Babe anatakiwa kuwa mshamba kidogo… Siyo unadate binti anajua mpaka Lukaku alifunga mabao mangapi msimu uliopita??…
Demu unakaa naye anamjua Boro Yanki, Van Dame, Bill Branks…. Anakuadithia "anodi ya jini mwanzo mwisho"…
Yaani huna hata kipya cha kumfundisha…
Binti anatakiwa ukimuuliza "Bebi unamjua Rooney?? " anakujibu "Namsikia tuu.. Hivi ameimba wimbo gani?? "
Babe anatakiwa kuwa mshamba kidogo… Yaani eti babe anampenda Undertaker na Marehemu Umaga…
Binti anangaalia Movie ya Wrong Turn hata hajifichi amekodoa mimacho kuanzia mwanzo mpaka list ya majina inapita…
Babe anatakiwa ukiangalia naye Final Destination muda wote kafumba macho… Kila Mara anaongea na waigizaji… "Jamani wewe usiende utakufa huko" Mara unasikia "babe toa hii nitaota"…
Siyo Bae anakaza mdomo kabisa kwa hasira mtu akikoswakoswa kufa unamsikia kudadeki afe tu huyo anakihelehele..
BAE anatakiwa kuwa mashamba kidogo.
0 comments:
Post a Comment