juu

Sunday 1 December 2019

SMS nzur iZa kumtumia mpenzi wako kumuonyesha unavyompenda

Related imageT.gifMeseji ya kumwambia mpenzi wako kuwa ulimpenda tangu siku ya kwanza na utazidi kumpenda

nilivyokutana nawe siku ya kwanza nilikupenda kwa
dhati,nikakueleza ukweli ukanikaribisha moyoni
mwako,siwezi kuchezea nafasi hiyo laaziz,nitakushika
daima.

🔥♥♥♥


T.gifMeseji nzuri ya salamu kwa umpendaye

Pokea sms yangu iliyojaa utamu, nimeipamba kwa maneno laini yenye ladha adimu, utamu wake ni kama apple haufanani na ndimu, nimeituma kwako sms hii ikuletee salamu "UHALI GANI MPENZI?"

🔥♥♥♥


T.gifSMS nzuri ya mapenzi ya kutakia usiku mwema

Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka.
Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika.
Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka.
Kitale katikati yake ukila utaridhika.
Matamu na maji yake hukata kiu haraka.
Weupe watui lake lina ladha ukipika.
Kupaka mafuta yake mwili hulainika.
Na kwenye machicha yake kazi nying hufanyika.
Hata na upepo wake uvumapo utacheka.
Sikijui kitu chake kipi kisichotumika.usiku mwema

🔥♥♥♥


T.gifSMS ya kimahaba kumwambia mpenzi wako kuwa yeye ni ndoto yako

Nilikuwa nikifiria kwamba ndoto haziwezi kuwa kweli,
lakini nilibadili mawazo yangu pale tu nilipokuona wewe.

🔥♥♥♥


T.gifSMS ya kimahaba ya kumwambia mpenzi wako yeye ndiye yupo kwenye ubongo wako

Bongo zenye fikra kali huwa na mawazo, suluhu na sababu;
ubongo wa kisayansi huwa na kanuni, nadharia na takwimu;
wangu una wewe tu!

🔥♥♥♥


T.gifSMS nzuri ya kumtumia mpenzi wako kumuonyesha unavyompenda

Naweza kukuazima mabega yangu upande, masikio yangu usikilizie mikono yangu ushikie, miguu yangu, utembelee, lakini si moyo wangu kwani tayari unao wewe.

🔥♥♥♥


T.gifSMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye

Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.

🔥♥♥♥


T.gifUjumbe wa kumtumia mpenzi wako wakati anahuzuni kumwambia kuwa uko kwa ajili yake

Nitafute wakati una huzuni, nitafute wakati hamna wa
kukusikiliza. Sijali kama mimi ni kimbilio lako la mwisho,
bali sipendi ulie peke yako.

🔥♥♥♥

Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger