Sio siri, hali ya kuwa Single inaboa na ukizingatia umri wa kuwa na Mchumba umeshafika, na sasa unaenda ukubwani kabisa. Hebu Rahisisha Maisha kwa KUPOTEZEA haya yafuatayo:
1. Namtaka Mwanadini Mwenzangu
Kama una Mpenzi ambaye ni dini nyingine lakini ana sifa zote za kuwa Mume au Mke, kwa nini ujihisi kwamba hujapata bado mtu wa kufunga naye ndoa. Dini ni muhimu lakini hizi dini tumeletewa, je ingekuwa zamani zile msingeweza kuoana. Kwa hiyo angalia usijifunge sana hadi unakuwa mzee, na wakati Mapenzi ni watu wawili kupendana.
2. Namtaka Msomi Mwenzangu
Hili jambo limekuwa likisumbua sana Vijana Wasomi, wakidhani kwamba watu wanaolingana kielimu wakioana basi wataendana vizuri. Ndoa au mapenzi wala hayako hivyo, elimu ya darasani ni ya huko huko, na Elimu ya ndoa au mapenzi ni nyingine kabisa ambayo ni ya asili na Mungu ndiye Mwalimu wake.
3. Namtaka mwenye Pesa au Kazi nzuri
Ni kweli pesa ndio kila kitu, lakini kwenye mapenzi sio hivyo. Kwa nini wewe usipange kuwa na pesa zako kwanza halafu ndio umjaji mwenzako. Na kama pesa ikiisha au akafukuzwa kazi, au akafa mapema na akakuacha, utafanyaje hapo? Mabinti wengi sana wapo kwenye hii changamoto.
4. Namtaka Kisura au mwenye Shepu hii
Hii ipo sana kwa Vijana wa kiume, ni jambo zuri kumpata mtu mwenye mvuto lakini kwenye Ndoa au Mapenzi ni Zaidi ya hapo. Unaweza tumia nguvu kumpata mwenye mvuto au sura nzuri, lakini baadaye ukaja gundua kwamba ana vitabia fulani ambavyo sio vizuri kabisa. Je, si vema ukamchukua mtu wa kawaida lakini mkaishi kwa amani miaka yote?
5. Watu wa Makabila fulani hawafai
Hii kasumba imekuwa ikiwachanganya baadhi ya watu, wakiamini kwamba kuna Makabila ambayo hayafai kuoa au kuolewa nayo. Kwa nchi kama Tanzania ukishikilia Ukabila basi wewe una lako jambo, na bado kwenye mapenzi uko nyuma sana.
Zingatio
Huu ni Ushauri tu, na pia haya ni Mawazo yangu tu. Wewe kama wewe bado unayo nafasi ya kufikiria na kuchanganua Zaidi.
0 comments:
Post a Comment