juu

Thursday 12 December 2019

SIO LAZIMA UWE NA MPENZI, UNAWEZA ISHI BILA YEYE



Watu wengi wanadhani kwamba ili uwe na furaha ni lazima uwe na mpenzi, uwe na mwanaume au mwanamke wa kuishi naye. Watu wengi hudhani kuwa labda maisha hayajakamilika kwakua hawana wenza.

Hii huwalazimisha kutumia muda mwingi wakitafuta wapenzi kuliko kutafuta furaha. Lakini maisha hayako hivyo, huhitaji mtu wa kukupa furaha bali unahitaji mtu wa kufurahia naye.

Hapa naomba mnielewe, usitegemee kama huna furaha sasa utapata mwanaume au mwannamke wa kukupa furaha! Hapana unatakiwa kuwa na furaha kwanza ndiyo utafute mtu wa kufurahia naye.

Hapa nikimaanisha kuwa fanya mambo yote yanayokupa furaha sasa na si kusubiri mtu aje akufanyie hayo mambo. Unapenda kutoka kufurahi nnje ya nyumbani, unapenda muziki, unapenda starehe flani fanya.

Usisubiri mpaka ukiolewa au ukioa ndipo mwanaume au mwanamke akufanyie, kwanza hatakufnayia na pili hata akikufanyia hutajua namna ya kuifurahia. Hii iko sana hasa kwa wanawake kudhani kuwa ili upate mume unapaswa kuwa na huzuni.

Unapaswa kuwa mnyenyekevu, unapaswa kuacha kufanya starehe na mwanaume akuone kama mtu aliyetulia. Mapenzi hayako hivyo, watu hupenda watu wenye furaha.

Hii ndiyo maana yule rafiki yako aliyekua akishinda club mkasema kua holewi sasa ameolewa na anawatoto na familia nzuri wakati wewe bado unadanga na waume za watu.
Hapa sisemi uwe mtu wa starehe, hapana ninachosema nikuwa fanya vitu vinavyokupa furaha sasa na utawavuita watu wenye furaha. Usijizuie na kusema mimi nikioa au nikiolewa ndiyo nitafanya kitu flani.

Hutakua na muda huo wa kufanya na kutokana na kuwaza ndoa huko unaweza ukajikuta unaingia kwenye ndoa na mtu ambaye hata humpendi kwakua huna maisha zaidi ya kusubiri ndoa tu.

Kwamba kwakua unataka tu kuolewa au kuoa kwakua unaamini kua ndoa ndiyo itakuletea furaha basi unaweza kujikuta unaingia kwenye ndoa na mtu ambaye kumbe naye kashachoka maisha anakuja kupumzikia kwako.

Unaingia ukitegemea furaha, unaingia kwa kuigiza na mwisho unakuta kila kitu ni kichungu. Chagua furaha, fanya mambo yanayokufurahisha sasa, jua furaha na jiweke katika mazingira ya kukutana na watu wenye furaha na si wenye msongo wa mawazo!
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger