juu

Wednesday 28 August 2019

Ni nini maana ya ukosefu wa nguvu za kiume?


Ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume ni ile hali ya mwanaume kutokuwa na uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa kwa ufasaha.
Tatizo hili linawakabili mamilioni ya wanaume duniani na limekuwa na athari nyingi kama vile kuvunjika kwa mahusiano na hata ndoa.
Mwanaume mwenye tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume anakuwa hana uwezo wa kumtosheleza mwanamke kwenye tendo la ndoa.
DALILI ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME
Mwanaume anayekabiliwa na tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume huonyesha dalili zifuatazo:-
1. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake barabara. Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali ) unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama msumari, lakini kwa mwanaume anaye kabiliwa na tatizo hili uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na huweza kusinyaa wakati wowote. Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume. Mishipa ya uume ndio inayo ufanya uume usimame barabara.
Mishipa hii inapokuwa imelegea, uume hauwezi kusimama barabara hata iweje. Kulegea kwa mishipa ya kiume kunasababishwa na upigaji wa punyeto kwa muda mrefu. Mtu anaye piga punyeto anakuwa anaiminya mishipa inayo sababisha kusimama kwa uume, baada ya muda fulani, mishipa hiyo huishiwa nguvu na kulegea na hivyo linapo kuja suala la kusimamisha uume, mwanaume huyu anakuwa hana uwezo tena wa kusimamisha uume wake.
Vilevile matumizi ya madawa makali (hususani madawa ya kizungu) ya kuongeza nguvu za kiume, husababisha mishipa ya uume kulegea. Hii ni kwa sababu madawa haya hui-overdose mishipa hiyo na kuilazimisha kufanya kazi zaidi ya kiwango chake.
Matumizi haya yanapokuwa ya muda mrefu humfanya muhusika kuwa tegemezi na pia hufanya mishipa ya uume wa muhusika kulegea na kukosa nguvu.
2. Kukosa hamu ya tendo la ndoa: Hapa mwanaume anakuwa hana uwezo wa kutamani kufanya tendo la ndoa hata anapokuwa faragha na mke wake. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa husababishwa na msongo wa mawazo.
3. Kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara moja. Hapa mwanaume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakuwa hana tena uwezo wa kurudia mshindo mwingine. Hali hii husababishwa na kutokuwa na msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya kwenye uume.
4. Kufika kileleni mapema
5. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha kabisa. Hali hii hutokea pindi tatizo la kutokuwepo kwa msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume, linapokuwa limekomaa. Na wakati mwingine, hali hii hutokea pindi vyanzo zaidi ya kimoja vya tatizo la kiume vinapo kuwa vimejitokeza kwa mtu mmoja.
6. Uume kusinyaa na kurudi ndani. Hapa uume wa mwanaume unakuwa umesinyaa na kurudi ndani. Uume huu unakuwa hauna uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa. Hali hii kwa kiasi kikubwa husababishwa na upigaji wa punyeto kwa muda mrefu pamoja na magonjwa hasa hasa chango la kiume au ngiri.
Tajwa hapo juu ni dalili kuu za tatizo la ukosefu ama/na upungufu wa nguvu za kiume.




Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger