Mwanaume ambaye atakuwa na ukwasi wa kutosha huyo ndiye anayefaa kuwa naye kwenye uhusiano au hata ndoa. Anaamini kwamba pesa ndiyo kila kitu. Pesa ndiyo itakayompa mahitaji yake ya kupendeza na kila kitu. Mwanaume bila pesa kwake ni sawa na debe tupu. Upepo wa imani hiyo upo sana mjini.
Baadhi ya wanawake wanaolewa na watu wenye pesa, lakini matokeo yake wanageuka kuwa watumishi wa nyumbani wa hao wanaume wao. Wanageuka kuwa wafanyakazi wa ndani na si wake tena. Wanakosa sauti ya kusema, lakini mioyoni wanabeba mambo mazito yanayofukuta kama moto.
Hawazifurahii ndoa zao, wanaambulia masimango, manyanyaso ya kila aina maishani mwao. Hii ni hatari sana! Unaweza kuishi na mwanaume asiyekuwa na pesa, lakini
kipaumbele kikubwa kiwe ni mambo niliyoyataja hapo juu. Ishi na mtu ambaye hata kama hana pesa, lakini ana utu, ana ubinadamu na hofu ya Mungu.
Kikubwa zaidi angalia mwanaume ambaye anajielewa. Anayejitambua, anayeamini katika kutafuta maisha. Kwamba hata kama hana pesa, lakini akili yake iamini katika kutafuta. Kama hiyo akili, mwanamke ni jukumu lako kumkumbusha.
Mweleze mwanaume wako juu ya umuhimu wa kutafuta. Wekeni mipango ya pamoja, mnapowaza pamoja juu ya changamoto zenu hakuna kitakachowashinda.
Baadhi ya wanaume huwa ni wazito kuwashirikisha wanawake wao mambo ya kimaendeleo. Mshtue mwanaume wako kuhusu masuala ya kimaendeleo.
Mjengee utaratibu wa kuzungumza kuhusu fursa mbalimbali zenye mtaji mdogo na hata mkubwa. Zile zenye mitaji mikubwa mnaweza kuzifikia pale mtakapofanikisha zile za mitaji midogo.
Mnachotakiwa ni kufurahia maisha yenu. Kuyakubali na kupanga mikakati ya pamoja ya kuelekea kwenye maisha mnayoyatamani.
0 comments:
Post a Comment