juu

Sunday, 8 December 2019

Suluhisho Rahisi Kwa Wanaodhani Wamepungukiwa Nguvu, Wanaosumbuka Kurudia Tendo au Kuwahi Kufika



Inavyoonekana siku hizi japo kweli kuna tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haswa kwa mazingira ya mijini, Lakini hili tatizo linaonekana kukuzwa kuliko lilivyo hadi imepelekea woga mkubwa kwa baadhi ya wengi wetu.

Kwa kuanzia yafuatayo yaweza kusaidia kuboresha kulifurahia tendo la ndoa zaidi na kwa muda zaidi.

Kuuweka Mwili vizuri: Ni wazi kuwa tendo hili linachagiwa sana na mzunguko mzuri wa damu. Mwili ukiwa kwenye hali nzuri kiafya na tendo huwa linaenda ipasavyo. Na mwili ukiwa dhoofu basi tegemea tukio dhoofu pia. Hivyo ukitaka kuwa na matokeo mazuri kwenye ndoa yako, jitahidi sana kujiweka vizuri kwa kula sahihi na kufanya mazoezi mepesi mepesi tu kwa wale wanaoweza kuutumia muda vizuri wapiti pite Gym walau siku mbili na kuendelea kwa wiki.

Kufahamu kuwa kupumzika kwa uume baada ya baada kufika mara ya kwanza sio tatizo. Kwa wanaume walio wengi, baada ya mshindo wa kwanza hupumzika kidogo kabla ya kuendelea na awamu nyingine. Japo kuna ambao wana uwezo wa kuendelea moja kwa moja bila kupumzika (law ya use and misuse inahusika kwa wengine apa). Kwa hio kusinyaa kwa uume baada ya mshindo wa kwanza, isifahamike kuwa ni upungufu wa nguvu bali ni ajdustiment ya mwili wenyewe kutokana na kwamba mwanaume kabla ya tendo mapigo ya moyo huongezeka na huchangia damu kwenda kwa kasi, na kwa hali hio anakua yupo juu sana kimhemko, inapofikia anamaliza raundi ya kwanza mwili unakua unapoa /umesharudi kwenye hali yake ya kawaida, ndiko kunakosababisha hio maneno kusinyaa kwa wengi wakati mapigo ya moyo yanaporudi kawaida (MWILI KUPOA).

Maandalizi ya mwili. Wanaume tupo tayari muda wote… ila linapokua swala ya mwenza wako (kwa kuwa muda unaotumia kwa maandalizi na tendo una uhusiano wa moja kwa moja na satisfaction ya mwenzio)… unahitaji muda angalao nusu saa na kuzidi kujiandaa na mwenzi wako. Kama timu ya mpira inapoenda ugenini huhitaji muda kuzoea mazingira, ndio na mwanaume anavyohitaji muda kuzoea mazingira ya ugenini. Hili linakusaidia sana mwanaume kutoka kwenye mihemko na kurudi kwenye hali yako ya kawaida ambayo itakusaidia kuwa na muda mzuri zaidi wa kufurahia tendo. Jitahidi pia kuvuta pumzi nyingi ndani na uiachie polepole kukusaidia kukuweka kwenye utulivu mzuri.

Timing ya kuanza tendo: Kwa kuwa tendo linahusisha sana hisia za mwili, ukiwa umetumia muda unaotosha kuandaana, basi usiwe na papara mwanzoni, bali uwe na utulivu, pia jitahidi kuzungumza moja mawili wakati unaanza kuzoea mazingira mengine (core business) EPUKA UHARAKA na kuweka sana akili yako hapo, jinafikie mwenyewe kuwa its just a normal thing (mental pride)

Concetration/ Umakini uliopitiliza: Unapaswa kumfanya mkeo aweke akili yake yote hapo, na wewe unatakiwa katika kumuweka mkeo kwenye concentration uuharibu umakini wako (level of concentration). Ukiweka concentration ya juu sana kwenye tendo… haikuchukui dakika mbili umemaliza, na kuirudisha tena ile hali ya concentration uliokua nayo mwanzo itakuwia ngumu sana….. Usiweke sana akili yako hapo kama unataka kufurahia kwa muda zaidi. ila kama hutaki kudumu.. weka akili na umahini wako hapo woote.. just seconds or a minute you are done

MAZOEZI ya mwili ni muhimu sana sana sana sana sana kwetu wanaume. Kama huna muda wa kwenda jimu walau ukiamka piga ‘PUSH-UPS walau 50'' kila siku na ‘'SQUARTS'' . haya ni mazoezi mepesi lakini ni BORA zaidi kwa mwanaume. Kwetu sisi wanaume tunatumia sana misuli yetu wakati huu, kwa hio kuna ulazima wa kutafuta ustahimilivu wa misuli ''mussle strength n perseverance''. Hio kitu ni starehe na unatakiwa baada ya tendo uwe umekuwa refreshed na sio uwe unaumwa kila mahali na sijui joints zinauma sijui nini nini? ukijiona unakuwa hivyo baada ya tendo ujue mwili wako haujakaa fiti ipasavyo kimazoezi/kiafya

Pia Afya ya Akili inahusika sana, Japo inahitaji jitihada makhususi... lakini kila mtu ana uwezo wa kuchagua nini cha kufikiria na nini si cha fikiria(kupuuzia) na pia akienda hatua zaidi anaweza kupuuza kila kitu kwa wakati fulani kama unajua una huo uwezo na ukaamua kuutumia. Pia kuchagua kufikiri yale yaliopo kwenye uwezo na urefu wa kamba yako pekee; vitu usivyo na uwezo navyo utajisumbua tu bure na kujipa stress zaidi. Weka nguvu na jitihada zako kwenye kutafuta ufumbuzi wa changamoto zako, jifunze na acha kufikiria matatizo kwa maana hakubadilishi kitu na yataendelea kuwa hivyo n.k n.k................ Ukiwa na namna nzuri ya kuyachanganua mambo yako utasaidika sana kwenye afya ya akili yako na kuwa vizuri zaidi

Karibuni wadau kusaidia utatuzi wa hili jinamizi linalojizolea umaarufu kadiri siku zinavyokwenda kwenye jamii yetu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger