juu

Wednesday, 28 August 2019

ZIFAHAMU FAIDA ZA KUWA KWENYE NDOA

Ndoa ni muungano wa watu wawili wenye nia ya kuishi pamoja pengine kwa maisha yao yote. Ni muungano wenye malengo ya kujenga familia pamoja na kuiongoza kwa namna ambavyo itakuwa bora kwao.

Utafiti unaonyesha kuwa kuna faida za kuwa katika ndoa kiuchumi na kiafya. Watu walio katika ndoa huwa na afya njema na pia huwa na maendeleo zaidi kiuchumi ukilinganisha na wale ambao wanaishi peke yao.

Watu ambao wapo katika katika ndoa wana nafasi ndogo ya kupata magonjwa ya moyo kwa 5% ukilinganisha na wale ambao hawako katika ndoa ambao wana hatari kwa 3% zaidi ya kupata magonjwa hayo.

Hali kadhalika wale ambao wako katika ndoa wananafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa zaidi ya maendeleo kuliko watu wawili ambao hawako katika ndoa. Hii inasababishwa na mtindo wa maisha ambao wasio katika ndoa wanaishi. Vitu kama ulaji mbaya,ulevi usio na mipaka na matumizi mabaya ya fedha zao.

Faida za Kuwa Katika Ndoa Kiafya
Kwa wastani utafiti unaonyesha watu ambao wako katika ndoa wanaishi maisha marefu yenye afya na furaha zaidi kuliko wale wasiokuwa katika uhusiano ya ndoa.

Wanaume ambao hawana uhusiano wa ndoa wanakawaida ya kula vibaya vyakula visivyo na faida kiafya. Baadhi yao wanakuwa walevi na matumizi yao ya fedha yanakuwa makubwa.

Kwa kuwa hawapiki nyumbani, hula sehemu za jumuia kama migahawani na katika vilabu vya pombe. Vyakula hivi havina mchanganyiko mzuri wa virutubisho vinavyohitajika katika mwili.

Wanawake wasioolewa nao ulaji wao wakati mwingi unakuwa wa kula nje japo si kama wanaume,lakini pia wanakula vibaya vyakula vyenye mafuta mengi na visivyo na virutubisho muhimu. Vyote katika hivi vinapelekea kuhatarisha afya zao.

Wanawake na wanaume ambao wameachana au mwenza wao amefariki wanazongwa sana na upweke wa kihisia. Hili hupelekea kupata magonjwa yanayosababishwa na msongo wa mawazo.

Uzalishwaji wa kemikali ya endorphin ambayo inafanya kazi ya kutuliza maumivu mwilini na kumfanya mtu awe mwenye furaha unakuwa wa kiasi kidogo na hivyo kikumbwa na matatizo ya kiafya na kihisia.

Imefahamika kuwa wanawake na wanaume wasio na ndoa wanakuwa na hasira na wakali sehemu za kazi na kwa watu wengine wanaokutana nao,na wanakuwa wagumu kuelewana na watu katika mahusiano ya kikazi au jumuiya nyingine.

Faida za Kuwa Katika Ndoa Kiuchumi

Kuna faida nyingi zinazotokana na watu kuwa katika ndoa ambazo huleta mafanikio kiuchumi

Matumizi Machache
Tumeona kuwa watu wasiokuwa katika ndoa hula chakula nje zaidi na kunywa vilevi, hivyo hutumia fedha zaidi kwa mambo yasiyo ya msingi hasa kwa wanaume.

Wanawake hali kadharika hutumia fedha nyingi katika mavazi na vipodozi wakiwa hawako katika ndoa kuliko wale walioolewa.

Malengo ya Muda Mrefu
Mipango ya watu wasio katika ndoa huwa ni ya muda mfupi na starehe zaidi hivyo kufanya maendeleo yao kiuchumi kuwa chini. Kinyume chake ni kuwa wale ambao wako katika mahusiano hupunguza matumizi kwa kula nyumbani zaidi na kupunguza matumizi katika vitu visivyo vya muhimu kama mavazi ya fahari.

Malengo ya watu waliooana huwa ya kujenga familia na ni malengo ya muda mrefu. Badala ya kufanya starehe kupita kiasi huwekeza katika ujenzi na biashara ambazo zitaongeza kipato chao.

Kipato Kikubwa
Kipato chao pia huongezeka kwa kuweka nguvu pamoja. Kama wote ni waajiriwa basi kutakuwa na mishahara miwili mwisho wa kila mwezi badala ya mtu mmoja na hivyo uwezo wao wa kufanya mambo makubwa unaongezeka.

Watoto wanapozaliwa katika familia huongeza mahitaji ya familia na ghrama huongezeka. Kwa kuwa inasemekana kuwa “uwezo wa binadamu kufikiri hukua kutokana na tatizo” wazazi walio katika ndoa hupata jinsi nyingine ya kuongeza kipato na hivyo kukua kiuchumi. Watafikiria miradi zaidi au hata kutafuta kazi inayowalipa zaidi.

Ni wazi kuwa kuna raha ya kuwa na mtu unayempenda katika maisha yako na kujenga naye familia. Kama ndoa yenu ina furaha ni wazi utakuwa mtu mwenye furaha; na inajuliknana kuwa mtu mwenye furaha huishi maisha marefu na huwa na afya nyema.

Hali kadhalika walio katika ndoa wana wajibika zaidi kuliko wale wasio katika ndoa na huweka jitihada za ziada za kujiongezea kipato. Hivyo uchumi wa walio katika ndoa huimarika zaidi na kuwafanya waendelee kwa haraka.

Lakini ifahamike kuwa hili linawezekana tu kama ndoa yao ina furaha, ikiwa vinginevyo matokeo huwa kinyume chake.






Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger