juu

Sunday, 8 September 2019

Jinsi Ya Kumshawishi Mwanamke Mtandaoni


1. Mtongoze
Kama maisha ya kawaida, kumtongoza mwanamke akiwa online ni lazima kama ibada. Itakuwa bora zaidi ukichanganya mitindo spesho ya kutongoza mara kwa mara, Mnyeshee kwa kumsifu siku moja halafu unakuwa mfidhuli siku nyingine. Jambo muhimu hapa ni utambue kuwa lazima unafaa kumfanya awe ametulia wakati unapochat nayeye. Pia lazima awe anajiskie yuko huru kabisa wakati mnapoongea. Hii itahakikisha kuwa anapenda na kufurahia kutaka kukujua zaidi na labda siku moja atatamani muweze kukutana ana kwa ana.
2. Tafuta maneno ya kwako
Usithubutu kutafuta mistari ya papo kwa papo kwani kawaida haifaulu katika mitandao. Kile unachohitajika kufanya ni kuhakikisha umepanga conversation yenu vizuri ili isiweze kukwama mbeleni. Pia hakikisha kuwa unaingiza maneno ambayo yataleta hisia za kucheka na furaha. Hii itamfanya amakinike zaidi na wewe.
3. Mfanye Acheke
Ok najua si kila mtu ana talanta ya kumfanya mwanamke yeyote acheke kama vile mzee Majuto lakini unafaa angalau utumie maujanja uliozaliwa nayo ili kumfanya mwanamke acheke. Nasema hivi kwa sababu wanawake wengi kawaida hupenda wanaume wacheshi. Ukitumia mbinu hii utamfanya akiwa offline ama online, fikra zake zitakuwa kwako.
4. Usimwambie kila kitu chako
Ukiwa unachat na mwanamke online, hakikisha humwambii kila kitu chako kwa wakati mmoja. Hakikisha ya kuwa kama mnachat unamfungulia moyo wako pole pole. Hii itamfanya yeye kuwa na shauku ya kutaka kukujua zaidi. Ukiweka baadhi za siri zako kikapuni, lazma ataingiwa na tamaa ya maswali hivyo kutaka kuongea na wewe zaidi na zaidi.

5. Kutana na yeye uso kwa uso.
Mwisho wa siku -baada ya kumtongoza na kumjua nje na ndani -unafaa kumuuliza kama atatoka out na wewe. Kumbuka hii ni level nyingine kubwa sana katika chat ya online hivyo kabla hujamuagiza mukutane uso kwa uso, lazima ujipange vilivyo
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger