Wapendwa karibuni kwenye darasa la mahusiano. Leo tutazungumzia umuhimu wa wapenzi wanapofurahia kuwa pamoja hasa zile nyakati za usiku na kupeana raha za ulimwengu.
Wapo ambao wanawake huzikosa raha hizo kwa vile tu mwanaume wake huchelewe kurudi nyumbani ama kuingia alfajiri au mwingine asirudi kabisa nyumbani.
Mara nyingi masuala ya kuchelewa kurudi nyumbani ama kutokuonekana kabisa huwa yanafanywa mara nyingi na wanaune.
Katika mahusiani jambo hilo huwaumiza wanawake wengi hasa wanaune zao wanaporudi alfajiri ama hawarudi huku wake zao wakiwa hawana taarifa zao.
Mwingine anapigiwa simu anamuambia mkewe yupo baa hivi hizo baa zisizoisha hadi alfajiri kulikoni je ni marafiki zako kila siku unakuwa nao au michepuko unasingizia marafiki.
Kwa nini hata siku moja hujawahi kumchukua mkeo na kuwa naye katika hivyo viwanja vya kujivinjari naye akajionea hayo mnayoyafanya hadi alfajiri
Hakuna raha mwanamke anayoipenda kama kutolewa Out na mumewe ama mpenzi wake.
Baadhi ya wanaume wamekuwa na tabia za ajabu akitoka na mkewe watawahi kurudi nyumbani akiwa mwenyewe anarudi majogoo yanaweka.
Mke nyumbani kazi yake ni kushtuka mara kuangalia saa akipiga simu haipokelewe mnawachosha wanawake wenu nyumbani.
Ni vizuri mwanamke mwenzangu ukachukua hatua hata siku moja moja ukajua hayo maeneo yake ambayo anayataja anajivinjari hata ukafika usikubali kuwa mlinzi wa nyumba.
Asikuambie mtu hakuna maumivu unayoyapata kama kuwa mlinzi wa nyumba na mbaya zaidi akirudi hana muda na wewe unazidi kupata maumivu mara mbili.
Chunguza kwa umakini mwanaume wako ukiona inafika alfajiri yeye ndio anarudi alafu hana muda na wewe jua ndio katoka kwa mchepuko.
Haiwezekani uwe ni mtu wa kurudi nyumbani kumekucha alafu unasema ulikuwa misele.
Hivi misele gani unaipiga mwenyewe wanaume wanapenda wawe na mtu pembeni iweje wa kwako umuache awe security nyumbani.
Hivi kweli unaenda baa unakaa mpaka kumekucha upo mwenyewe hapo ni kudanganyana kwa nini usimuite mkeo mkawa pamoja mpaka kukuche mkarudi nyumbani.
Usiku ni muda wa kumilikiwa na mkeo anahitaji huduma zake kama pipi ya kijiti sasa anapoikosa anapatwa maumivu.
Mwanamke alichokifuata kwako ni mapenzi na upendo sasa wewe unavyomuacha awe mlinzi wa nyumba sikuelewe embu wanaume badilikeni.
Ukijiona hujamaliza ujana wako ni heri binti wa watu ukamuacha aendelee kukaa nyumbani kwao kuliko kumfanya mlinzi wa nyumba.
0 comments:
Post a Comment