juu

Saturday 7 September 2019

Mambo 8 Mwanamke Huangalia Kabla Kukupenda – Mtizamo Kutoka Kwa Wanawake

#1. Kuwa na msimamo
Jambo ambalo wanawake wanachukizwa kutoka kwa wanaume ni kuona mwanaume ambaye hana msimamo thabiti. Mara leo anasema hivi mara siku nyingine yuko hivi. Well, hapa siongei kuhusu mwanaume ambaye mambo yake hayajulikani (mysterious) La. Naongea kuhusu wale wanaume ambao hawawezi kuwa na misimamo yao wenyewe. Akili zao haziwezi kujitegemea, hawezi kusema jambo mpaka aulize ushauri kwa wenzake ama kwa marafiki zake. So kama wewe ni mwanaume ambaye una tabia kama hizi ziache kuanzia sasa. Nataka ujeuke. Ukiwa na tabia kama hii hutatoboa katika kutongoza mwanamke.
#2. Mwanaume mwenye kuvutia
Mwanaume ambaye anajua kuvutia wanawake ni silaha nzito katika sanaa ya kutongoza. Wanawake wanapenda mwanaume yeyote ambaye ana chembechembe za kusisimua wanawake. Na mwanaume kama huyu ni yule ambaye ana uwezo wa kutumia miondoko ya mwili ipasavyo, wale ambao wanajua kutumia sanaa ya kubanta, na wale wanaojua kuzungumza maneno ya kunata. Upo?
#3. Kuwa na sanaa ya ucheshi
Mwanamke anaweza kujua iwapo mwanaume anachembechembe za ucheshi au la wakati ambapo anaongea naye. Ni hivyo tu ambavyo unahitajika kuwa navyo wakati kama unataka kumfurahisha mwanamke. Kila wanawake wanajua kwamba mwanaume ambaye ni mcheshi huwa anavutia sana haswa ikija katika maswala ya kudeti na wakati wanapochat nao kupitia kwa simu. Hivyo jambo lako la kufanya ni hakikisha ya kuwa wakati unapoongea na mwanamke unamchekesha. Usijilazimishe kama wewe si mcheshi.
#4. Mwanaume ambaye halazimishi mambo
Mwanaume ambaye hulazimisha mambo huwa ni wanaume wanaochukiza zaidi ikija katika mchezo wa kudeti. Mwanaume wa kulazimisha ni yule ambaye anakubali kushindwa ili kuzuia mgogoro na mtu ambaye amemshinda kihadhi. Wewe kama mwanaume haupaswi kujidhalilisha mbele ya yeyote yule, hata kama ni marafiki zako. Kuwa na misimamo yako mwenyewe katika maisha yako. Kama unaona kuwa unakosewa una haki ya kupaza sauti yako usikike  balada ya kukasirika ama kusinyaa.
#5. Mwanaume ambaye anaheshimiwa na wengine
Wanawake wanapenda wanaume ambao wanawaheshimu, lakini pia wanapenda kuwa na wanaume ambao wanaheshimiwa na wengine. Kama kuna mtu hakuheshima, hayo ni makosa yako? Kama ni yako basi hakikisha kuwa unatatua. Lakini kama si makosa yako basi si lazima ujihusishe nao. Simama wima na utetee haki yako ya kuheshimiwa na kila mtu. Tumeelewana?
#6. Mwanaume anayejiamini
Kuwa na confidence ni muhimu kwa kila mwanaume. Ni nguvu ya kuzimu ambayo kila mtu utakayekutana naye atakuonea gere. Mwanaume anayejiamini huwavutia wanawake kwa kuwa anajiamini yeye mwenyewe pamoja na uwezo wake wa kuyaona mambo jinsi yalivyo ulimwenguni.
#7. Mwanaume anayeonekana vizuri
Huku ni kuanzia kule kujiweka kimwili. Vile ambavyo unasimama kama mwanaume. Je mapozi yako yakoje? Je unavalia nguo kulingana na mwili wako? Wakati unapoongea unazungumza na ishara zipi? Haya yote ni baadhi ya mambo ambayo  ni muhimu na yanayowafanya wanawake wakutambue kama wewe ni mwanaume bora wa kumchumbia au la.
#8. Mfanye ajihisi huru
Wanawake wanapenda wanaume ambao wanawafanya wajihisi huru wakiwa nao. Hii ni kulingana na usemi kutoka kwa wanawake. Hivyo kama wewe unakuwa na tabia za maswali yasioisha, ukali, woga ama kutojiamini basi utamfanya mwanamke ashindwe kujiskia comfortable akiwa na wewe. Jambo la kuhakikisha ni kuwa unautoa wasiwasi wowote ambao unaweza kujitokeza wakati unapoongea na yeye.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger