Saturday, 31 August 2019
USHAURI: NIMESHIKA SIMU YA MPENZI WANGU, SINA HAMU
Mimi ni kijana umri miaka 26 mchumba wangu anafanya kazi katika kampuni moja hivi ya binafsi ,japo hatujaoana lakin tuna kawaida ya kutembeleana mara kwa mara,yeye anaishi Kinondoni Mkwajuni mimi naishi Ubungo Riverside,
Weekend hii nilienda kumtembelea akanipa simu yake nimwekee vocha nikiwa naweka vocha nikashangaa sms inaingia "honey uko wapi". Sikumwambia chochote na wala sikuifingua iyo sms ila niliweza kuisoma coz simu yake ni smartphone aina ya Sony yaan sms ikitumwa uwa inapita kwa juu unaweza kuisoma yote.
Niliamua kufungua whatsApp yake nikaanza kupitia baadhi ya chatting zake cha ajabu nikakutana na chatting moja amechat na mwanaume nilijua ni mwanaume coz niliangalia profile picture yake na sms zao zilinitsha sana jamaa kuna sms anasema " Juzi nilifurah mno nilipokuingizia nyuma" halafu mchumba wangu alisms akajibu". Mwenzio sijazoea nyuma". Kuna sms nyingine jamaa alituma akisema " Mwezi wa 6 inabd nikutie mimba".Daah niliishiwa pozi lakini sikusema kitu chochote hadi leo bado niko kimya nafikiria cha Kufanya......
Naombeni ushauri wenu
JIHADHARI NA MAADUI WA PENZI LAKO
NI Ijumaa nyingine murua. Siyo mbaya kwa wanajamvi hili, ndugu, jamaa na marafiki kushirikiana katika mapenzi kama vile wakati wa sherehe au msiba.
Pia siyo mbaya kujuliana hali na kutambulishana mambo ya msingi yanayoendelea kwenye uhusiano wako na mpenzi wako.
Hata hivyo, kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa sumu ya uhusiano wako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya kimapenzi. Kuna mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa au wazazi kuwa kuvuruga penzi lako.
Kwanza kabisa ni kujitahidi kudhibiti taarifa zenu kwenda kwa wengine; kadiri unavyoelezea uhusiano wako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako.
Katika eneo hili, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu masuala yako ya uhusiano kabla hujaanza kutafuta maoni na ushauri kwa wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na mada mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya uhusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.
Pili ni lazima uwe na uwezo wa kufanya mambo yako kipekee; Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika uhusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.
Tatu ni lazima ujue mwenye uamuzi ni wewe; ni kweli kwamba kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndiye mwenye kubeba lawama ya uamuzi utakaochukua.
Nne ni lazima uwe na subira; Usichukue uamuzi wa haraka katika uhusiano hususan uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka, unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha, hususan madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza kuzitumia kupata suluhu ya tatizo.
Tano ni kufungua njia za mawasiliano kati yenu; Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu uhusiano wenu kwa watu wengine ni kwa kuwa umekosa nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha wengine.
Sita ni vyema kuwa peke yenu; Hata kama hutaki kueleza watu kuhusu mambo yanayoendana na maisha yenu, mazingira unayoishi yanaweza kuchangia watu kutaka kuingilia uhusiano wenu kwa kutoa maelekezo, ushauri au maoni kuhusu muishivyo wewe na mpenzi wako. Inapobidi hakikisha hamuishi karibu na wazazi wenu, ndugu au rafiki wa karibu.
Au hufanyi kazi na mwenzi wako sehemu moja, kwani hiyo itakuwa njia rahisi sana ya watu kuona mnavyoishi. Inapobidi kuwa karibu na watu wengine, hakikisha mnakubaliana wewe na mwenza wako namna bora ya kuendesha mawasiliano kati yenu mbele za watu, ili msiwape nafasi ya wao kuanza kutoa maelekezo ya vile wanavyoona mnapaswa kuishi.
MAMBO YA KUFANYA MPENZI WAKO AKIKUFANYIA KISIRANI
KWA watu waliopo katika uhusiano wa kudumu, watakubaliana na mimi kwamba kuna wakati huwa inatokea mwenzi wako anaamua tu kukufanyia kisirani, na hii inawahusu zaidi wanawake, hataki kuzungumza chochote na wewe. Kila unachomuuliza anakujibu kwa mkato kisha anaendelea na mambo yake, hataki kushirikiana chochote na wewe na hata haki yako ya msingi huipati!
Wengine huweza kudumu kwenye hali hii kwa muda mrefu na kama usipokuwa makini, hii inaweza kuwa sababu itakayowaingiza kwenye matatizo makubwa zaidi. Bahati mbaya ni kwamba ni wanaume wachache sana wanaoelewa nini cha kufanya inapotokea mwanamke unayeishi naye, au unayempenda sana anakubadilikia kiasi hiki.
Yaani unamuona kabisa hayupo sawa, hakuchangamkii, hataki kuzungumza na wewe lakini unapomuuliza kama ana tatizo lolote, anakujibu kwamba hakuna tatizo lolote na yupo sawa. Wengine hudhani kwamba mwanamke husika ameanza dharau, amepata wanaume wanaompa jeuri au hampendi tena!
Kama nilivyosema, ukishindwa kujua hali yake imesababishwa na nini na unatakiwa kufanya nini ili kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida, unaweza kujikuta ukisababisha matatizo makubwa zaidi. Kwa hiyo, jambo la msingi unatakiwa kuwa
mwepesi kumsoma mwenzi wako na hii itakusaidia kumgundua muda ambao hayupo sawa.
Ukishagundua kama hayupo sawa na anakuwekea mgomo baridi, muulize kwa upole kama yupo sawa au kama kuna kitu kinamsumbua. Bila shaka majibu yake yatakuwa ni yaleyale, ‘nipo sawa’, ‘hakuna tatizo’ na mengine ya aina hiyo. Ukishamuuliza mara moja au mbili akakujibu vilevile, huna haja ya kuendelea kumuuliza mara nyingi zaidi kwani utasababisha azidi kukasirika.
Kwa jinsi tulivyoumbwa, wanawake wanaongozwa zaidi na hisia. Unapomuudhi mwanamke wako jambo fulani, kitu pekee anachoweza kukifanya kukuonesha kwamba amekasirika, ni kukulalamikia lakini akiona huelewi au kama humpi nafasi ya kulalamika, basi huishia kukununia. Kwa hiyo unapoona amefika katika hali kama hiyo, tambua kwamba kuna ujumbe anataka kukufikishia!
Anataka kukuonesha kwamba umemkasirisha, umemuumiza moyo wake na hafurahishwi na matendo yako. Unachotakiwa kufanya kwanza ni kutulia lakini pili ni kuanza kujichunguza mwenyewe, ni jambo gani umefanya mpaka ukamuudhi? Jiulize mwenyewe ndani ya kichwa chako lakini wakati huohuo, tambua kwamba anahitaji sana ‘attention’ yako.
Mwanamke akinuna, anataka umuoneshe kwamba umeshaelewa kwamba hayupo sawa na unajitahidi kumfanya arudi kuwa sawa! Wengine wanakosea kwamba akishaona amenuniwa, basi na yeye anaanza visa, anaanza kufokafoka na kuwa mkali, hayo ni makosa.
Unatakiwa kushuka chini hata kama bado hujajua kosa lako ni lipi, kuwa mpole kwake, muoneshe kumjali, jitahidi kujiweka karibu naye na mfanyie mambo mazuri. Kama unajiweza, unaweza hata kumuomba mtoke ‘out’, kama amekasirika sana anaweza hata kukataa kutoka na wewe lakini ni jukumu lako kumbembeleza.
Kihulka wanawake wameumbwa kubembelezwa kwa hiyo katika mazingira kama hayo ni nafasi yako ya kuonesha uwezo wako wa kumbembeleza mpaka akubaliane na kile unachokitaka. Ukishapata nafasi ya kutoka naye, au hata kama hamjatoka mpo wenyewe mahali tulivu, anza kuzungumza naye kwa upole ukitanguliza maneno matamu ya kujishusha na kumuomba akusamehe, bila shaka kama kuna jambo umemuudhi atakueleza kwa uwazi, hata kama unaona siyo jambo la msingi sana, rudia kumuomba radhi na mhakikishie kwamba halitajirudia.
Utashangaa anaanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida na lile tabasamu lililopotea kwenye uso wake litaanza kuchanua upya. Ukitumia nguvu na ubabe, utakuwa sawa na mtu anayemwagia petroli kwenye moto. Kwa leo ni hayo tu, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.
Mmeachana, Umeachwa ila moyoni bado unahisi unampenda, fanya haya umrudishe na kutengeneza nafasi ya kuwa naye tena.
Hivi karibuni msichana wako ameamua kuachana na wewe au labada wewe ndie uliyeamua kumuacha naye ila baada ya maamuzi hayo kupita na kufanyika, moyoni unahisi upendo wako juu yake bado umeutawala moyo wako na bado anaumiliki tena kwa sehemu kubwa sana na hauko tayari kumwachia aende kwa kuwa umeshaona wazi ya kuwa maamuzi uliyoyafanya au yaliofanyika yana makosa makubwa.
Waulize wanaume imekuandalia njia itakayokusaidia kurudisha muda nyuma na kuwa naye tena, kukurudishia yule mmoja umpendae ambaye juu yake ndio moyo wako unapokamilika, njia hii itategemeana sana na hali ya mwenza wako mlieachana na jinsi anavyojisikia juu yako kwa kile ulichotenda au kumtendea.
#; Yatambue makosa.
Unaweza fikiria unachofikiria kichwani mwako ila lazima huyo msichana atataka kujua ni nini kilichosababisha wewe kubadilika, wanawake wa karne ya digitali huitaji majibu ya sababu sababishi ya kile kilichokusababisha ubadilike kiasi cha huo uwamuzi kufanyika, uwe umesababisha wewe au yeye majibu yanatakiwa, na mwelezee kwa umakini utafanya nini ili kuibadilisha hio hali na kumpa mikakati thabidi na kumuonyesha nia ya kuyatatua hayo matatizo.
Wanaume wengine hujiona ngangali na kuona hali ya kuomba msamaha ni kujishusha, na inawezekana kabisa alishawahi kukutana hio hali kwenye uhusiano uliopita, muonyeshe una nia ya kubadilika badala ya kujielezea na kuomba msamaha, muonyeshe nia yako kwa matendo, kama ulikuwa unachelewa kupokea simu zake badilika wewe ndo uwe wa kwanza kumtafuta.
#; Mpe muda.
Mpe muda wa kufanya maamuzi yake, maamuzi makubwa kama hayo huwa yanachukua muda kuamuliwa, usiwe na haraka ya kutegemea majibu hapo hapo, kama kweli unamuhitaji mpe muda wa kufanya maamuzi yake mwenyewe iwapo anataka kuwa na wewe au la, inaweza kumchukua sikua au hata wiki mpaka aweze kukuamini tena na kukukabidhi moyo wake, kuwa mvumilivu na usikurupuke na kulazimisha mambo kwani itakuweka mahali pabaya zaidi ya ulipokuwa.
Mahusiano ya kimapenzi ya umbali na jinsi ya kuyafanya yawe ya mafanikio na furaha.
Usipomuona mpenzi wako kwa muda moyo huingia upweke, matamanio ya kumtaka kumuona huongezeka mara dufu, mawazo ya jinsi alivyo na kila kitu kuhusu yeye hukufanya utabasamu na kufurahia uwepo wake kila umuonapo, na hukupa hisia na tamaa ya kutaka kumuona zaidi na kukufanya hitajio la kuwa naye kukuwa na hamasa zako juu yake kuongezeka na kumpenda zaidi.
- Namba 1, Hakikisha unaongea kile kilicho moyoni mwako.
- Namba 2, Hakikisha mnapanga jinsi ya kukutana.
- Namba 3, Fanyeni vitu kwa pamoja mkiwa mbali.
- Namba 4, Tambulishaneni kwa marafiki wapya na usiwe na wivu na marafiki wake wa kiume.
Kutambulishana kwa marafiki wapya inawafanya muwe huru na kupata mengi ya kuongea.
- Namba 5, Ongeeni kwa kutumia njia za kuonana mara kwa mara.
Kuona tena tabasamu lake na jinsi uso wake unapotabasamu kulipua hisia zako maradufu na za kwake pia na kusababisha hamasa na hisia zilizosahaulika kurejea tena kwa mara nyingine.
Unampenda kimapenzi hautaki kumpoteza, ila humuelewi amebadilika.
"Je upo kwenye uhusiano wa mapenzi na mtu maalumu ambaye hutaki kumpoteza?, Je unapata hisia mbaya na unahisi kunakitu hakiko sawa maana kila ukitaka kumbusu mpenzi wako au kukaa nae muongee hana hisia tena kama alizokuanazo awali, kila kitu anakuwa na kisingizio na mizungusho mpaka unapata hisia labda kuna mtu mwingine katikati?".
Mwanaume Kiongozi anawavutia wanawake kama sumaku, unajua ni nani na anafanya nini na je wewe ni mmoja wao?
"Ni watulivu, wanajiamini, wakiingia sehemu kila mtu anasimamisha anachokifanya na kugundua uwepo wao, wakiongea watu wote wengine wanawasikiliza, wengine wanataka kukaa nao wawasikie kile wanachozungumzia na kufanya, wanawake wanataka kutoka nao, hawa ni wanaume viongozi."
Umeshamboa na kumuuzi Mpenzi wako, Tumia Njia Nzuri ya Kumuomba Msamaha.
"Hakuna kitu hawa watu wa jinsia tofauti wanachokijua kama kununa, na kama upo kwenye uhusiano wa kimapenzi lazima siku ifike mwenzio anapokataa kuongea nawe, inawezekana kosa likawa dogo au kubwa, hata kama hujui ni nini kimesababisha hawa viumbe ndivyo walivyoumbwa, kwao lazima kuna kitu utakosea tu, uwe umemtukana bibi yake au hujamsalimia mama yake lazima tatizo litakukumba tu ."
#1; Tengeneza hali ya kimaongezi.
Utajua amekununia ikiwa kila ukimsemesha hataki kuongea nawe na kamwe huwezi kuyamaliza matatizo mpaka pale atakapoanza kuongea nawe na kukitoa kile kinachomuumiza moyo, kwa hiyo tengeneza hali ya kimaongezi ili aweze kukiongelea kile kinachomsibu mpaka kuwa hivyo na kukununia, using'ang'anize neno kwa kumuuliza mfululizo ni tatizo gani linalomsibu, kurudia rudia swali ni kusababisha makubwa zaidi.
Kama hujui kweli chochote kinachomfanya awe hivyo, jaribu kupatishia hata kama ukipatishia ambacho sio itasaidia maana utakua umetengeneza hali ya kimaongezi itakayofanya nyie wawili muweze kuongea tena.
#2; Mfanye acheke na kutabasamu.
Ukiwa na uwezo wa kumchekesha ni kipaji kizuri kitakachoweza kukufikisha mbali na wanawake, japo sio kila muda kumfanya arudishe tabasamu kunawezekana, saa nyingine kunaweza kukufanya uonekane wa ajabu na kulipua hasira yake zaidi, kwahiyo kama ameuzika kwa hali ya juu, kumtania kutaongeza matatizo mara mbili zaidi na kuona kama unamchukulia ki mzaha sana.
Unatakiwa kupima hali halisi, kama kosa lako ni kusahau kuendea maziwa dukani kama ulivyokua umemuahidi, ucheshi kidogo unaweza kumaliza tatizo, na iwapo kosa ni kuwa amekukuta na alama ya lipstiki kwenye shati lako la kazini lile jeupe, hapo kijana usiingize utani hata kidogo.
#3; Mnunulie maua ukiambatanisha chokuleti na kadi.
Kumnunulia zawadi ni njia rahisi nzuri kuondoa mnuno wake.
Ushauri; Kumtumia maua au zawadi baada tu ya kumuuzi kunapoteza uzito, anaweza kukudhania unajaribu kumnunua kwa zawadi wakati unajua ulichokifanya kimemuuiza hisia zake.
Ili uweze kudhibiti hii hali, mtumie zawadi baada ya kuwa umeshazungumza naye na kuweka mambo kidogo katika hali nzuri, na itaongeza chachu nzuri zaidi maana hata kuwa anategemea kitu kama hicho kutoka kwako na kufanya aongeze hamasa zaidi juu yako.
Ukimtuia kazini kwake ni vizuri zaidi maana atapewa sifa na wafanyakazi wenzake na kukufanya uwekwe juu zaidi.
#4; Msikilize kile anachokiongea.
Mara nyingi wanawake wanapenda kutoa hasira zao kwa kuongea, anataka kujua kuhusu tabia yako mbaya iliyomchukiza na kwanini imetokea hivyo, na unaweza kuta ni kitu kidogo tu, labda wewe hukumsikiliza vizuri na ndo kimesababisha mambo yote haya kutokea.
Kusikiliza ni karama, mwache aongee na hakikisha upo makini wakati unamsikiliza na ni vizuri ukamwacha aongee bila wewe kuingilia kati kwenye maongezi, kumuingilia wakati anaongea ili kujitetea kutasababisha zogo na kufanya tatizo lipanuke zaidi.
#5; Ondoka.
Saa nyingine kitu cha msingi unachoweza fanya ni kuondoka, toka nje ya chumba au nyumba, mpe nafasi apumue hasira zishuke, ni mwiko na usijaribu kuondoka wakati bado anaongea, ukishatambua yupo kwenye hasira kubwa sana haja ya kuendelea kuongea naye haito saidia, kwa muda huo ni vizuri kumwambia kuwa unampa nafasi apunguze hasira na kuweka mawazo yake vizuri ili baadae muweze kuongea mpate mwafaka na kuelewana vizuri zaidi, baada ya hapo unaweza kuondoka.
#6; Omba msamaha.
Mwishoni hakuna kitu kinachoweza kufunika neno "Samahani" lililotoka moyoni, na huwezi kumaliza ugomvi naye iwapo usipolitumia.
Hakikisha wakati unaliongea unalimaanisha, mwangalie machoni kwa upole na sema "SAMAHANI", usiseme naomba msamaha wala samahani matendo yangu yamekuudhi, maelezo kama hayo hufanya maongezi kuhusu hilo jambo yaendelee zaidi, sema samahani na maanisha kweli baada ya hapo bainisha samahani yako ni ya sababu gani ili aelewe umeelewa kwanini ulikua umemuudhi, kama ulikua ni uhusiano wa muda mrefu, mkumbushe mlikotoka.