Nyumbani kwetu kila siku ni kulalamika kwani msahara wangu ni kama milioni na nusu lakini huwezi amini kuna wakati hata pesa ya vocha nakosa. Nikimuomba mume wangu ananiambia nina matumizi mabaya, hela yake sijawahi kuiona nikiongea anasema ana majukumu kwani wadogo zake wanasoma. Nahangaika kwenye viposho vya ofisini nakusanya, nilikusanya mpaka nikapata milioni tatu, lengo lilikua ni kununua kiwanja kwani mume wangu pamoja na kuchukua pesa zote ni mtu wa pombe tu na wanawake.
Yaani ukimuambia mambo ya maendeleo atakutukana na hata kukupiga kuwa unampangia maisha. Nilipopata ile pesa nikamuambia mume wangu, akasema basia atanunua kiwanja, kweli alipata kiwanja akanunua lakini badala ya kuandika majina yetu wote aliandika jina lake mwenyewe, namuuliza kwanini anasema inamaana huniamini. Basi nikakaa kimya, tatizo linakuja kwenye kujenga, kila nikimuambia kujenga anasema hana pesa ana mambo mengi. Lakini mimi pesa zake sizioni anasingizia majukumu majukumu.
Mwezi wa sita aliniambia nichukue mkopo, tukaongea vizuri akasema kwakua tuna kiwanja basi tuchukue kopo kwa msahahara wangu ili tujenge harakaharaka, alionekana kubadilika na kuwa na mawazo mazuri alisema yeye atakakua anahudumia familia. Nilichukua mkopo wa milioni 18 nikampa, kwaajili ya ujenzi, lakini Kaka juzu nakuta mwanaume kumbe kaagiza gari, namuuliza anasema watu wanamdharau mtaani hana gari hivyo ni bora tuwe na gari ya kutembelea, kaka nimeumia sana kwani mkopo nakatwa mimi, gari aliyonunua ni tya ghali, milioni 28 kaka kanunua gari wakati hata nyumba hatuna.
Naomba ushauri nifanye nini maana naona kama nachanganyikiwa na tangu anunue gari hata nyumbani hajarudi yupo tu na marafiki zake huko
0 comments:
Post a Comment