1.Huimarisha uhusiano na kuongezeka mapenzi ya kweli
Pindi utoapo zawadi kwa mwenzi wako, mwenzi huyo hujihisi yeye ni wa thamani sana mbele yako. kwani zawadi kutafsiriwa na mpokeaji kama ni mtu wa thamani sana, mtu ambaye anapendwa kweli . hivyo pindi ufanyapo kitendo cha utoaji wa zawadi yeyote ile kwa mwenzi wako, hufanya mahusiano yenu yaimarike na si kuteteleka.
2. Humfanya mtu ajihisi yupo mahali salama.
Usishangae huo ndio ukweli, kama ulikuwa hauna kawaida ya kumpa zawadi mpenzi wako basi anza kufanya hivyo mara moja. Kwani zawadi hutafsiwa na mpokeaji ya kwamba yupo mahali sahihi. Hivyo ili kuweza kuudumisha upendo wako na mwenzi wako jenga utaratibu wa kumpa zawadi mpenzi wako.
3. Zawadi huacha kumbukumbu.
Hakuna kitu ambacho huacha alama kubwa katika mahusiano kama zawadi. Hivi hajawahi kukutana na mtu anamwambia ya kwamba kitu hiki alinipa fulani? Bila shaka umewahi kukutana na mtu wa aina hiyo. Kama ndivyo hivyo amini ya kwamba zawadi huacha alama katika mahusiano.
Na ili kuacha alama hiyo, kama nilivyosema hapo awali ua kwamba zawadi ni lazima iwe ni ya kudumu. Pia kabla sijaweka nukta nikumbushe pande zote mbili mvulana na msichana ana haki ya kutoa zawadi kwa mwezi wake. Hivyo nikusihi ya kwamba ujijengee utaratibu wa kutoa zawadi kwa mwezi wako.

0 comments:
Post a Comment