Kwa nini watu wengi huwa tunafikiria kuwa ndoa ndio itatupatia furaha?
Napenda kuona ndoa zilivyo na muungano mzuri, zinatumia mapatano– ambamo kuna sheria zinazohusu uchumi na faida au kusimamia jamii au kuleta uzalishaji. na kuwa na watoto.
Lakini siku hzi i watu wanaamua kuolewa au kuoa kisheria kwa malengo yao binafsi watu wengi sana hufanya hivyo kwa nia ya kuishi pamoja na kuwa na mahusiano ya kudumu.
Ingawa kuna wanawake wengi wameolewa kwa makusudi ya kwao . na wapo ninaowafahamu ambao wanategemea waume zao wawape furaha. Huenda kwa kujua au kutokujua , mambo yanapokuwa magumu , na mara nyingi wanafanya , badala ya kuangalia ni wapi wanakosea , wanawanyoshea vidole wanaume., wanalaumu kwa kuleta matatizo katika mahusiano .
Wanasema kama mwanaume angenisikiliza mahusiano yetu yangekuwa ni mazuri. Au kama angekuwa anasaidia kazi nilizonazo nyumbani mambo yangekuwa mazuri.
Wanaongeza mambo mengi yasio na maana kwa kuendelea kuwalaumu wanaume , na matokeo yake wanakosa hamu ya tendo la ndoa . hio yote ni sababu ya kulalamika na kufikiria mambo tofauti. Mara nyingi wanakataa hata kushiriki tendo la ndoa.
‘’Atapika mwenyewe’’
‘’Sitashiriki tendo la ndoa mpaka hapo atakapoomba msamaha’’
‘’Atafua mwenyewe manguo yake’’
‘’Sitafanya anachokitaka, nipo sahihi na yeye ndiye ana makosa.’’
Hawa wanawake huachia haya mambo madogo yawe sumu kwenye mahusiano, kubishana kwa mambo madogo yanakuwa ni tabia ya kila siku inayozidi kuharibu.
Lakini kubishana huko kuhusu vyombo sio kweli.
Ni kwa sababu wanaona hakuna mtu wa kuwajali. Hisia zao zinachukua nafasi ya, Lakini wanajisikia kutopendwa hata kidogo na wenza wao.
Inatokea mara nyingi hawa wanawake, hata kama wana uwezo , wako smart namna gani , wengi wao wako huru, wanaamini mambo ya ajabu kwamba kama wasiposhiriki tendo la ndoa , wenza wao watafahamu ni kitu gani wanahitaji kutoka kwao
Hawajui kama ndio itakuwa mbaya zaidi, na kupata maumivu zaidi.
Ni kama kuweka stika za kinabii za kizamani; kwamba vita itaendelea kwa kutaka uhakika . lakini hakuna uhakika utakaopata.
Usimfanyie mtu kitu kibaya kama hicho kwa kutaka akufanyie unachotaka, tena hakuna mahusiano ya aina hio yenye afya nzuri, ni bora kuaminiana na kupata salama.
Unaweza kupiga kelee, kupigana, kushikilia, unaweza kukaa nalo kwa kuhukumu na kujiona una uhalali. Unabaki kwenye kichwa chako kujiona uko sahihi kumbe hauko sahihi ni mbinafsi na hupati kitu chochote.
Lakini hebu ngoja nikuulize: Tabia hio inafanya kazi kwako?
Unapata kweli kile ambacho unakitaka?
Najua hii inakushangaza , niliwahi kuwa hivyo, na sikuwahi kufaidika na kitu chochote zaidi ya kupata magonjwa ya kujitakia., nilikuwa na hasira, maumivu, sioni kitu, na sikuwa nasikia, pia sikuwahi kuhisi kuwa mme wangu ananipenda vya kutosha .
Kitu gani nilichokifanya? Nilitazama nyuma. Nilitazama na kuona kuwa nimefanya mambo ya kijinga, ya ukichaa. Nilianza kufikiria kwa nini nilifanya ujinga wa kumpa adhabu mume wangu, kwa kutaka anifanyie kitu ambacho nilikuwa nakitaka? Kitu ambacho hata kama ningeendelea nisingekipata.
Nitakaje upendo, mapenzi, usikivu na kutukuzwa endapo mimi sifanyi hayo yote. Ni mbinafsi.
Kwa nini wengi wetu tunafanya hivi? Kwa nini unafanya haya?
Wanawake, Kama unataka kuwa na furaha kwenye ndoa yako , iwe ndio kazi yako ya kumfanyia mume wako awe na furaha ( au mke wako awe na furaha)
Acha kusubiri mtu fulani aanze kufanya hivyo. Anza wewe kufanya hivyo, achilia moyo wako, upendo wako, ukarimu wako, ukweli wako . furaha ni yako kamilisha hio.
Unaweza ukawa na mume mwema, mpole, muelewa , lakini ukawa unamsuukumia mbali ,, matokeo yake unaumia wewe mwenyewe.
Baada ya kugundua haya badilika leo , sasa hivi. Usimpe adhabu mume wako mkewako eti kwa sababu ya kutaka akukamilishie kitu unachokitaka. Matokeo yake mtakuwa mnasukumiana lawama zisizo na maana.
Amua kufanya mambo ambayo yanawapa furaha wote wawili na kuhisi vizuri kulea ndoa yenu. Kujaribu kubadilika wewe mwenyewe ni vitendo vinavyoonyesha upendo wa pekee.
Inaweza kukuchukua muda mrefu kuelewa hili lakini ni maamuzi tu.
Fahamu kuwa upendo unaanza na wewe. Na kila kitu kinaweza kubadilika.
Kama unakubali kufanya kazi na kuweka mapenzi ndani yake; na kama utaamua kufungua moyo na kufahamu kuwa upendo unaanzia ndani yako. Na ni kazi yako kumfanya mume wako awe na furaha . kujikubali kutabadilisha mahusiano yako.
0 comments:
Post a Comment