Maumivu haya yaweza kuwa;
– Wakati tu uume unaingia
– Unapoingiza kitu chochote hata kidole
– Wakati uume ukiwa ndani
– Maumivu ya kupwita (throbbing pain) yanayodumu masaa kadhaa baada ya tendo.
Sababu za maumivu
Sababu zaweza kuwa za kimwili (physical) au za kisaikolojia.
Sababu za kimwili baadhi ni kama;
Kutokua na ute wa kutosha kwa ajili ya kulainisha uke kutokana na kukosa maandalizi ya kutosha, kupungua kwa homoni baada ya ukomo wa hedhi, kujifungua au kunyonyesha, baadhi ya dawa za magonjwa ya akili, presha na uzazi wa mpango.
Ajali au upasuaji maeneo ya nyonga, ukeketaji na kuongezewa njia wakati wa kujifungua. Pia matibabu ya kutumia mionzi eneo la nyonga.
Tatizo la mishipa ya uke kusinyaa yenyewe (Vaginismus).
Tatizo la uumbaji linalopelekea mtu kuzaliwa wakati uke haujatengenezwa vizuri mfano “vaginal agenesis na imperforate hymen.”
Magonjwa ya kizazi kama “endometriosis, PID,fibroids.”
Sababu za kisaikolojia baadhi ni kama; msongo wa mawazo, wasiwasi, sonona, matatizo ya mahusiano, woga wa mimba, historia ya kuumizwa kimapenzi (sexual abuse) siku za nyuma.
0 comments:
Post a Comment