juu

Friday 13 December 2019

Epuka majuto katika Mahusiano.



Mpenzi msomaji wa makala hii kwanza kabisa nataka nikukumbushe kuwa katika mahusiano hamna kitu kibaya kama dharau.

Usije ukaja puuzia na kumdharau mtu anaye kupenda,mara nyingi kwa kukosa msimamo umejikuta umemkubalia mtu kuwa mpenzi wako au unamtongoza mtu then baadae unakuja ona hana jipya,wakati umeshampotezea muda wake,yamkini na umri ushaenda unakuja kumwacha kwasababu za ajabu zisizoeleweka,yamkini umepata mwingine unaanza kumdharau mpenzi wako.

Kosa dogo akifanya unashikilia na kumdharau,hii siyo nzuri ipo siku utaanza kukumbuka umuhimu wake na wakati huo utakuwa ushampoteza,utakumbuka mambo mengi lakini kwasababu utakuwa umeshamshusha thamani itakuwa ndoto kwako kurudisha ile heshima na uaminifu aliokupa mwanzo.

Tunza heshima ya Mke au mpenzi wako hii itakufanya ufurahie mahusiano yako na kuwa na furaha kila siku.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger