Wiki hii nataka kuzungumzia mada ya kitaalam zaidi kuelezea swali ambalo nimekuwa nikiulizwa na wasomaji wangu kwamba, kwanini mume ana hamu kubwa ya kufanya mapenzi kuliko mke.
Kama wewe ni mfuatiliaji wa karibu wa safu hii utakumbuka niliwahi kuzungumzia faida za kufanya tendo la ndoa. Naamini wapo ambao walikuwa wakizifahamu faida hizo lakini pia, kuna ambao walishtuka kusikia kuwa kufanya tendo la ndoa kuna faida nyingi zaidi ya kustarehesha kama wengi wanavyojua ukiachilia mbali kwamba wapo wanaofahamu kwamba, kufanya tendo hilo ni kwa ajili ya kutafuta mtoto tu.
Wapo ambao walipofahamu kwamba, kufanya ngono kuna faida hizo, wamekuwa wakiongeza ‘usumbufu’ kwa waenzi na wanandoa wenzao hali ambayo imesababisha kuwepo kwa mvurugano ndani ya ndoa nyingi. Tukumbuke kwamba kila kitu kikizidi sana kina athari zake, wazungu wanasema ‘Too much is harmful’. Hivyo licha ya kuwepo na faida hizo za kufanya tendo la ndoa lakini inabidi tusizidishe sana. Tufanye kwa utaratibu ili tuweze kuzipata faida hizo badala ya matatizo.
Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wanawake wakielezea kukerwa na tabia za waume zao kuendekeza sana tendo la ndoa. Hali hii imewafanya wanawake wengine kufikia hatua ya kuomba talaka kutoka kwa waume zao kutokana na kushindwa kuhimili vishindo japo si wote wanaoidai talaka kukimbia kero za ngono.
Ndiyo maana wengi wamekuwa wakieleza kwamba, wanaume wamekuwa na hamu kubwa zaidi ya kufanya mapenzi kuliko mwanamke. Lakini sasa mbona kuna baadhi ya wanawake ambao nao wana hamu kubwa ya kufanya mapenzi kuliko wanaume?
Wapo wanawake ambao kila wakati wanataka kufanya tendo la ndoa na usipowatimizia hulazimika kwenda nje hali ambayo ni hatari. Wanawake hao wamepewa majina ama misemo kuwa ‘Wana pepo wa ngono’.
Hata hivyo, wengi tumekuwa tukifahamu kwamba, wanaume wengi wana hamu kubwa ya kufanya mapenzi kutokana na kuyaabudu kuliko kitu chochote katika maisha yao. Ni wazi wapo wanaume ambao ikipita siku bila kufanya mapenzi wanaumwa na wenyewe wanakiri hivyo.
Watu hawa wapo huko mitaani na hii hutokana na kuiga pamoja na kukosa kazi za kufanya. Unapokuwa huna kazi ya kufanya ni rahisi sana fikira zako kuzielekeza kwenye ngono na hivyo kulazimika kila wakati kujisikia kufanya hivyo.
Lakini pia wakati mwingine hali hii hutokana na ulimbukeni wao tu kwamba wanataka waonekane vidume. Kama hamu kubwa ya kufanya mapenzi inatokana na sababu hizo, ni rahisi sana kuondokana na tabia hiyo ya kuendekeza ngono kwa kubadili mfumo wa maisha yako.
Fahamu kwamba unaweza kubadilika kama utahitaji kubadilika katika hili. Kinachowafanya wanaume kuwa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi kuliko wanawake ni kutokana na sababu za kibaiolojia.
Inaelezwa kuwa, mwanaume ana testosterone homoni (Viamshi) ambayo huzalishwa kwa wingi katika kende hivyo kutokana na kuwepo kwa kiasi kikubwa cha homoni hiyo humfanya kuwa na mhemko mkubwa na hisia nyingi za kufanya mapenzi.
Homoni za estrogen kwa upande wa mwanamke huwepo kwa kiasi kikubwa wakati fulani katika mzunguko wa hedhi na hasa siku ya upevushaji wa yai ‘Ovulation’ ndipo mwanamke anapokuwa na joto. Mara nyingi mwanamke huhitaji sana kuamshwa hamu ya kufanya mapenzi kwa kushikwashikwa sehemu zinazosisimua zaidi.
Tofauti na wanaume walio wengi ambao hamu zao hazihitaji kuamshwa. Wapo ambao wanapowaona wanawake tu wakiwa wamevaa nguo zinazoonesha maungo yao, hujihisi kufanya mapenzi. Mwanamke yeye anaweza kumuona mwanaume ‘handsome’, mwenye kifua kizuri na vigezo vingine ambavyo wanawake wengi huangalia, lakini huwezi kumkuta akipatwa na hamu ya kufanya mapenzi.
Inaelezwa kwamba tendo la ndoa ni maridhiano baina ya wanandoa wote sasa kama itatokea mmoja kuwa na hamu kubwa zaidi kuliko mwenzake lazima kitu fulani kifanyike ili kuinusuru ndoa la sivyo ndoa itayumba kama siyo kusambaratika kabisa. Nini kifanyike? Tukutane kesho katika muendelezo wa makala haya.
usikose mwendelezo wa sehemu ya pili
0 comments:
Post a Comment