juu

Thursday, 5 December 2019

Mambo Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuoa Au Kuolewa

Related image

1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa ni ya maisha yote.

2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada ya Ndoa.

3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema.

4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi fanywa na mtu yeyote.

5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.

6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama kuolewa na mtu asiye sahihi.

7.Furaha ya kudumu maishani hutegemea na chaguo lako la mwenzi ktk Ndoa.

8. Usioe/kuolewa na pesa au mali. Oa/Olewa na mtu. Pesa/Mali hufilisika lakini utu hudumu milele.

9. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa isiyo na amani wala furaha.

10. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa.

11. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa sababu tu anakidhi haja zako kingono.

12. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki wema. Vivyo hivyo kwa marafiki wabaya
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger