juu

Friday, 6 December 2019

Namna Ya Kuondoa Wasiwasi Wa Kufanya Tendo La Ndo

Related imageWakati kila mmoja wa wahanga angependa kupata kitu cha kumwondolea tatizo hili mara moja, ukweli ni kwamba, kama ilivyo kwa wasiwasi wa aina nyingine, si swala la kulifanyia kazi kwa muda mfupi. Mtu ye yote anaweza kuondokana na tatizo hili, ila inahitajika juhudi, kujituma, na kuchukua hatua sahihi. Hapa chini ni baadhi ya hatua za kuchukua katika jitihada za kuondokana na tatizo hili:

. Kumweleza Mpenzi Wako Kuhusu Tatizo

Njia moja ambayo si sahihi katika kuepukana na tatizo hili ni kujaribu kupambana nalo bila kumwambia mpenzi wako. Hatua hii italifanya tatizo lako kuwa kubwa zaidi, na utakuwa kila wakati unayatuma mawazo yako kwenye kuchunguza kila kinachoendela kila wakati.







Kuwa jasiri na kumwambia mwenzio kabla ya kuanza tendo la ndoa kwamba unasumbuliwa na wasiwasi wakati wa tendo na jinsi unavyojisikia. Uwezekano ni mkubwa sana kwamba mwenzi wako atakuelewa na kwa pamoja mtalifanyia kazi tatizo hilo.

. Jenga Upendo

Kimsingi, mtu uliye naye leo anaweza akawa ni mpenzi wako wa kudumu. Uzoefu – na hasa wa kuwa na mtu mmoja – ni tiba ya wasiwasi wa kufanya mapenzi. Hii inatokana na kuwa akili yako itakutuma kuamini kuwa, lo lote litakalokuwa, mwenzi wako bado ataendelea kuwa na wewe. Imani hiyo itakupunguzia woga ya kuwa wasiwasi wako wa kumudu kufanya mapenzi utakuja kukuharibia maisha yako.

. Ondoa Aibu Ya Kufanya Maandalizi

Wakati ambapo wanaume na wanawake wengi wanapata shida kushiriki maandalizi wakiwa na wasiwasi wa kufanya mapenzi, wengi bado wanaweza kujitahidi. Kiasi kikubwa cha wasiwasi kinakuwa kuhusu mwenzi anafurahia kwa kiasi gani tendo lenu. Unaweza kupunguza wasiwasi huu kwa kujitahidi kushiriki zaidi katika maandalizi, hivi kwamba, hata kama kiwango chako katika tendo hakikufikia pale mwenzi alipotegemea, bado utakuwa umemridhisha.

. Fanya mazoezi

Kuwa na kujiamini kimwili na nguvu za kutosha ni swala muhimu katika kuondoa wasiwasi wa kushindwa kufanya mapenzi kutokana na wasiwasi. Kadri unavyopunguza mawazo ya jinsi ulivyo au ya mwonekano wako, ndivyo utakavyoweza kushiriki tendo la ndoa bila ya kuwa na msongo wa mawazo. Fikiria mazoezi mazuri ya kuyafanya kama bado ulikuwa hufanyi, kuhakikisha kuwa unafikia hali ya juu ya kujiamini.

. Poteza Mawazo

Jaribu kuondoa mawazo ya kujifikiria na kuyarudisha kwenye shughuli iliyo mbele yako kwa kuweka muziki wa kimahaba au mkanda wa mapenzi wakati ukifanya mapenzi. Chagua kitu ambacho kinakuletea hisia. Kuondoa mawazo kutoka kwenye kulimudu tendo la ndoa kunaweza kukupunguzia wasiwasi unaokuzuia usipate ashiki.



Usisite kuuliza swali lo lote kuhusiana na mada yetu ya leo na tunakaribisha maoni yako kuhusu mada hii. Tutafurahi sana kukujibu na kwa wakati.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger