juu

Sunday, 8 September 2019

Jinsi Ya Kumdhaifisha Mwanamke Ili Akupende


#1 Kuwa mkarimu wa ukweli. Hauwezi kufeki jambo hili. Wanawake kwa kawaida huvutiwa na wanaume ambao wanaonyesha ukarimu wa ukweli. Ukiwa mkarimu kwa wengine, itamuonyesha mwanamke vile ambavyo utamchukulia. Huu ni udhaifu mkuu kwa kila mwanamke.
#2 Tabia za usaidizi. Udhaifu wa kila mwanamke ni kuwa na mwanaume msaidivu. Wakiwa wanapewa sapoti na mtu, huwa kawaida wanavutiwa na mtu kama huyo. Kuna kitu ambacho hujitokeza ndani yako wakati kuna mtu anajitokeza na kukusaidia katika maisha yako. Kwa mwanamke huwa maradufu. Usaidivu wako kwa mwanamke kunamfanya awe dhaifu kwako.
#3 Kushangilia mambo anayotimiza katika maisha yake. Kwa kuongezea usaidivu wako, wanawake hupenda mtu ambaye anafurahia na kushangilia mambo ambayo anatimiza maishani mwake. Wakati wamepandishwa cheo kazini ama amemaliza kufanya mradi wake, kukiwa na mtu karibu yake ambaye atashangilia mafanikio yake kila wakati ni jambo ambalo kila mwanamke anatamani.
#4  Kupendezwa na hamu zake. Hii haimaanishi kuwa udhaifu wa kila mwanamke ni kuiga kila kitu ambacho anapenda, la. Hii ni ile hatua ambayo unakuwa na interest na mambo muhimu ambayo huyapenda zaidi katika maisha yake. Kwa mfano ukimwona mwanamke anapenda sana mchezo wa magongo ama anapenda kufuatilia maisha wa wasanii aina flani, basi wewe jifunze kucheza mchezo wa magongo na pia uanze kuwatambua wasanii husika. Akiona kuwa unapenda mambo ambayo anapenda utakuwa umemdhaifisha.
Haya ndio mambo muhimu ya kuzingatia kama unataka kumfanya mwanamke adhaifike mbele yako. Kando na mambo hayo manne makuu unapaswa kujihami na mambo haya ambayo yatakufanya uuteke moyo wake:
#1 Lazima uwe mmakinivu na maswala yake ya ndani. Wakati mwingine wanaume huchoshwa kusikia malalamishi ya mwanamke lakini siri kuu ya kumteka mwanamke ni kuwa msikivu kwa kila kitu anachokuambia coz atakuona kama jangina wake wa maisha.
#2 Mpe saport kwa kila kitu. Kuna wakati anaweza kuongea mambo ambayo kwa msingi unaona kuwa hawezi kutimiza. Akifikia hapo wewe unapaswa kunyamaza tu. Unapaswa umpe sapoti kwa kila kitu. Haijalishi kama unamuelewa au la, unapaswa umsaidie tu.  Bora tu mambo yake anayojaribu kutimiza hayamdhuru yeyote ama yeye mwenyewe.
#3 Muulize maswali. Unaweza kuona labda jambo hili halina maana yeyote. Lakini ukiwa unamuuliza maswali mara kwa mara kuhusiana na miradi yake ama mambo anayofanya siku baada ya nyingine utakuja kumuelewa zaidi. Hii itasaidia kwa sababu atakuona unajihusisha na maswala yale ya maisha hivyo atavutiwa na wewe na utatumia swala hili kama udhaifu wake upo
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger