juu

Wednesday 21 August 2019

Hivi Unaujua Muda Sahihi wa Kufanya Tendo la Ndoa?


Somo hili linaweza kukushangaza msomaji wangu, kutokana na ukweli kwamba
ufanyaji mapenzi, hauwezi kuupangia muda, lakini katika hali ya kawaida ipo tofauti kubwa ya kufanya mapenzi, mchana, usiku, alfajiri na nyakati za joto na kelele nyingi za wapita njia.

Utofauti huu ndiyo unaweza kutofautisha hali ya kufurahia tendo kati ya mtu na mtu. Hakuna ubishi kwamba watu wanaofanya mapenzi nyakati za joto, hupoteza msisimko wa tendo si tu kwa sababu ya kuchoka haraka bali hata kwa kukinai harufu ya jasho liwatokalo mwilini.

Sababu hiyo na nyingine nyingi, zitokanazo na kutojua muda sahihi wa kufanya tendo la ndoa, zimewafanya wapenzi wengi kushindwa kuridhika au kupata raha stahili wakati wa kujamiiana na wapenzi wao, jambo ambalo linanipa sababu ya kufundisha muda sahihi wa kufanya mapenzi ni upi?

Hata hivyo, muda huo ulikubaliwa na wengi si tu kwa sababu una utulivu wa hali na mazingira, lakini pia ni wakati ambao hisia za mapenzi huamka kwa watu ambao pengine walikuwa na majukumu ya kazi mchana kutwa. Ukichunguza utabaini kuwa wanandoa wengi nyakati hizi huwa faragha na hata mafumanizi mengi hutokea kati ya saa 3 na saa 4 usiku.

Inaelezwa kwamba mwanaume hufikiria tendo la ndoa mara 13 kwa siku takribani mara 5,000 kwa mwaka tofauti na mwanamke ambaye anatajwa kufikiri mara 5 kwa siku na 1,825 kwa mwaka, mawazo ambao yote yamebainika kutekelezwa zaidi nyakati za usiku kwa muda huo niliotaja.

Ifahamike kuwa kinachozungumzwa katika makala haya si uwezo wa kufanya tendo la ndoa, bali ni matokeo sahihi. Watu wengi wanaweza kulima, kufanya kazi, kufanya biashara, kucheza na hata kusoma nyakati za joto, baridi sana na hata usiku na wakapata matokea, lakini kitalaamu litakuwepo swali wamepata matokeo mazuri, wamefurahi sawa na wale
waliochagua muda sahihi?

Huu ndiyo ujumbe wangu kwa leo, ni vema wapenzi wakafanya uchunguzi na kufahamu ni muda gani mzuri kwa mazingira ya kwao kufanya tendo la ndoa, vinginevyo wanaweza kufanya lakini wakajikuta wanakinai mapema au wakapata raha kidogo.




Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger