juu

Friday 23 August 2019

FAHAMU AINA YA WANAUME NA TABIA ZAO

Katika mahusiano ni vizuri unapoingia katika mahusiano ya uchumba au kwenye ndoa,jitahidi kusoma tabia na Hulka ya Mwenza wako na Uridhike nayo au Uiboreshe sawa na unavyopenda_. 
Kwanza inabidi ujue aina ya mme wako(kulingana na muukiza swali):. 
1.Wanaume wasiotaka kuonekana hawajui kitu flan.( *_Hawa bhana ni wanaume ambao kila kitu anakijua,hata kile asichokijua anajifanya anakijua, mara nyingi hawa uwa wanakawaida ya kupenda kujulikana na sifa) Tabia hii hutokana na kukaa kwenye mazingira yasiyompa changamoto au watu wasiompa changamoto ila yeye anajiona ndo yuko juu ya wote. 
Watu wa aina hii awe mke au mme mara nyingi huwa kero hata kwenye familia au kwenye jamii maana HAWASHAURIKI ila yeye akushauri. Mara nyingi maamuzi yao niya KUSHUTUKIZA hayana mipango na mashauri kwakuwa wanapenda waendelee kuoekana wao ndo wanaweza na wanajua sana kuliko wengine ili waendelee kuogopwa(Hii ni aina ya kwanza ya watu(kwa muuliza swali, aina ya kwanza ya mme) 
2. *Wanaume wasiotambua nafasi ya mwanamke* Hawa ni aina ya wanaume ambao saikolojia yao imeathiriwa na mazingira ya kimakuzi,kimalezi,na makundi, hawa mara nyingi wana kitu tunakiita *Poor Psychological Interpretation* (Udhaifu wa tafsiri katika akili zao)mara nyingi wanapenda kuona wenzao Hawawezi,hawajui….. *Hawa wana Generalization Problem* (tatizo la kujumuisha) kama waliona,walipitia,walisikia, kwa wazazi,ndugu, jamii udhaifu wa mwanamke mmoja au baadhi ya wanawake wanamapungufu kadhaa, *Uyahamisha na kuyafanya ni matatizo ya wanawake wote* uanza kujihami (defense mechanism ) hapa ndo tunapata wale *Wasiosifia wake zao,hata wafanye vizuri,wavae wapendeze,lolote niwagumu kusifia* kwa nini hawafanyi…. Saikolojia yao inawambia KUMSIFIA NIKUMPANDISHA NAFASI mlingane,au akudharau,kukuzoea. 
3. *Aina nyingine ni wanaume wa Heshima(tunawaita WANAUME MACHIFU ),hawa wanapenda tu kuwa juu,kuheshimiwa,wanapenda kuweka mipaka (daraja kubwa)kati yao na wake zao mpaka watoto wao. Hawapendi kuzoelewa na mke wala watoto. 
4. *Kuna BABY HUSBAND(Wanaume watoto)* hawa ni wanaume wadekaji,lakini pia niwapolee,ila hawajishulishi kiakili,kila kitu mpaka aamuliwe na mtu mwingine aidha wazazi,ndugu au marafiki. Hawa ikitokea shida ndogo kwenye ndoa na familia kila eneo watajua,wahaha na kuogopa sana. 
5. *Friendly Husband*(Mwanaume Rafiki) hawa ni miongoni mwa wanaume AMAZING & ROMANTIC (wanaume wa pekee na wamahaba)wanaheshimu hisia za wake zao,wanapenda ku Present wake zao vizuri kwa watu,wanapenda sana kuwa karibu na wake zao na watoto zao, ni Caring husband,ni walinzi wa familia na hisia za wenzao,wanapenda romantic play(kucheza na kutaniana na wenza wao)wanasifia,wanashaurika,wanasikiliza,wanadekeza nk. Hili ni kundi ukifanikiwa kulipata hakikisha unakuwa mnyenyekevu sana kwao utafanijiwa sana na ndoa yako itakuwa Tamu sana. 
*_Kama una aina zingine nne hapo juu,jitahidi sana kufanya vizuri,usi React kwenye udhaifu wake,usishindane naye,TIMIZA WAJIBU WAKO hilo ndo litakusaidia kuepuka makali yake na kumwombea maana hiyo ndo HULKA YAKE.






Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger