juu

Saturday, 17 August 2019

MITINDO YA KULALA HUELEZEA MAPENZI BAINA YA WANANDOA

Wakati wa kulala si lazima wapenzi wafuate utaratibu ule ule kila mara.Hii inawezekana msimamo wa akili ulivyo kwa wakati huo.Fuatilia mitindo ya ulalaji na maana yake::  
KUKUMBATIANA  
Mtindo huu hutumika sana kwa miaka 5 ya mwanzo wa ndoa.Mume huweka miguu juu ya mkewe na mikono kumkumbatia eneo la kifuani.Aina hii hupendwa sana na wanawake kwani hujiona yuko salama  
Ni alama ya mahusiano bora ya kimapenzi.
::  
KUTAZAMANA  
Hukumbatiana lakini baada ya saa 2 au 3 hujibagua na kila mmoja kulala upande wake.Ni alama ya kusaidia kuondoa mkinzano unaoweza kujitokeza.  
::  
MALIWAZO YA MUME  
Hushikana mikono na mke kuweka kichwa chake kwenye mabega au juu ya kifua cha mumewe.  
Ni alama ya tafsiri ya mapenzi ya dhati ya mume kwa mke.  
::  
BARAFU WA MOYO  
Mke hupanda juu ya mume na wanaweza kujadiliana mambo mbalimbali.Ni alama nzuri nyakati za maelewano.  
::  
KILA MMOJA UPANDE WAKE  
Ikiwa mmoja kaweka mguu mmoja au mkono kwa mwenzake,mtindo huu hujulikana kama daraja la mahusiano.Si alama ya kutiliwa mashaka  
::  
USINGIZI BARIDI  
Pale wanandoa wanapolala kama wasiotambuana bila kugusana pasipo kujielewa ni alama kuwa wako mbali kifikra.Hutokea pale mvuto usipokuwepo  
Hali hii isiruhusiwe ikue.  
::  
VISIWA TOFAUTI  
Wanalala bila ushirikiano kwa visingizio vya kuchoka,ni kama visiwa viwili tofauti.  
Chanzo chaweza kuwa matatizo ya kimwili,kiakili au kiuchumi.Hali hii ikitokea mara kwa mara huweza hata kuachanisha wapenzi  
::  
MGONGO KWA MGONGO  
Mtindo huu hujitokeza sana kwa wapenzi.Ingawa wanaweza kupeana migongo lakini wanaweza kuwasiliana.Ni alama ya kawaida na wanasaikolojia wanauita mtindo huu “muda wa kupumzika”  
::  
MZIGO USIOHITAJIKA  
Kila mmoja hulala kivyake na mara nyingi ni kama vile wanandoa wanataka kuonyeshana umwamba.Kila mmoja hamjali mwenzake,,hali hii si ya kawaida ni mbaya sana kwani hutengana kuanzia wanapopanda kitandani hadi kunapokucha.Si ajabu hata kununua vitanda viwili au kulala vyumba tofauti.Wanasaikolojia wanaita hali hii kiburi na jeuri.






Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger