Nimeamua kuzungumzia ishu ya vyakula baada ya kuwasikia baadhi ya shoga zetu wakiwalalamikia waume zao kwamba hawawakati kiu wakati wa chakula cha usiku.
Nilipomwuliza mmoja wa wenzetu hao chakula anachopendelea kumpa mumewe, akaniambia ubwabwa, tambi, chipsi mayai na mishkaki.
Baada ya shoga yetu huyo kuniambia hivyo, nilimwuliza kama mista wake ni mtu wa kilaji, akasema nisiulize virungu polisi, nikaishia kucheka.
Kwa kuwa naelewa vyakula hivyo siyo vizuri hasa kwa wanaume, nilimshauri aache kumwandalia misosi hiyo badala yake awe anampikia ugali wa dona kwa samaki, mbogamboga za kila aina hususan nyanya chungu, tangawizi, kutumia asali, maziwa nk.
Sikuishia hapo, nilimshauri karanga mbichi, mihogo mibichi pamoja na nazi zisikatike ndani kwake atauona muziki wa mumewe utakavyobadilika.
Wakati shoga huyo akinisikiliza kwa makini, nilimwuliza kama mumewe huwa anafanya mazoezi ya viungo, akaniambia tangu alipomuoa hajawahi kumuona achilia mbali kumsikia akizungumzia suala la mazoezi.
Moja kwa moja nikabaini shoga zetu wanaolalamika kwamba hawainjoi mlo wa usiku, waume zao hawazingatii kupata mlo nilioutaja pamoja na kufanya mazoezi.
Kwa kuwa ndoa inaimarishwa na kitendo cha baba kumpa mkewe chakula cha usiku cha kutosha, basi jenga utamaduni wa kumwandalia chakula bora nilichokushauri pamoja na mazoezi mambo yatakuwa mazuri.
0 comments:
Post a Comment