juu

Monday 2 December 2019

Je wewe ni mrahisi au maharage ya Mbeya, maji mara moja?

Image may contain: 1 person, closeup
Siku hizi kumekuwa na utamaduni wa wasichana kuwa na utitiri wa mabwana (madanga) wakihisi wanawachuna na kuwalia pesa zao kumbe wao ndio wanachunika bila kujua hatma ya maisha yao.

Mara nyingi dada zetu wanaofanya huo mchezo wanawaza wasikubali kwa haraka kama wanatabia ya udangaji kwakuwa hawasimami mabarabarani kusubiri au kuwatafuta wanaume. Ila kama umekuwa ni mtu usiye na msimamamo juu ya maisha yako na kuheshimu thamani na utu wako na unaruhusu kila mwanaume aonje utamu wako kizembe zembe, basi ujue wewe ni maharage ya Mbeya, maji mara moja

Ukitaka kuamini kwamba wewe ni mrahisi au maharage ya mbeya, soma tabia hizi. Ikiwa unatabia moja kati hizi ujue wewe ni MAJI MARA MOJA.

1. Kama ulikuwa na wapenzi siku za nyuma na ukadumu nao kwenye mahusio kwa muda kadhaa na mkaachana kwa sababu mahusiano hayo hayakuwa na tija, hayakuwa na malengo ya kudumu, yalikuwa mahusiano yenye kero, mateso, usaliti nk, kisha baada ya siku, mwezi au miaka kadhaa ukarudiana na watu wa aina hiyo bila kujali waliyokufanyia siku za nyuma, basi wewe ni MAHARAGE YA MBEYA.

2. Kama umekuwa ni mtu wa kupokea pokea vijizawadi kutoka kwa wanaume usiowajua undani wao hazma zao juu ya zawadi zao ila wewe unapokea tu kwa tamaa zako, basi wewe ni MAHARAGE YA MBEYA.

3. Kama unatabia ya kugawa gawa namba zako za simu hovyo hovyo kwa wanaume usio wajua bila kujali lolote, wewe ni MAHARAGE YA MBEYA.

4. Kama umepelekwa kutambulisha kwa mpenzi au mume wa rafiki yako na mwisho wa siku ukajilegeza legeza kwa mume wa rafiki yako ukampa uroda, wewe ni MAJI MARA MOJA.

5. Kama unatabia ya kutoka kimapenzi na mwanaume siku ya kwanza tu baada ya kutongozwa au kuona naye bila kijali afya yako, heshima yako, utu na thamani yako, wewe ni MAHARAGE YA MBEYA, MAJI MARA MOJA.

6. Kama unatabia ya kuunganishwa na wanaume usiowajua, wanapewa namba zako, wanakutafuta wanakutongoza, unakubali kwa kigezo cha kupewa namba zako na rafiki yako. Wewe ni MAHARAGE YA MBEYA.

7. Kama unatabia ya kuomba omba pesa hovyo kwa wanaume unaokutana nao siku chache baada ya kufahamina kwa juu juu. Wewe ni MAJI MARA MOJA.

8. Kama unatabia ya kujipendekeza na kushoboka kwa wanaume wenye mali, pesa au elimu zao bila kujali umuhimu na thamani yako. Wewe ni MAJI MARA MOJA.

9. Kama unakawida ya kutolewa out na wanaume usiwajua, ila tu uanataka ukatumie vyakwao. Wewe ni MAJI MARA MOJA.

10. Kama hujui kukataa unapotongozwa na kukiri kuwa upo kwenye mahusiao au kwenye ndoa, wewe kazi yako ni kucheka cheka na kuwaahidi wanaume kuwa utawafikiria. Wewe ni MAHARAGE YA MBEYA, MAJI MARA MOJA.

Dada zangu takwimu za watu wanoingia kwenye ndoa zinazidi kushuka siku hadi siku, labda ni kutokana na ulegevu wenu kwa wanaume na kutokuwa na msimamo.

Sifa ya wife material ni kuwa thabiti katika maisha yake kwa ujumla. Ukiwa ni msichana usiyejua hatma ya maisha yako, utakuwa kipozeo cha wanaume wakware.

Jiheshimu, jipende, jitunze, jikubali, jithamini na kutambua umuhimu wa wewe kuwepo katika dunia hii, utafurahie raha ya maisha yako. Acha kujikatia tamaa, acha kuishi kwa mitazamo na fikra za watu walioshindwa maisha, anza upya bado unanafasi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger