachohitaji, unaweza usiongeleshwe wiki nzima hadi pale utapokamilisha hitaji lake.

Ukishindwa kabisa kumpa anachokitaka basi anavunja uhusiano na wewe na kutafuta mtu mwingine anayeweza kumpa anachokitaka.
Share:

Mambo sitini (60) ya kumwambia mpenzi wako katika mahusiano ya kimapenzi

Wakati kijana uko kwenye process ya kutafuta na kujaribu kuuteka moyo wa msichana, unatakiwa kujifunza kutumia maneno matamu. Na lazima ujue kuwa sio kila neno unalotumia litagusa moyo wa mwanamke unayemtaka, Lakini maneno matamu yanafanya kazi ya kushangaza.

Wakati vijana wengine wanalalamika kuwa ni vigumu kuuteka moyo wa msichana, jibu ni rahisi kwa sababu hawatumii maneno sahihi. Watu wengi pia huwa hawana maneno ya kusema na wengine hawajui kabisaaa hata jinsi ya kuanza.

Sasa hebu tujifunze haya maneno ya kumwambia msichana unayempenda na unahitaji awe wako milele;

1. Macho yako ni mazuri , yananifanya nipotelee kwako kila nikiyatizama.

2, Unanifanya niwe mwanaume bora , kwa hio nastahili mapenzi yako.

3. Tumbo langu hutetemeka unapoleta mikono yako usoni pangu.

4. Wewe ni mzuri na ni mrembo naogopa hata kukugusa naona kama nitakuchafua.

5. Unapotabasamu huzuni kwangu hupotea , ghafla nakuwa mtu wa furaha.

6. Ungeweza kupata mwanaume yeyote duniani , lakini umenichagua mimi.

7. Hapana.wewe sio mnene uko poa na ndivyo nipendavyo.

8. Ninapokushika nashisi kulegea kwenye magoti.

9. Wewe ni rafiki yangu, najifunza vitu vingi kwako,ndiye mtu ambae nimekuchagua, ndio mpenzi wa maisha yangu. ni wangu pekee, wewe ndio kila kitu kwangu.

10. Siamini , maana jinsi ulivyo amazing, lakini upo na mimi.

11. kila nikiangalia muda naona kama hautoshi kukupenda , natamani niwe na wewe milele. yaani wasife.

12. Umenifanya niamini kuwa zipo nafsi zinazoungana, zinazokutana pamoja.

13. Usiku nikiwa naangalia nyota na kuzilinganisha kila moja ili kuelewa ni kwa nini nakupenda,nilifanya vizuri hatimae nikazikimbia.

14. Kukutana nawe ni kitu ambacho hakijawahi kutokea.

15. Unapoonyesha kunipenda, huwa nazidiwa na hisia , hapo hupotea kabisaaa.

16. Kabla ya kulala ni lazima kwanza nikupigie simu ndio nitapata usingizi.

17. Naweza kuwa nawe maisha yote, lakini bado nahisi kama haitatosha kukupenda.

18. Napata furaha nikiwa na wewe.

19. Napenda kutumia muda na wewe.

20. Napenda ngozi yako laini, ninapoigusa.

21. Natamani maishsa yangu yote nikuone ukiwa na furaha.

22. Usibadilike nakupenda jinsi ulivyo.

23. Nikiwa na wewe nafurahi kama mtoto.

24. Napenda nywele zako.

25. Napenda nikukumbatie ninapokuaga.

26. Natamani kukubusu kila sehemu ya mwili wako.

27. Naanza siku na wewe ndani ya mawazo yangu, na ninamaliza siku na wewe kwenye ndoto zangu.

28. Ukiwa na mimi huwa natamani kusimamisha muda, maana muda unakwenda haraka.

29. Nikisikia sauti yako asubuhi , siku nzima nakuwa ni mtu wa furaha.

30. Tabasamu lako zuri linanifanya niyeyuke.

31. Unaponiaga napata shida kukuruhusu uende.

32. Umenielewa vizuri, ni kama unasoma mawazo yangu.

33. Mungu alikupendelea kukuumba, akili na kila ulichonacho.

34. Najivunia kuwa na wewe na ninafurahia.

35. Napenda unavyosema unanipenda.

36. Mapenzi yetu ni kama mawimbi ya bahari, wakati mwingi hutulia, na wakati mwingine huvuma,lakini yanarudi palepale.

37. Mapenzi yetu yawe kama ua rose ambalo halina miiba.

38. Najua kwa nini watu wanatutazama , ni kwa sababu wewe ni mzuri kuliko mwezi.

39. Muda utakuwa hauna thamani endapo sitatumia na wewe.

40. Kama siku yangu ingeanza na busu lako, nisingehitaji kahawa.

41. Kama ningeambiwa nielezee rangi, basi ningeenda kwenye rangi za rainbow, kwa sababu wewe ni mzuri.ni wa muujiza.

42. Mimi bila wewe ni mbaya, lakini ni mzuri nikiwa na wewe.

43. Tukishikana mikono na mioyo yetu inashikana,na nafsi zetu zinapatana .

44. Siku ya kwanza tulipokutana, nilijua ipo siku tutakutana tena, na nafurahi imetokea.

45. Nafurahi tumekua pamoja, sina cha kukosa hata kidogo.

46. Moyo wangu unapumua kama ndege, kila unapotabasamu.

47. Kila ninapokuwa nimeshuka moyo, nikikusikia wewe moyo wangu unapata nguvu.

48. Shika mikono yangu nami nitashika moyo wako, tunza kwa maisha yote.

49. Maisha yote , milele yote,isio na mwisho, toka nimekutana na wewe maneno yote yana maana.

50. Siku naona kama mwaka, na siku inapita kama sekunde.

51. Natamani ningekuwa kama pweza mwenye mikono mingi ili nikukumbatie na mikono myote.

52. Siamini katika nafsi mpya, lakini baada ya kukutana na wewe nimeamini, natamani kama ningeweza kurudi nyuma na kutengeneza kitu.

53. Sitaweza kukutoa kwenye mawazo yangu , kwa maana nakuhitaji uwepo.

54. Kuna wakati nahisi upweke, kwa wakati huo, basi huamua kukupigia simu na kusikia sauti yako.

55. Ninapokutizama namuona mungu jinsi alivyokuumba na kukubariki.

56. Unanifanya niwe wa muhimu .

57. Ni siri ambayo inanifanya nikutazame zaidi kwa kila siku.

58. Kuongea na wewe kila siku unanifanya nikufahamu zaidi na zaidi.

59. Moyo wangu nakupa,nipe moyo wako ili tuifungie kwa pamoja, na tutupe ufunguo mbali.

60. Nakuhitaji muda wote, siku , mwaka na hata milele.
Share:

Tabia za watu wenye usaliti katika mahusiano ya kimapenzi

Usaliti ni jambo baya sana katika mahusiano, usaliti si ujanja japo wengi wanaowaza kusaliti huwa wanajiona wajanja. Wanajiona wamefanikiwa pale ambapo wanasaliti na wenza wao kutogundua kama wanasalitiwa.

Siku zote anaesaliti huwa anajiona mjanja kwamba yeye anasaliti wakati mwenzake hasaliti. Kwa asilimia kubwa wanaume hujiona kama usaliti ni halali yao, wanataka wao wasaliti lakini wapenzi wao wasithubutu kusaliti.

kwanini hawataki wenzi wao wasaliti? Eti wanaumia, hakuna kitu kinacho mchukiza mwanaume kama kusalitiwa. Kusaliti asaliti yeye, akisaliti mwenzake ni kosa la jinai anaona amedhalilishwa.

Anajisikia fedheha kwamba mpenzi wake amemuonaje? Amemchukuliaje? Hajakamilika idara gani? Anawaza sana na kujiuliza jamii nzima inayojua kitendo hichoitamtazamaje?

Hapo ndio unakuta mwanaume anaamua kuchukua uamuzi mgumu ikiwemo hata kuhatarisha maisha ya mwenza wake.

Zifuatazo ni dalili za usaliti:

Kutopenda kuchimbwa.
Mara nyingi anaesaliti huwa hapendi kuchimbwa mambo kwa undani, anahofu anaweza kuchanganya madawa, hupenda mazungumzo mafupi na moja kwa moja.

Hapendi kuulizwa maswali mengi, ukimuuliza anayakwepa haraka na kutaka kukupeleka kwenye mazungumzo anayo yataka yeye.

Ukimuuliza kuhusu mipango yenu, ukimuuliza kuhusu mustakbali wa penzi lenu baadae hukuondoa kwenye mstari na kukufanya usiwe na hamu ya kumuuliza.

Hapendi ujue ratiba zake.
Mara nyingi mtu ambae ana lake jambo huwa hapendi ujue ratiba yake, anataka usimzoee, iwe anafanya maamuzi yake kulingana na yeye mwenyewe anavyojua, ikitokea unaijua ratiba yake atakuwa ni mtu wa kutoa udhuru kila wakati.

Leo atakuambia kuna mgonjwa anakwenda kumuona, kesho atakwambia kuna vikao na wafanyakazi wenzake, siku nyingine atakuambia gari imepata pancha analazimika kusubiri mafundi hadi wafike ndio aweze kuanza safari.

Simu yake ni kituo cha polisi.
Anaesaliti mara nyingi hapendi kuacha simu yake kiholela, simu inakaa mfukoni kwake hata kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo, mpo nyumbani mpo kwenye mazungumzo ya kifamilia yeye yake ipo mfukoni.

Imetolewa mlio hataki uione inaita maana inawezekana akatumiwa ujumbe, picha na mambo mengine ya kimapenzi.

Anaejiamini na yupo na yupo kwenye uhusiano imara hana sababu ya kuficha ficha simu yake anaiweka hadharani.

Mwingine atakusetia simu yake ukimpigia kila wakati inaonekana inatumika, kumbe yeye ndio anatumika wakati huo anakusaliti.

Anachat sana.
Wanaosaliti wengi wao hupenda kutumia meseji katika mawasiliano yao, yaani amewazoesha michepuko yake wote kusaliti hapendi kupokea sana simu, zaidi anapenda kuchati hivyo ni rahisi kuwasiliana na michepuko.

Mwisho hakutambulishi kwa watu wake wa karibu.
Share:

Thursday 26 December 2019

Mwanamke Akikujibu Hivi Achana nae Haraka Sana Ujue Hakuna Kitu Hapo....

Wanawake wa uswahilini wa siku hizi wamekuwa na swagger ya aina moja wanapotongozwa.utasikia "MIMI NAWAOGOPA WANAUME",ukiuliza wewe ni bikra kwani? Atajibu hapana,ukiuliza kwa nini unawaogopa wanaume wakati we sio bikra atakujibu" NISHATENDWA SANA".ndugu yangu nakushauri,kama ukijibiwa hivo basi ondoka fasta ujue hapo hakuna mwanamke kabisa,kwa sababu haiwezekani mtu atendwe yeye tu na kila mwanaume,ujue huyo ana mapungufu ambayo hata wewe hutaweza kuvumilia ,mapungufu ambayo hata wewe utamtenda tu na mwisho wa siku utamuongezea idadi ya wanaume waliomtenda.ila mara nyingi wanawake wanaojibu hivo au wanaotendwa hivo unakuta ni hawajatulia kabisa(vicheche).
Share:

Wednesday 25 December 2019

Kwenye mahusiano yapo ya kuvumilia, lakini siyo haya

Neno uvumilivu lisitumike vibaya kiasi cha kuharibu mfumo wako wa maisha.. Kuna mengine hayavumiliki zaidi ya mara moja.. Kuna tabia zenye kuumiza na kukera unapo vumilia unafuga ubovu.

Ukiona mtu mpenzi au rafiiki yako havumiliki kwa tabia zake usiogope kukaa nae mbali.. Huwezi vumillia kupigwa au kutukanwa hadharani. Huwezi vumilia mpenzi kukusaliti zaidi ya mara mbili zote anasema shetani alimpitia tu..alimpitia waende wapi?

Huwezi endelea kuvumilia mtu asiye kuheshimu wala kukusikiliza hata mambo ya msingi.

Kumbuka, Siku zote anaye penda na kujali sana katika mahusiano ndiye anayeishia kuumia. Wanasema mwenye upendo wa dhati hana bahati...unaweza mpenda sana mtu naye akajua ila yeye atapuuza hisia zako na kwenda kwa mwingine au kukusumbua makusudi akiamin kuwa huwezi muacha.

Anapo taka kuachana nawe kamwe usimlazimishe kamwe abaki kwako. Kuna wakati bado una mhitaj ila yeye ameamua kuachana nawe huenda ameona amempata bora zaidi yako au amechoshwa na tabia zako. Nikwambie kitu muache aende huwezi zuia mafuriko japo ni kweli inauma kuachwa na unaye mpenda lakini yapokee maumivu leo ili kesho uishi kwa furaha na amani pasipo yeye. Ukilazimisha abaki kwako wakati yeye anataka kuondoka kesho atakuumiza zaidi na kusema wewe ndo umemlazimisha kubaki.

Kama ulishamuwekea malengo ngumu sana kumtoa akilini mwako ila utalazimika ufanye hivyo kwa faida yako... Amin kuwa yeye sio mwanaume au mwanamke pekee duniani.. Kuna sehemu yupo kwa ajili yako ndiye atae kuwa furaha na faraja yako.

Uzuri wake au pesa zake zisikufanye umlilie anapo taka kukuacha. Hapo ulipo bado unayo nafasi kumpata atakaye ogopa kukupoteza. Huyo hukuwa katika malengo yake ila yupo atakae timiza ndoto zako kuitwa baba au mume ama mke.

Hakuzaliwa kwa ajili yako..yupo wako huenda naye analia na kuumizwa  kama wewe..mda utafika mtakutana na kuanzisha safair kisha kuishi pamoja.

Usiogope kupendwa kisa umetendwa/ uliachwa au kutendwa vibaya.

Unapo yasusa mapenzi kwa sababu yake yeye kukuumiza kumbuka  yeye ana wapenzi kwa nini ujitese kisa yeye?

Kuachana naye sio mwisho wa maisha bado utabaki yule yule

Kwa nini uendelee kulia ikiwa yeye kule aliko ana furaha??. Akikuona una lia na kukonda unampa jeuri ya kusema yeye ndo alikuwa nyota yako na anajipa kiburi kwa kusema huwezi kumpta zaidi yake yeye, unajua nini my dear?

Ni kweli huwezi kumpta kama yeye maana yeye si bora zadi ya wote 
 hvyo muache aende na atakapokuona ukiwa na  furaha na kupendeza atajidharau na kujiona boya tu hvyo jambo la hekima inuka uendelee na safari yako.
Share:

Mpenzi wako akiwa ana tabia hizi muache aande

Ebu litambue hili vyema ni  muhimu sana kuelekezea nguvu  zako, muda wako na upendo wako kwa anayekupenda.. Hapa nina maana kwamba mpende anayekupenda asiyependa achana naye.

Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio mungu wa kukufanya atakavyo.

Ndiyo asiyekupenda huwezi ukaona anapoteza muda na wewe kwenye mambo ya msingi ya kimaisha ila utaona tu hisia zikimzid  huko ndio anapiga simu nyingi nyingi na kujidai mtulivu na mwenye mapenzi siku hiyo hadi washangaa

Unajua nini my dear? Nikwambie hivi.
Muache aende .. Unalala, haupati usingizi juu ya mtu ambae huenda amelala na mtu mwingine muda huu kwa amani tele...muache aende!

Unaangalia simu yako sasa hivi ukisubiri text ya mtu ambae unamuona yuko online anachati na mtu mwingine kwa furaha zote...muache aende!

Unaweka status za huzuni watsapp kuonesha namna gani unavyoumizwa, wakati yeye yuko busy anamfikiria mtu mwingine, anampa furaha mtu mwingine, anamuweka status kuwa anampenda sana na wewe amekuficha usiweze kuiona status.

Muache aende..! Kweli unalia juu ya mtu ambae anamfurahisha mwingine?? Sio sawa kabisa, hebu sikiliza, kama wewe siye ambaye anakujali, basi hutakiwi kuwa na wasiwasi tena, wewe siye wake. Yuko mtu mwingine badala yako.

Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi nyani kwamba asali ni tamu kuliko ndizi...muache aende!

Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...muache aende!

Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu..muache aende!
Cha kujifunza ni hiki
Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!

Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano. Kwani aliyesema mahusiano lengo lake kukondeshana na kutoana machozi kama mtu unapika ugali wa vitungu ni nani? Ebu muache aende

Nikutie_moyo: usivunjike moyo, inuka na endelea.. "pause and remember nothing lasts forever. Better days are coming, but they will come faster with faith"
Share:

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger