MAISHA ya uhusiano yana changamoto nyingi sana. Yana raha na wakati mwingine yana karaha. Penzi linapokuwa moto, ni vigumu sana kujua au kufikiria yule aliyeko kwenye mateso ya mapenzi. Unaona kila kitu kinakwenda sawia, unaamini watu wote wapo hivyo. Sikia, kuna watu wanapitia kwenye wakati mgumu kwenye mapenzi kiasi cha kufika mahali pa kujuta. Mtu anajitahidi kufanya kila liwezekanalo ili tu kuhakikisha uhusiano wake unaendelea kukua, lakini wapi!
Rafiki zangu, maisha ya uhusiano haya yanahitaji kuelewana. Ndiyo maana nimekuwa nikieleza mara kwa mara katika makala zangu, ukiwa angali kwenye hatua za mwanzo, basi shughulikia sana kuhusu suala la maelewano. Ulipime kwenye mizani ili uweze kuona kama ‘damu’ zenu zinaendana au la. Achana na haya mambo, sijui mwenzangu mpole sana au mzuri sana, kila mtu anamtamani, lakini kubwa kwako liwe ni kuangalia ‘kuivana’.
Mtu ambaye unataka aje kuwa mume au mke wako ni vizuri mkawa mnaelewa. Yule ndiye msiri wako, ni mtu ambaye atakuwa wako wa maisha. Hivyo basi unashauriwa sana kutokata tamaa, kuwa mvumilivu kwa kiasi ambacho utaona kinafaa.
Watu wengi wamekuwa wakikutana na changamoto ya kuanzisha uhusiano mpya kila siku kwa sababu tu ya kushindwa kuwa wavumilivu, lakini katika uvumilivu huo unapaswa kuwa mtu wa kupima. Weka kwenye mizani kiwango cha ugomvi wenu halafu linganisha na furaha.
Kama unaona furaha inazidiwa na ugomvi kwa kiasi kikubwa halafu kwa muda mrefu, basi ujue kabisa ulipo si sehemu sahihi. Sehemu ambayo ina maumivu makali, yanayojirudia na umefanya jitihada za kuweka mambo sawa, lakini imeshindikana, basi ni bora kujitoa. Nasema jitoe pale tu unapoona umefanya jitihada za muda mrefu, halafu unaona matatizo makubwa yamekuwa yakikuandana, basi huo ni muda wa kujitoa. Nasema jitoe kwa sababu haiwezekani ukawa mtu wa mateso maisha yako yote.
Wahenga walisema, mapenzi yanaua, upo tayari kufa kwa ajili tu ya kumpenda mtu? Mathalan unayempenda anakudunda kila kukicha, anakutishia kukuchinja, anatamani kukuwekea sumu ufe, sasa hapo kuna maisha tena?
Ndiyo maana nikasema inapofikia hatua kama hiyo niliyoianisha hapo juu, penzi la kujitoa linakuhusu. Unapoishi na mtu halafu akawa anakutamkia mara kwa mara juu ya suala la kukutoa uhai, eneo hilo siyo salama kabisa.
Penzi bora ni lile ambalo lina amani. Penzi ambalo wote mkionana mnafu-rahiana. Kila mmoja anakuwa na hamu na mwenzake, mnaishi kama marafiki na hamgo-mbanigo-mbani mara kwa mara. Mnapo-ishi kwenye furaha namna hiyo, basi hata maisha yenu yata-stawi.
Mapenzi yanaleta maendeleo kwenye nyumba. Kama unaishi na mtu ambaye mnasi-kilizana na mnape-ndana, basi hata mafanikio yatakuja. Maana mtaelekezana kwa upole, mtatiana moyo na kuwekeza akili yenu katika masuala ya maendeleo.
Mnapokuwa kwenye mbilinge za ugomvi kila siku mtaendelea lini? Ni vyema sana kuwa makini na hili hususan mnapokuwa kwenye kipindi cha awali. Mtu ambaye ana matatizo ya kila siku, umempa muda mrefu wa kubadilika imeshindikana, lakini mbaya zaidi anakuwa tishio baya kwako, basi ni bora mkaachana mapema na kwa amani.
Usingoje kutokea kwenye vyombo vya habari kama marehemu kutokana na ugomvi wa mapenzi. Ishi na mtu ambaye mnazungumza lugha moja, mnapendana kwa dhati na mwenye hofu ya Mungu. Hapo ndipo utayaona mapenzi ni matamu! Instagram& Facebook: Erick Evarist, Twitter: ENangale. Watu wengi wamekuwa wakikutana na changa-moto ya kuanzisha uhusiano mpya kila…
The post Kuna penzi la kujitoa, jitoe ikibidi appeared first on Global Publishers.
source https://sirinzitozamapenzi.blogspot.com/2019/08/kuna-penzi-la-kujitoa-jitoe-ikibidi.html
0 comments:
Post a Comment