juu

Wednesday, 12 June 2019

YAJUE MAMBO MANNE YA KUFANYA BAADA YA KUMALIZA KUFANYA TENDO LA NDOA!




Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia siha njema na pia kwa kunipa mwangaza wa kuandika hiki ninachokusudia. Pia niwashukuru wapenzi wasomaji wa safu hii ambao tumekuwa tukiwasiliana na kushauriana hili na lile katika tasnia hii adhimu ya mapenzi. Nawakaribisha sana!

Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kuizungumzia.

Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa. Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.

Nalazimika kuandika makala haya baada ya kubaini kuwa wengi wamekuwa wakifanya makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo hilo takatifu, kila mmoja anageukie kwake kisha kuuchapa usingizi.
Sisemi kwamba ni lazima kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na manufaa yake na mara nyingi yanaboresha

uhusiano.

Kuoga pamoja
Mtakuwa ni watu wa ajabu kama mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na majasho yake. Wapo wasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu. Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza lazima muoge.

Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia kuwaandalia maji wenza wao, wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza wako? Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa maisha?
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha ogeshaneni kimahaba.
Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji pandeni kitandani mkiwa wapesi.

Kusifiana
Hakuna muda maalum uliotengwa kwa ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni lazima utakuwa na jambo zuri la kumuambia mwenza wako.
Msifie kwa utundu na ubunifu wake. Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na ikibidi mpe sifa ya uzuri wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu yake ujisikie amani ya kupitiliza.

Wapo ambao hawana kabisa kasumba ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani wao wanachukulia kila kitu poa tu bila kujali kwamba kusifiana kunanogesha mambo.

Kuelekezana
Kwenye kale kamchezo, wapo ambao wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la kawaida. Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha wakati mkiendelea na burudani yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha ya kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na kubadilika.

Zungumzieni maisha
Huu ni wakati muafaka wa kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake. Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu kwa ujumla.

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa. Yapo mnayotakiwa kuyaepuka ili kutotibua furaha iliyopatikana. Hayo nitakuja kuyaeleza katika makala zinazokuja kupitia ukurasa huu. Niwatakie siku njema na tukutane wiki ijayo!
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger